< Timotheum Ii 3 >

1 Hoc autem scito, quod in novissimis diebus instabunt tempora periculosa:
Lakini fahamu hili: katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati ngumu.
2 erunt homines seipsos amantes, cupidi, elati, superbi, blasphemi, parentibus non obedientes, ingrati, scelesti,
kwa sababu watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye majivuno, wenye dhihaka, wasiotii wazazi wao, wasiokuwa na shukurani na waovu.
3 sine affectione, sine pace, criminatores, incontinentes, immites, sine benignitate,
Wasio na upendo wa asili, wasiotaka kuishi kwa amani na yeyote, wachonganishi, wasingiziaji, wasioweza kujizuia, wenye vurugu, wasiopenda mema.
4 proditores, protervi, tumidi, et voluptatum amatores magis quam Dei:
Watakuwa wasaliti, wakaidi, wenye kujipenda wenyewe na wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.
5 habentes speciem quidem pietatis, virtutem autem eius abnegantes. Et hos devita:
Kwa nje watakuwa na sura ya ucha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe na watu hao.
6 ex his enim sunt, qui penetrant domos, et captivas ducunt mulierculas oneratas peccatis, quæ ducuntur variis desideriis:
Kwa kuwa baadhi yao ni wanaume wanaoingia kwenye familia za watu na kushawishi wanawake wajinga. Hawa ni wanawake waliojawa dhambi na wenye kuongozwa na tamaa za kila aina.
7 semper discentes, et numquam ad scientiam veritatis pervenientes.
Wanawake hawa hujifunza siku zote, lakini kamwe hawawezi kuufikia ufahamu wa ile kweli.
8 Quemadmodum autem Iannes, et Mambres restiterunt Moysi: ita et hi resistunt veritati, homines corrupti mente, reprobi circa fidem,
Kama vile ambavyo Yane na Yambre walisimama kinyume na Musa. Kwa njia hii walimu hawa wa uongo husimama kinyume na kweli. Ni watu walioharibiwa katika fikira zao, wasiokubalika kuhusiana na imani.
9 sed ultra non proficient: insipientia enim eorum manifesta erit omnibus, sicut et illorum fuit.
Lakini hawataendelea mbali. Kwa kuwa upumbavu wao utawekwa wazi kwa watu wote, kama ulivyokuwa wa wale watu.
10 Tu autem assecutus es meam doctrinam, institutionem, propositum, fidem, longanimitatem, dilectionem, patientiam,
Lakini wewe umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu na ustahimilivu wangu,
11 persecutiones, passiones: qualia mihi facta sunt Antiochiæ, Iconii, et Lystris: quales persecutiones sustinui, et ex omnibus eripuit me Dominus.
mateso, maumivu na yaliyonipata kule Antiokia, Ikonio na Listra. Niliyavumilia mateso. Bwana aliniokoa katika yote hayo.
12 Et omnes, qui pie volunt vivere in Christo Iesu, persecutionem patientur.
Wote wanaotaka kuishi katika maisha ya kumcha Mungu katika Kristo Yesu watateswa.
13 Mali autem homines, et seductores proficient in peius, errantes, et in errorem mittentes.
Watu waovu na wadanganyifu watazidi kuwa waovu zaidi. Watawapotosha wengine. Wao wenyewe wamepotoshwa.
14 Tu vero permane in iis, quæ didicisti, et credita sunt tibi: sciens a quo didiceris.
Lakini wewe, dumu katika mambo uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti. Kwa kuwa unajua umejifunza kwa nani.
15 Et quia ab infantia sacras litteras nosti, quæ te possunt instruere ad salutem, per fidem, quæ est in Christo Iesu.
Unatambua ya kuwa tangu utotoni mwako uliyajua maandiko matakatifu. Haya yanaweza kukuhekimisha kwa ajili ya wokovu kwa njia ya imani katika kristo Yesu.
16 Omnis Scriptura divinitus inspirata utilis est ad docendum, ad arguendum, ad corripiendum, et erudiendum in iustitia:
Kila andiko limetiwa pumzi na Mungu. Linafaa kwa mafundisho yenye faida, kwa kushawishi, kwa kurekebisha makosa, na kwa kufundishia katika haki.
17 ut perfectus sit homo Dei, ad omne opus bonum instructus.
Hii ni kwamba mtu wa Mungu awe kamili, akiwa amepewa nyenzo zote kwa ajili ya kutenda kila kazi njema.

< Timotheum Ii 3 >