< Petri Ii 2 >

1 Fuerunt vero et pseudoprophetæ in populo, sicut et in vobis erunt magistri mendaces, qui introducent sectas perditionis, et eum, qui emit eos, Dominum negant: superducentes sibi celerem perditionem.
Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe.
2 Et multi sequentur eorum luxurias, per quos via veritatis blasphemabitur:
Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli.
3 et in avaritia fictis verbis de vobis negotiabuntur: quibus iudicium iam olim non cessat: et perditio eorum non dormitat.
Kwa uchoyo watawanyonya watu wakitumia maneno ya uongo Hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata.
4 Si enim Deus angelis peccantibus non pepercit, sed rudentibus inferni detractos in Tartarum tradidit cruciandos, in iudicium reservari. (Tartaroō g5020)
Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia. (Tartaroō g5020)
5 Et originali mundo non pepercit, sed octavum Noe iustitiæ præconem custodivit, diluvium mundo impiorum inducens.
Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani. Bali, alimhifadhi Nuhu, mwenye wito wa haki, pamoja na wengine saba, wakati alipoachila gharika juu ya ulimwengu ulioasi.
6 Et civitates Sodomorum, et Gomorrhæorum in cinerem redigens, eversione damnavit: exemplum eorum, qui impie acturi sunt, ponens:
Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kuwa majivu na uharibifu ili iwe mfano kwa ajili ya waovu katika siku za usoni
7 et iustum Lot oppressum a nefandorum iniuria, ac luxuriosa conversatione eripuit:
Lakini alipofanya hilo, alimwokoa Lutu mtu wa haki, aliyekuwa amehuzunishwa na tabia chafu za wasiofuata sheria za Mungu.
8 aspectu enim, et auditu iustus erat: habitans apud eos, qui de die in diem animam iustam iniquis operibus cruciabant.
Kwa kuwa huyo mtu wa haki, aliyeishi nao siku kwa siku akiitesa nafsi yake kwa ajili ya yale aliyoyasikia na kuyaona.
9 Novit Dominus pios de tentatione eripere: iniquos vero in diem iudicii reservare cruciandos.
Kwa hiyo Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wake wakati wa mateso na jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajili ya hukumu katika siku ya mwisho.
10 magis autem eos, qui post carnem in concupiscentia immunditiæ ambulant, dominationemque contemnunt, audaces, sibi placentes, sectas non metuunt introducere blasphemantes:
Kwa hakika huu ndio ukweli kwa wale wanoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka. Watu wa jinsi hii wana ujasiri katika dhamiri zao, Hawaogopi kuwakufuru watukufu.
11 ubi Angeli fortitudine, et virtute cum sint maiores, non portant adversum se execrabile iudicium.
Ingawa malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu, lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana
12 Hi vero velut irrationabilia pecora, naturaliter in captionem, et in perniciem in his quæ ignorant blasphemantes in corruptione sua peribunt,
Lakini hawa wanyama wasio na akili wametengenezwa kwa asili ya kukamatwa na kuangamizwa.
13 percipientes mercedem iniustitiæ, voluptatem existimantes diei delicias: coinquinationes, et maculæ deliciis affluentes, in conviviis suis luxuriantes vobiscum,
Wanaumizwa kwa ujira wa maovu yao. Mchana kutwa huishi kwa anasa. Wamejaa uchafu na maovu. Hufurahia anasa za udanganyifu wanaposherehekea na wewe.
14 oculos habentes plenos adulterii, et incessabilis delicti. Pellicientes animas instabiles, cor exercitatum avaritia habentes, maledictionis filii:
Macho yao yamefunikwa na uzinzi; hawatosheki kutenda dhambi. Huwalaghai na kuwaangusha waumini wachanga katika dhambi. Wana mioyo iliyojaa tamaa, ni watoto waliolaaniwa.
15 derelinquentes rectam viam erraverunt, secuti viam Balaam ex Bosor, qui mercedem iniquitatis amavit:
Wameiacha njia ya kweli. wamepotoka na wameifuata njia ya Balaam mwana wa Beori, aliyependa kupata malipo ya udhalimu.
16 correptionem vero habuit suæ vesaniæ: subiugale mutum animal, hominis voce loquens, prohibuit prophetæ insipientiam.
Lakini alikemewa kwa ajili ya ukosai wake. Punda aliyekuwa bubu akiongea katika sauti ya binadamu, alizuia wazimu wa nabii.
17 Hi sunt fontes sine aqua, et nebulæ turbinibus exagitatæ, quibus caligo tenebrarum reservatur.
Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayotoweshwa na upepo. Wingu zito limehifadhiwa kwa ajili yao.
18 Superba enim vanitatis loquentes, pelliciunt in desideriis carnis luxuriæ eos, qui paululum effugiunt, qui in errore conversantur:
Huongea kwa majivuno matupu. Huwaangusha watu kwa tamaa ya mwili. Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosaji.
19 libertatem illis promittentes, cum ipsi servi sint corruptionem: a quo enim quis superatus est, huius et servus est.
Huwaahidi watu uhuru wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi. Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa wa kile kinachomtawala.
20 Si enim refugientes coinquinationes mundi in cognitione Domini nostri, et Salvatoris Iesu Christi, his rursus implicati superantur: facta sunt eis posteriora deteriora prioribus.
Yeye ajiepushaye na uchafu wa ulimwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo, na kisha akarudia uchafu huo tena, hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo.
21 Melius enim erat illis non cognoscere viam iustitiæ, quam post agnitionem, retrorsum converti ab eo, quod illis traditum est sancto mandato.
Ingefaa watu hao kama wasingeifahamu njia ya haki kuliko kuifahamu na kisha tena kuziacha amri takatifu walizopewa.
22 Contigit enim eis illud veri proverbii: Canis reversus ad suum vomitum: et, Sus lota in volutabro luti.
Mithali hii huwa na ukweli kwao. “mbwa huyarudia matapishi yake. Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope.”

< Petri Ii 2 >