< Corinthios Ii 8 >

1 Notam autem facimus vobis, fratres, gratiam Dei, quæ data est in Ecclesiis Macedoniæ:
Tunawataka ninyi mjue, kaka na dada, kuhusu neema ya Mungu ambayo imetolewa kwa makanisa ya Makedonia.
2 quod in multo experimento tribulationis abundantia gaudii ipsorum fuit, et altissima paupertas eorum abundavit in divitias simplicitatis eorum:
Wakati wa jaribu kubwa la mateso, wingi wa furaha yao na ongezeko la umaskini wao umezaa utjiri mkubwa wa ukarimu.
3 quia secundum virtutem testimonium illis reddo, et supra virtutem voluntarii fuerunt,
Kwa maana nashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya walivyoweza, na hata zaidi ya walivyoweza.
4 cum multa exhortatione obsecrantes nos gratiam, et communicationem ministerii, quod fit in sanctos.
Na kwa hiari yao wenyewe kwa kutusihi kwingi, walituomba kwa ajili ya kushiriki katika huduma hii kwa waumini.
5 Et non sicut speravimus, sed semetipsos dederunt primum Domino, deinde nobis per voluntatem Dei,
Hii haikutokea kama tulivyokuwa tunatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa wao wenyewe kwa Bwana. Kisha wakajitoa wao wenyewe kwetu kwa mapenzi ya Mungu.
6 ita ut rogaremus Titum: ut quemadmodum cœpit, ita et perficiat in vobis etiam gratiam istam.
Hivyo tulimsihi Tito, aliyekuwa tayari ameanzisha kazi hii, kuleta katika utimilifu tendo hili la ukarimu juu yenu.
7 Sed sicut in omnibus abundatis fide, et sermone, et scientia, et omni solicitudine, insuper et charitate vestra in nos, ut et in hac gratia abundetis.
Lakini ninyi mna wingi katika kila kitu- katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii, na katika upendo wenu kwa ajili yetu. Hivyo hakikisheni kwamba ninyi mnakuwa na wingi pia katika tendo hili la ukarimu.
8 Non quasi imperans dico: sed per aliorum solicitudinem, etiam vestræ charitatis ingenium bonum comprobans.
Nasema hili si kama amri. Badala yake, nasema hili ili kupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine.
9 Scitis enim gratiam Domini nostri Iesu Christi, quoniam propter vos egenus factus est, cum esset dives, ut illius inopia vos divites essetis.
Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini. Ili kwamba kupitia umaskini wake mweze kuwa tajiri.
10 Et consilium in hoc do: hoc enim vobis utile est, qui non solum facere, sed et velle cœpistis ab anno priore:
Katika jambo hili nitawapa ushauri ambao utawasaidia. Mwaka mmoja uliopita, hamkuanza tuu kufanya jambo. Lakini mlitamani kulifanya.
11 nunc vero et facto perficite: ut quemadmodum promptus est animus voluntatis, ita sit et perficiendi ex eo, quod habetis.
Sasa likamilisheni. Kama tu kulivyokuwa na shauku na nia ya kulifanya, kisha, je, mngeweza pia kulileta katika ukamilifu, kwa kadri ya mnavyoweza.
12 Si enim voluntas prompta est, secundum id, quod habet, accepta est, non secundum id, quod non habet.
Kwa kuwa mnashauku ya kufanya tendo hili, ni jambo zuri na linakubalika. Lazima lisimame juu ya kile alichonacho mtu, siyo juu ya asichokuwa nacho mtu.
13 Non enim ut aliis sit remissio, vobis autem tribulatio, sed ex æqualitate.
Kwa kuwa kazi hii siyo kwa ajili kwamba wengine waweze kupata nafuu na ninyi mweze kulemewa. Badala yake, kuwe na usawa.
14 In præsenti tempore vestra abundantia illorum inopiam suppleat: ut et illorum abundantia vestræ inopiæ sit supplementum, ut fiat æqualitas, sicut scriptum est:
Wingi wenu wa wakati wa sasa utasaidia kwa kile wanachohitaji. Hii ni hivyo pia ili kwamba wingi wao uweze kusaidia mahitaji yenu, na kwamba kuwe na usawa.
15 Qui multum non abundavit: et qui modicum, non minoravit.
Hii ni kama ilivyoandikwa; “Yeye aliye na vingi hakuwa na kitu chochote kilichobaki na yeye aliyekuwa na kidogo hakuwa na uhitaji wowote.”
16 Gratias autem Deo, qui dedit eandem solicitudinem pro vobis in corde Titi,
Lakini ashukuriwe Mungu, aliyeweka ndani ya moyo wa Tito moyo uleule wa bidii ya kujali ambyo ninayo kwa ajili yenu.
17 quoniam exhortationem quidem suscepit: sed cum solicitior esset, sua voluntate profectus est ad vos.
Kwa kuwa si tu alipokea maombi yetu, bali pia alikuwa na bidii kuhusiana na maombi hayo. Alikuja kwenu kwa hiari yake mwenyewe.
18 Misimus etiam cum illo fratrem, cuius laus est in Evangelio per omnes Ecclesias:
Tumemtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa miongoni mwa makanisa kwa ajili ya kazi yake katika kutangaza injili.
19 non solum autem, sed et ordinatus est ab Ecclesiis comes peregrinationis nostræ in hanc gratiam, quæ ministratur a nobis ad Domini gloriam, et destinatam voluntatem nostram:
Si hivi tu, lakini pia alichaguliwa na makanisa kusafiri nasisi katika kulibeba sehemu mbalimbali tendo hili la ukarimu. Hii ni kwa utukufu wa Bwana mwenyewe na kwa shauku yetu ya kusaidia.
20 devitantes hoc, ne quis nos vituperet in hac plenitudine, quæ ministratur a nobis.
Tunaepuka uwezekano kwamba yeyote napaswa kulalamika kuhusiana na sisi kuhusiana na ukarimu huu ambao tunaubeba.
21 Providemus enim bona non solum coram Deo, sed etiam coram hominibus.
Tunachukua uangalifu kufanya kilicho cha heshima, sio tu mbele za Bwana, lakini pia mbele za watu.
22 Misimus autem cum illis et fratrem nostrum, quem probavimus in multis sæpe solicitum esse: nunc autem multo solicitiorem, confidentia multa in vos,
Pia tunamtuma ndugu mwingine pamoja nao. Tumempima mara nyingi, na tumemwona ni mwenye shauku for ajili ya kazi nyingi. Hata sasa ana bidii zaidi kwa sababu ya ujasiri mkubwa alionao ndani yenu.
23 sive pro Tito, qui est socius meus, et in vos adiutor, sive fratres nostri, Apostoli Ecclesiarum, gloria Christi.
Kwa habari ya Tito, yeye ni mshirika mwenza wangu na mtendakazi mwenzangu kwa ajili yenu. Kama kwa ndugu zetu, wanatumwa na makanisa. Ni waheshima kwa Kristo.
24 Ostensionem ergo, quæ est charitatis vestræ, et nostræ gloriæ pro vobis, in illos ostendite in faciem Ecclesiarum.
Hivyo, waonesheni upendo wenu, na muoneshe kwa makanisa sababu ya majivuno yetu kwa ajili yenu.

< Corinthios Ii 8 >