< Timotheum I 2 >

1 Obsecro igitur primum omnium fieri obsecrationes, orationes, postulationes, gratiarum actiones pro omnibus hominibus:
Kwa hiyo awali ya yote, nahitaji maombi, na dua, na maombezi, na shukrani vifanyike kwa ajili ya watu wote,
2 pro regibus, et omnibus, qui in sublimitate sunt, ut quietam et tranquillam vitam agamus in omni pietate, et castitate.
kwa ajili ya wafalme na wote ambao wako kwenye mamlaka, ili kwamba tuweze kuishi maisha ya amani na utulivu katika utauwa wote na heshima.
3 Hoc enim bonum est, et acceptum coram Salvatore nostro Deo,
Hili ni jema na lenye kukubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu.
4 qui omnes homines vult salvos fieri, et ad agnitionem veritatis venire.
Yeye hutamani kuwa watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli.
5 Unus enim Deus, unus et mediator Dei et hominum homo Christus Iesus:
Kwa kuwa kuna Mungu mmoja, na kuna mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu ambaye ni Kristo Yesu.
6 qui dedit redemptionem semetipsum pro omnibus, testimonium temporibus suis:
Alijitoa mwenyewe kama fidia kwa wote, kama ushuhuda kwa wakati muafaka.
7 in quo positus sum ego prædicator, et Apostolus (veritatem dico, non mentior) doctor Gentium in fide, et veritate.
Kwa sababu hii, mimi mwenyewe nilifanywa kuwa mjumbe wa injili na mtume. Nasema kweli. Sisemi uongo. Mimi ni mwalimu watu Mataifa katika imani na kweli.
8 Volo ergo viros orare in omni loco, levantes puras manus sine ira, et disceptatione.
Kwa hiyo, nataka wanaume kila mahali waombe na kuinua mikono mitakatifu bila ghadhabu na mashaka.
9 Similiter et mulieres in habitu ornato, cum verecundia, et sobrietate ornantes se, et non in tortis crinibus, aut auro, aut margaritas, vel veste pretiosa:
Vivyo hivyo, nataka wanawake wajivike mavazi yanayokubalika, kwa heshima na kujizuia. Wasiwe na nywele zilizosukwa, au dhahabu, au Lulu, au mavazi ya gharama kubwa.
10 sed quod decet mulieres, promittentes pietatem per opera bona.
Pia nataka wavae mavazi yanayowastahili wanawake wanaokiri uchaji kwa kupitia matendo mema.
11 Mulier in silentio discat cum omni subiectione.
Mwanamke na ajifunze katika hali ya utulivu na kwa utii wote.
12 Docere autem mulieri non permitto, neque dominari in virum: sed esse in silentio.
Simruhusu mwanamke kufundisha, au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume bali aishi katika hali ya ukimya.
13 Adam enim primus formatus est: deinde Heva.
Kwa kuwa Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva.
14 Et Adam non est seductus: mulier autem seducta in prævaricatione fuit.
Adamu hakudanganywa, lakini mwanamke alidanganywa kabisa katika uasi.
15 Salvabitur autem per filiorum generationem, si permanserit in fide, et dilectione, et sanctificatione cum sobrietate.
Hata hivyo, ataokolewa kwa kupitia kuzaa watoto, kama wataendelea katika imani na upendo na katika utakaso na akili njema.

< Timotheum I 2 >