< ローマ人への手紙 3 >

1 然らばユデア人に何の長ぜる所かある、又割禮に何の益かある、
Kisha ni faida gani aliyo nayo Myahudi? Na faida ya tohara ni nini?
2 其は各方面に多し、即ち先神の曰し御言は彼等に托せられたるなり。
Ni vyema sana kwa kila njia. Awali ya yote, Wayahudi walikabidhiwa ufunuo kutoka kwa Mungu.
3 假令彼等の中に信ぜざる者ありしも、是何かあらん、彼等の不信仰は神の眞實を空しからしむべきか、決して然らず。
Lakini, itakuwaje iwapo baadhi ya Wayahudi hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kuwa batili?
4 神は眞實にて在し、人は総て僞る者なり。録して「(主よ)是汝が其言に於て義とせられ、審判せられ給ふも勝を得給はん為なり」、とあるが如し。
La hasha. Badala yake, acha Mungu aonekane kuwa kweli, hata kama kila mtu ni mwongo. Kama ilivyokuwa imeandikwa, “Ya kwamba uweze kuonekana kuwa mwenye haki katika maneno yako, na uweze kushinda uingiapo katika hukumu.”
5 若我等の不義が神の義を顕すとせば、我等何をか云はん、怒を加へ給ふ神は不義なるか、――
Lakini ikiwa uovu wetu unaonesha haki ya Mungu, tuseme nini? Mungu si dhalimu atoapo ghadhabu yake, je yupo hivyo? Naongea kutokana na mantiki ya kibinadamu.
6 是は人の云ふ如くに云へり――決して然らず、若然りとせば、神は如何にしてか此世を審判し給ふべき。
La hasha! Ni jinsi gani basi Mungu atauhukumu ulimwengu?
7 若我等の僞によりて神の眞實顕れ、其光榮の増したらんには、争でか我も罪人と定めらるる事あらんや。
Lakini ikiwa kweli ya Mungu kupitia uongo wangu hutoa sifa tele kwa ajili yake, kwa nini ningali bado nahukumiwa kama mwenye dhambi?
8 また――我等の罵られて然稱ふと或人々に云はるる如く――善を來さん為に惡を為すべけんや、斯る人々の罪せらるるは宜なり。
Kwa nini tusiseme, kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyothibitisha kwamba tunasema, “Tufanye uovu, ili mema yaje”? Hukumu juu yao ni ya haki.
9 然らば何ぞや、我等は異邦人に先つ者なるか、決して然らず、其は既にユデア人もギリシア人も皆罪の下に在りと證したればなり。
Ni nini basi? Tunajitetea wenyewe? Hapana kabisa. Kwa kuwa sisi tayari tumewatuhumu Wayahudi na Wayunani wote pamoja, ya kuwa wapo chini ya dhambi.
10 録して、「誰も義しき者なく、
Hii ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hata mmoja.
11 覚る者なく、神を求むる者なし、
Hakuna mtu ambaye anaelewa. Hakuna mtu ambaye anamtafuta Mungu.
12 皆迷ひて相共に空しき者となれり、善を為す者なし、一人だもある事なし。
Wote wamegeuka. Wao kwa pamoja wamekuwa hawana maana. Hakuna atendaye mema, la, hata mmoja.
13 彼等の喉は開きたる墓なり、其舌を以て欺き、其唇の下に蝮の毒あり、
Makoo yao ni kaburi lililo wazi. Ndimi zao zimedanganya. Sumu ya nyoka ipo chini ya midomo yao.
14 其口は詛と苦とに充ち、
Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15 其足は血を流す為に疾く、
Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16 破と禍とは、其道途に在り、
Uharibifu na mateso yapo katika njia zao.
17 彼等は平和の道を知らず、
Watu hawa hawajajua njia ya amani.
18 其目前に神に對する畏れなし」とあるが如し。
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao.”
19 但総て律法の言ふ所は律法の下に在る人々に向ひて言ふこと、我等之を知れり、是凡ての口塞りて、全世界が神に屈服するに至らん為なり。
Sasa tunajua kwamba chochote sheria isemacho, husema na wale walio chini ya sheria. Hii ni ili kwamba kila kinywa kifungwe, na hivyo kwamba ulimwengu wote uweze kuwajibika kwa Mungu.
20 蓋神の御前には、如何なる人も律法の業に由りて義とせらるる事あらじ、律法に由りて得るは罪の意識なればなり。
Hii ni kwa sababu hakuna mwili utakaohesabiwa haki kwa matendo ya sheria mbele za macho yake. Kwa kuwa kupitia Sheria huja ufahamu wa dhambi.
21 然るに律法と預言者とに證せられて、神の[賜ふ]義は今や律法の外に顕れたり。
Lakini sasa pasipo sheria, haki ya Mungu imejulikana. Ilishuhudiwa kwa sheria na Manabii,
22 即ちイエズス、キリストに於る信仰に由て神の「賜ふ」義は信仰する者の凡に及び、凡ての上に在り、蓋し差別ある事なし、
hiyo ni, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo kwa wale wote wanaoamini. Maana hakuna tofauti.
23 其は皆罪を犯したる者にして、神の光榮を要すればなり。
Kwa kuwa wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
24 人々の義とせらるるは、功なくして唯神の恩寵に由り、キリスト、イエズスに於る贖に由りてなり。
Wamehesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.
25 即ち神は從前の罪を忍び給ひしに、其赦を以て己が正義を顕さん為に、イエズス、キリストを宥の犠牲に供へ、其御血に於る信仰を有たしめ、
Kwa maana Mungu alimtoa Kristo Yesu awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alimtoa Kristo kama ushahidi wa haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizopita
26 今は己が正義を證せんとて、自ら其正義を顕し給ひ、イエズス、キリストに於る信仰の人をも義と為し給ひしなり。
katika uvumilivu wake. Haya yote yalitokea ili kuonesha haki yake wakati huu wa sasa. Hii ilikuwa ili aweze kujithibitisha mwenyewe kuwa haki, na kuonesha kwamba humhesabia haki mtu yeyote kwa sababu ya imani katika Yesu.
27 然らば誇る所何處にか在る、其は除かれたり。如何なる法を以て除かれたるか、業を以てなるか、然らず、信仰の法を以てなり。
Kuwapi basi kujisifu? Kumetengwa. Kwa misingi ipi? Misingi ya matendo? Hapana, lakini kwa misingi ya imani.
28 蓋我等謂ふに、人の義とせらるるは律法の業に由らずして信仰に由る。
Hivyo tunahitimisha kwamba mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.
29 神豈ユデア人のみの神ならんや、異邦人にも亦然るに非ずや、然り異邦人にも神たるなり。
Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Je yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Ndiyo, wa mataifa pia.
30 其は神は唯一に在して、割禮の人を信仰に由りて義とし、無割禮の人をも信仰に由りて義とし給へばなり。
Ikiwa kwa kweli Mungu ni mmoja, atawahesabia haki walio wa tohara kwa imani, na wasiotahiriwa kwa njia ya imani.
31 然らば我等は信仰を以て律法を亡ぼすか、然らず、却て律法を固うするなり。
Je sisi twaibatilisha sheria kwa imani? La hasha! Kinyume cha hayo, sisi twaithibitisha sheria.

< ローマ人への手紙 3 >