< ローマ人への手紙 12 >

1 第一款 キリスト信者相互の義務 然れば兄弟等よ、我神の諸の恤に由りて汝等に勧む。汝等其肉身を以て、活ける、聖なる、神の御意に適へる犠牲、己が道理的禮拝として供へよ。
Kwa hiyo nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, inayokubalika kwa Mungu. Hii ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 又此世に倣ひ從ふ事なく、却て神の御旨、即ち善と御意に適ふ事と完全との如何なるものなるかを暁らん為、精神を一新して自ら改革せよ。 (aiōn g165)
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Fanyeni hivi mpate kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na kamilifu. (aiōn g165)
3 蓋我賜はりたる恩寵によりて、汝等の中に在る凡ての人に謂はん、己を重んずべき程度以上に重んぜず、適宜に、而も神の夫々分配し給ひし信仰の量に從ひて重んぜよ。
Kwa maana nasema, kwa sababu ya neema niliyopewa, kwamba kila mtu ambaye yupo miongoni mwenu hapaswi kufikiri zaidi juu yake mwenyewe kuliko inavyompasa kufikiri. Bali, imempasa kufikiri kwa hekima, kama ambavyo Mungu amewapa kila mmoja kiasi fulani cha imani.
4 蓋我等は一の體に多くの肢ありて、凡ての肢其用を同うせざるが如く、
Kwa kuwa tuna viungo vingi katika mwili mmoja, lakini si viungo vyote vina kazi moja.
5 我等多くの人は、キリストに於て一の體にして、各互に肢たるなり。
Vivyo hivyo, sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake.
6 然れば我等に賜はりたる恩寵に從ひて賜を異にしたれば、預言は信仰の理に随ひて為し、
Tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadiri ya neema mliyopewa. Ikiwa karama ya mtu ni unabii, na itendeke kwa kadiri ya imani yake.
7 聖役は聖役に[從事し]、教ふる人は教に[止り]、
Ikiwa karama ya mtu ni huduma, na atumike. Ikiwa mwingine ana karama ya kufundisha, basi, afundishe.
8 勧を為す人は勧を為し、與ふる人は淡白を以てし、司る人は奮發を以てし、慈悲を施す人は歓を以てすべし。
Ikiwa karama ya mtu ni faraja, basi, afariji. Ikiwa karama ya mtu ni kutoa, afanye hivyo kwa ukarimu. Ikiwa karama ya mtu ni kuongoza, na litendeke kwa uangalifu. Ikiwa karama ya mtu ni katika kuonesha huruma, na litendeke kwa furaha.
9 愛は表裏あるべからず、汝等惡を嫌ひて善に就き、
Pendo lisiwe na unafiki. Chukieni uovu; mshikilie yaliyo mema.
10 兄弟の愛を以て相寵み、互に相推重し、
Kuhusu upendo wa ndugu, pendaneni ninyi kwa ninyi. Kuhusu heshima, heshimianeni ninyi kwa ninyi.
11 注意を怠らず、熱心にして主に事へ、
Kuhusu bidii, msiwe walegevu. Kuhusu roho, iweni na shauku. Kuhusu Bwana, mtumikieni.
12 希望によりて歓び、患難に忍耐し、絶えず祈祷に從事し、
Furahini katika ujasiri mlionao kuhusu siku zijazo. Muwe na subira katika matatizo yenu. Mdumu katika kuomba.
13 聖徒の入用を補け、接待を行ひ、
Mshiriki katika mahitaji ya waumini. Tafuteni njia nyingi za kuonesha ukarimu.
14 汝等を迫害する人を祝せよ、祝して詛ふこと勿れ。
Watakieni baraka wote wanaowatesa ninyi; muwabariki na wala msiwalaani.
15 喜ぶ人々と共に喜び、泣く人々と共に泣き、
Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.
16 心を相同じうし、高きを思はずして低きに甘んじ、自ら智しとすること勿れ。
Muwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msifikiri kwa kujivuna, lakini wakubalini watu wa hali ya chini. Msiwe na hekima juu ya mawazo yenu wenyewe.
17 如何なる人にも惡を以て惡に報ゆる事なく、啻に神の御前のみならず、衆人の前にも善なる事を圖り、
Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Fanyeni mambo mema machoni pa watu wote.
18 汝等が力の及ぶ限り、為し得べくんば衆人と相和せよ。
Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote.
19 至愛なる者よ、自ら復讐せずして[神の]怒に任せよ、其は録して、「主曰く、復讐は我事なり、我は報いん」とあればなり。
Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, '' 'kisasi ni changu; Mimi nitalipa,' asema Bwana.”
20 却て汝の仇飢ゑなば之に食せしめ、渇かば之に飲ましめよ。斯くすれば汝彼の頭に燃炭を積むならん、
“Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake.”
21 惡に勝たるる事なく、善を以て惡に勝て。
Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.

< ローマ人への手紙 12 >