< ヨハネの黙示録 4 >

1 第一款 豫備の出現 其後我見たるに、折しも天に開けたる門あり、而して我が初に我に語るを聞きし喇叭の如き聲言ひけるは、此處に登れ、我此後に成るべき事を汝に示さん、と。
Baada ya mambo haya nilitazama, nikaona kuwa mlango ulikuwa umefunguliwa mbinguni. Ile sauti ya kwanza, ikizungumza nami kama tarumbeta, ikisema, “Njoo hapa, nitakuonesha yatakayotokea baada ya mambo haya.”
2 斯て我忽ち氣を奪はれたるが如くになりしに、折しも天に一の玉座備へられ、其玉座の上に坐し給ふものありて、
Mara moja nilikuwa katika Roho, niliona kulikuwa na kiti cha enzi kimewekwa mbinguni, na mtu amekikalia.
3 其坐し給ふものは碧玉及び赤條瑪瑙の象の如く、又玉座の周圍に緑玉の象の如き虹ありき。
Mmoja aliyekuwa amekikalia alionekana kama jiwe la yaspi na akiki. Kulikuwa na upinde wa mvua umekizunguka kiti cha enzi. Upinde wa mvua ulionekana kama zumaridi.
4 然て玉座の周圍に廿四の高座あり、其高座の上には白衣を纏ひて頭に金冠を戴ける廿四人の翁坐し居れり。
Kukizunguka kiti cha enzi kulikuwa na viti vya enzi vingine ishirini na vinne, na waliokaa kwenye viti vya enzi walikuwa wazee ishirini na wanne, wamevikwa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani mwao.
5 斯て玉座より電光と數多の聲と雷鳴と出でつつありしが、玉座の正面には輝く七の燈火あり、是即ち神の七霊なり。
Kutoka katika kiti cha enzi kulitoka miale ya radi, muungurumo na radi. Taa saba zilikuwa zikiwaka mbele ya kiti cha enzi, taa ambazo ni roho saba za Mungu.
6 又玉座の前に水晶に似たる玻璃の海あり、玉座の中央と周圍とに、前後共に目にて満ちたる四の動物ありき。
Tena mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na bahari, iliyowazi kama kioo. Wote kuzunguka kiti cha enzi kulikuwa na wenye uhai wanne, waliojaa macho mbele na nyuma.
7 第一の動物は獅子の如く、第二の動物は犢の如く、第三の動物は人の如き顔ありて、第四の動物は飛ぶ鷲の如し。
Kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, kiumbe wa pili mwenye uhai alikuwa kama ndama, kiumbe wa tatu mwenye uhai alikuwa na uso kama wa mwanadamu, na yule mwenye uhai wa nne alikuwa kama tai apaaye.
8 此四の動物各六の翼ありて、内外共に目にて満ち、晝夜絶間なく、聖なる哉、聖なる哉、聖なる哉、曾て在し、今も在し、又将に來り給ふべき全能の神にて在す主よ、と言ひ居れり。
Viumbe wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa na mabawa sita, wamejaa macho juu na chini yake. Usiku na mchana hawakomi kusema, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu, mtawala juu ya wote, aliyekuwepo, na aliyepo na atakayekuja.”
9 斯て此四の動物、玉座に坐し給ひて世々に限なく活き給ふものに、光榮と尊崇と感謝とを歸し奉るに、 (aiōn g165)
Kila wakati viumbe wenye uhai walipotoa utukufu, heshima, na kushukuru mbele za aliyekuwa ameketi kwenye hicho kiti cha enzi, yeye aishiye milele na daima, (aiōn g165)
10 廿四人の翁、玉座に坐し給ふものの御前に平伏し、世々に限なく活き給ふものを禮拝し奉り、己が冠を玉座の前に投じつつ、 (aiōn g165)
wazee ishirini na wanne walisujudu wenyewe mbele yake aliyekikalia kiti cha enzi. Waliinama chini kwake aishiye milele na daima na kutupa chini taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema, (aiōn g165)
11 主にて在す我等の神よ、主こそは光榮と尊崇と能力とを受け給ふべけれ、其は御自ら萬物を創造し給ひ、萬物の存在にして創造せられしは御旨によればなり、と言ひ居れり。
“Wastahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Kwa kuwa uliviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako, vilikuwepo na viliumbwa.”

< ヨハネの黙示録 4 >