< ヨハネの黙示録 2 >

1 エフェゾ教會の天使に斯く書遣れ、右の御手に七の星を持ち、七の金の燈台の中央に歩み給ふもの曰く、
“Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika: 'Haya ni maneno ya yule anayeshikilia zile nyota saba katika mkono wake wa kuume. Yeye atembeaye kati ya vinara vya dhahabu vya taa saba asema hivi, “
2 我は汝の業と働と忍耐とを知り、又汝が惡人を忍び得ざる事と、自ら使徒と稱しつつ然らざる人々を試みて其僞れる者たるを認めし事と、
'“Najua ambacho umetenda na bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti, na kwamba huwezi kuhusiana nao walio waovu, na umewajaribu wote wanaojiita kuwa mitume na kumbe siyo, na wameonekana kuwa waongo.
3 汝の忍耐ある事と、我名の為に患難を忍びて倦まざりし事とを知れり。
Najua una subira na uvumilivu, na umepitia mengi kwa sababu ya jina langu, na haujachoka bado.
4 然れども汝に咎むる所あり、即ち汝は最初の愛を離せり、
Lakini hili ndilo nililonalo dhidi yako, umeuacha upendo wako wa kwanza.
5 然れば其何處より堕落せしかを思ひ、改心して最初の業を為せ。若然らずして改心せずば、我汝の許に至り、汝の燈台を其處より取除かん。
Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka, ukatubu na kufanya matendo uliyofanya tangu mwanzo. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako kutoka mahali pake.
6 然りながら汝に長所あり、即ちニコライ党の業を憎める事にして、我も亦之を憎めるなり。
Lakini wewe una hili, unachukia yale ambayo Wanikolai wameyatenda, ambayo hata mimi nayachukia.
7 耳ある者は[聖]霊の諸教會に曰ふ所を聞け、即ち勝利を得たる人には我わが神の樂園に在る生命の樹の果を食せしめん。
Kama una sikio, sikiliza yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Na kwa yeye ashindaye nitampa kibali cha kula kutoka katika mti wa uzima ulio katika paradiso ya Mungu.'
8 又スミルナ教會の天使に斯く書遣れ、最初のものにして最終のものたり、且死したりしに活き給へるもの曰く、
“Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika: 'Haya ni maneno ya yule ambaye ni mwanzo na mwisho ambaye alikufa na kuwa hai tena:
9 我は汝の患難と貧窮とを知れり、然れど汝は富めり。又自らユデア人と稱しつつ、然らずして、却てサタン教會たる人々に罵らるるなり。
'“Nayajua mateso yako na umasikini wako (lakini wewe ni tajiri), na uongo wa wale wanaojiita ni wayahudi (lakini siyo - wao ni sinagogi la Shetani).
10 受けんとする苦を一も懼るる事勿れ、看よ惡魔は汝等を試みんとて、汝等の幾人を監獄に入るべく、汝等は十日の間患難に遇はんとす。汝等死に至るまで忠信なれ、然らば我生命の冠を汝に與へん。
Usiogope mateso yatakayokupata. Tazama! Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani ili mpate kujaribiwa, na mtateseka kwa siku kumi. Iweni waaminifu hadi kufa, na nitawapa taji ya uzima.
11 耳ある者は[聖]霊の諸教會に曰ふ所を聞け、即ち勝利を得たる人は第二の死に害せられじ。
Kama una sikio, sikiliza Roho anavyoyaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapata madhara ya mauti ya pili.'
12 又ベルガモ教會の天使にかく書遣れ、兩刃の利き剣を持ち給へるもの曰く、
“Kwa malaika wa kanisa la Pergamo andika: 'Haya ndiyo anenayo yeye aliye nao huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
13 我は汝の何處に住むかを知れり、即ちサタンの座の有る處なり。然るに汝我名を保ちて、我忠信なる證人アンチパスが汝等の中なるサタンの住む處にて殺されし時すら、汝は我に於る信仰を否まざりき。
'“Najua mahali unapoishi -mahali kilipo kiti cha enzi cha shetani. Hata hivyo wewe walishika sana jina langu, na hukuikana imani yako iliyo kwangu, hata siku zile za Antipasi shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa miongoni mwenu, hapo ndipo Shetani anaishi.
14 然れども少しく汝に咎むべき事あり、即ち汝の處にはバラアムの教を保てる人々あり、彼は禁物を食せしめ又私通せしめん為に、躓く物をイスラエルの子等の前に置くべしと、バラクに教へ居りしが、
Lakini nina mambo machache dhidi yako: unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki kuweka vikwazo mbele ya wana wa Israel, ili wale vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu na kuzini.
15 斯の如く汝の地にニコライ党の教を保てる人々あり。
Katika hali iyo hiyo, hata wewe unao baadhi yao wanaoshika mafundisho ya Wanikolai.
16 汝も亦改心せよ、然らずんば我速に汝の許に至り、我口の剣を以て彼等と戰はん。
Basi tubu! Na usipofanya hivyo, naja upesi, na nitafanya vita dhidi yao kwa upanga utokao katika kinywa changu.
17 耳ある者は[聖]霊の諸教會に曰ふ所を聞け、即ち勝利を得たる人に我隠れたるマンナを與へ、又白き石に新しき名を記して與へん、其名は白き石を受くる者の外之を知る者なし。
Kama una sikio, sikiliza Roho anachowaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, pia nitampa jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya juu ya jiwe, jina ambalo hakuna alijuaye isipokuwa yeye alipokeaye.'
18 又チアチラ教會の天使に斯く書遣れ、神の御子、即ち御目は焔の如く、御足は青銅の如くに在すもの曰く、
“Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika: “Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na nyayo kama shaba iliyosuguliwa sana:
19 我は汝の業と信仰と、愛と務と忍耐と、又後の業の前の業より多き事とを知れり。
'“Najua ambacho umefanya - upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti, na kwamba kile ulichofanya hivi karibuni ni zaidi ya kile ulichofanya mwanzo.
20 然れども聊汝に咎むべき所あり、即ち汝は預言者と自稱する婦人イエザベルの、我僕等を教へ且惑はして、私通せしめ偶像に献げられし物を食せしむるを措けり。
Lakini ninalo hili dhidi yako: unamvumilia mwanamke Yezebeli anayejiita mwenyewe nabii mke. Kwa mafundisho yake, anawapotosha watumishi wangu kuzini na kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.
21 我彼婦人に改心すべき暇を與へたれど、敢えて其私通より改心せず、
Nilimpa muda wa kutubu, lakini hayuko tayari kuutubia uovu wake.
22 看よ、我彼を床に臥さしむべく、又彼と共に姦淫を為す人々にして、己が業より改心せずば、大いなる患難に遇ふべく、
Angalia! Nitamtupa kwenye kitanda cha maradhi, na wale watendao uasherati naye kwenye mateso makali, vinginevyo watubu kwa alichofanya.
23 我又彼が子等を撃殺すべく、斯て諸教會は我が人の心腸を探るる者たるを知るに至るべく、我又汝等に各其業に應じて報ゆる所あらん。而して汝等、
Nitawapiga wanawe wafe na makanisa yote watajua kwamba mimi ndiye niyachunguzaye mawazo na tamaa. Nitampa kila mmoja wenu kadiri ya matendo yake.
24 即ちチアチラに在る他の人々に謂はん、総て彼教を有たざるもの、所謂サタンの奥義を知らざるもの我汝等に他の荷を負はせじ。
Lakini kwa baadhi yenu mliosalia katika Thiatira, kwa wale wote msioshika fundisho hili, na msiojua kile ambacho baadhi huita mafumbo ya Shetani, nasema kwenu, 'sitaweka juu yenu mzigo wowote.'
25 但汝等が有てる所を我が來るまで保て、
Kwa jambo lolote, lazima muwe imara mpaka nitakapokuja.
26 而して勝利を得て、終まで我業を守りたる人には、與ふるに諸國民に對する権威を以てすべし、
Yeyote ashindaye na kufanya kile nilichofanya hadi mwisho, kwake yeye nitampa mamlaka juu ya mataifa.
27 彼は鉄の杖を以て之を治め、彼等は土器の如くに砕かれん、
'Atawatawala kwa fimbo ya chuma, kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande.'
28 猶我にも我父より賜はりたるが如し。而して我亦彼人に暁の明星を與ふべし。
Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu, nitampa pia nyota ya asubuhi.
29 耳ある者は[聖]霊の諸教會に曰ふ所を聞け。
Ukiwa na sikio, sikiliza kile ambacho Roho anayaambia makanisa.'

< ヨハネの黙示録 2 >