< マタイの福音書 28 >

1 斯て安息日の終、即ち一週の首の黎明に、マグダレナ、マリアと他のマリアと、墓を見んとて至りしに、
Baadaye jioni siku ya Sabato, jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya juma, Mariamu magadalena, na yule Mariam mwingine walikuja kuliona kaburi.
2 折しも大地震あり、即ち主の使天より降り、近づきて石を転ばし退け、然て其上に坐せしが、
Tazama kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe, kisha akalikalia.
3 其容は電光の如く、其衣服は雪の如し。
Sura yake ilikuwa kama ya umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.
4 番兵等怖れ慄きて死人の如くなれり。
Wale walinzi walijawa na hofu na kuwa kama wafu.
5 天使婦人等に答へて云ひけるは、汝等懼るること勿れ、蓋我汝等が十字架に釘けられ給ひしイエズスを尋ぬるを知れり。
Yule malaika akawafafanulia wale wananawake akisema, “msiogope kwa maana najua kuwa mnamtafuta Yesu, aliyesulibiwa.
6 彼は此處に在さず、即ち曰ひし如く復活し給へり。來りて主の置かれ給ひたりし處を見、
Hayupo hapa, lakini amefufuka kama alivyowaambia. Njooni muone mahali ambapo Bwana alilala.
7 且疾く往きて弟子等に其復活し給ひし事を告げよ。彼は汝等に先ちて既にガリレアに往き給ふ、汝等彼處に之を見るべし[と云へ]、我預之を汝等に告げたるぞ、と。
Nendeni haraka mkawaambie wanafunzi wake, 'Amefufuka toka wafu, tazama amewatangulia Galilaya. Huko ndiko mtamwona.' Tazama mimi nimewaambia.”
8 婦人等畏と大なる喜とを懐きて速に墓を去り、弟子等に告げんとて走れり。
Wale wanawake waliondoka pale kaburini haraka wakiwa na hofu na furaha kubwa, na wakakimbia kuwaambia wanafunzi wake.
9 折しもイエズス彼等に行遇ひ、安かれ、と曰ひければ、彼等近づきて御足を抱き、之を禮拝せり。
Tazama Yesu akakutana nao na kusema, “Salamu.”wale wanawake walikuja na kushika miguu yake, na kisha wakamwabudu.
10 時にイエズス彼等に曰ひけるは、懼るること勿れ、往きて我兄弟等にガリレアに往けと告げよ、彼等彼處に我を見るべし、と。
Kisha Yesu akawaambia, “msiogope, nendeni mkawaambie ndugu zangu watangulie Galilaya. Huko wataniona.
11 婦人等の去りし折しも番兵の中數人の者市に至り、有りし事を悉く司祭長等に告げしかば、
Wakati wale wanawake walipokuwa wakienda, tazama baadhi ya walinzi walienda mjini na kuwaambia wakuu wa makuhani mambo yote yaliyokuwa yametokea.
12 彼等は長老等と相集りて協議し、金を多く兵卒等に與へて、
Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari
13 云ひけるは、汝等斯く云へ、彼の弟子等夜來りて、我等の眠れる中に彼を盗めりと。
na kuwaambia, “Waambieni wengine kuwa, 'wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.'
14 此事若総督に聞えなば、我等彼を説きて汝等を無事ならしめん、と。
Kama taarifa hii itamfikia liwali, sisi tutamshawishi na kuwaondoleeni ninyi mashaka yote.”
15 番兵等金を取りて、云含められし如くにしたれば、此談は今日に至るまでもユデア人の中に広まれり。
Kwa hiyo wale askari wakazichukua zile pesa na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa. Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo.
16 斯て十一の弟子ガリレアに往き、イエズスの彼等に命じ給ひし山に[至り]、
Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza.
17 イエズスを見て禮拝せり。然れど疑ふ者もありき。
Nao walipomwona, walimwabudu. lakini baadhi yao waliona shaka.
18 イエズス近づきて彼等に語りて曰ひけるは、天に於ても地に於ても、一切の権能は我に賜はれり。
Yesu akaja kwao akawambia akisema, “Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni.
19 故に汝等往きて萬民に教へ、父と子と聖霊との御名によりて是に洗禮を施し、
Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu.
20 我が汝等に命ぜし事を悉く守るべく教へよ。然て我は世の終まで日々汝等と偕に居るなり、と。 (aiōn g165)
Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaamuru, Na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia. (aiōn g165)

< マタイの福音書 28 >