< マタイの福音書 27 >

1 第九項 イエズスピラトの前に出廷し給ふ 黎明に及びて、司祭長民間の長老等、皆イエズスを死に處せんと協議し、
Muda wa asubuhi ulipofika, wakuu wote wa makuhani na wazee wa watu walikula njama dhidi ya Yesu wapate kumuua.
2 縛りて之を召連れ、総督ポンショ、ピラトに付せり。
Walimfunga, walimwongoza, na kumfikisha kwa Liwali Pilato.
3 時にイエズスを付ししユダ、其宣告せられ給ひしを見て後悔し、三十枚の銀貨を司祭長長老等に齎して之を返し、
Kisha wakati Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti, aliona kwamba Yesu amekwisha kuhukumiwa, alijuta na kurudisha vipande thelathini vya fedha kwa mkuu wa makuhani na wazee,
4 我無罪の血を売りて罪を犯せり、と云ひしかば彼等云ひけるは、我等に於て何かあらん、汝自見るべし、と。
na akasema, “Nimefanya dhambi kwa kuisaliti damu isiyo na hatia.” Lakini wakajibu, “Inatuhusu nini sisi? Yaangalie hayo mwenyewe.”
5 ユダ銀貨を[神]殿の内に投棄てて去りしが、往きて縄を以て自縊れたり。
Kisha alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na kuondoka zake na kujinyonga mwenyewe.
6 司祭長等、其銀貨を取りて云ひけるは、是血の値なれば賽銭箱に入るべからず、と。
Mkuu wa makuhani alivichukua vile vipande vya fedha na kusema, “Si halali kuiweka fedha hii katika hazina, kwa sababu ni gharama ya damu.”
7 即ち協議して、是にて陶匠の畑を買ひ、旅人の墓地に充てたり。
Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.
8 故に此畑、今日までもハケルダマ、即ち血の畑と呼ばれたり。
Kwa sababu hii shamba hilo limekuwa likiitwa, “Shamba la damu” hadi leo hii.
9 是に於て預言者エレミアによりて云はれし事成就せり、曰く「彼等はイスラエルの子等に評價られしものの値なる銀貨三十枚を取り、
Kisha lile neno lililokuwa limenenwa na nabii Yeremia lilitimia, kusema, “Walitwaa vipande thelathini vya fedha, gharama iliyopangwa na watu wa Israel kwa ajili yake,
10 陶匠の畑の為に與へたり、主の我に示し給へる如し」と。
na waliitumia kwa shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyokuwa amenielekeza.”
11 然てイエズス、総督の前に出廷し給ひしに、総督問ひて云ひけるは、汝はユデア人の王なるか。イエズス曰ひけるは、汝の云へるが如し、と。
Sasa Yesu alisimama mbele ya liwali, na liwali akamwuliza, “Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu alimjibu, “Wewe wasema hivyo.”
12 斯て司祭長、長老等より訴へられ給へども、何事をも答へ給はざりければ、
Lakini wakati aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu chochote.
13 ピラト是に云ひけるは、彼等が汝に對して如何に大なる證言を為すかを聞かざるか、と。
Kisha Pilato alimwambia, “Hujayasikia mashitaka yote dhidi yako?”
14 イエズス一言も是に答へ給はざりしかば、総督感嘆する事甚しかりき。
Lakini hakumjibu hata neno moja, hivyo liwali alijawa na mshangao.
15 茲に、祭日に當りて総督が人民の欲する所の囚人一個を釈すの例ありしが、
Sasa katika sikukuu ilikuwa desturi ya liwali kumfungua mfungwa mmoja anayechaguliwa na umati.
16 折しもバラバと云へる名高き囚人あるにより、
Wakati huo walikuwa na mfungwa sugu jina lake Baraba.
17 ピラト彼等の集りたるに、汝等は我誰を釈さん事を欲するか、バラバかキリストと云へるイエズスか、と云へり。
Hivyo wakati walipokuwa wamekusanyika pamoja, Pilato aliwauliza, “Ni nani mnataka tumfungue kwa ajili yenu?” Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?”
18 其は人が妬によりてイエズスを付ししを知ればなり。
Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.
19 然て総督法廷に坐しけるに、其妻人を遣はして云ひけるは、汝此義人に係はること勿れ、蓋我今日夢の中に、彼の為に多く苦しめり、と。
Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, “Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake.”
20 司祭長、長老等人民に向ひ、バラバを乞ひてイエズスを亡ぼさん事を勧めしが、
Ndipo wakuu wa makuhani na wazee waliwashawishi makutano wamwombe Baraba, na Yesu auawe.
21 総督答へて、汝等は二人の中何れを釈されん事を望むか、と云ひしに彼等、バラバを、と云ひしかば、
Liwali aliwauliza, “Ni yupi kati ya wawili mnataka mimi nimwachie kwenu?” Walisema, “Baraba.”
22 ピラト云ひけるは、然らばキリストと云へるイエズスを我如何に處分せんか。
Pilato akawaambia, “Nimtendee nini Yesu anayeitwa Kristo?” Wote wakajibu, “Msulibishe”
23 皆曰く、十字架に釘けよ、と。総督、彼何の惡を為ししか、と云ひたれど彼等益叫びて、十字架に釘けよ、と云ひ居たり。
Naye akasema, “Kwa nini, ni kosa gani ametenda?” Lakini walizidi kupaza sauti hata juu mno, “Msulibishe.”
24 ピラト其何の効もなく却て騒動の彌増すを見て、水を取り、人民の前に手を洗ひて云ひけるは、此義人の血に就きて我は罪なし、汝等自ら見るべし、と。
Hivyo wakati Pilato alipoona hawezi kufanya lolote, lakini badala yake vurugu zilikuwa zimeanza, alitwaa maji akanawa mikono yake mbele ya umati, na kusema, “Mimi sina hatia juu ya damu ya mtu huyu asiye na hatia. Yaangalieni haya wenyewe.”
25 人民皆答へて、其血は我等と我等の子等との上に[被れかし]、と云ひしかば、
Watu wote wakasema, “Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu.”
26 総督バラバを彼等に釈し、イエズスをば鞭たせて十字架に釘けん為彼等に付せり。
Kisha akamfungulia Baraba kwao, lakini alimpiga mijeredi Yesu na kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa.
27 然て総督の兵卒等、イエズスを役所に引取り、全隊を其許に呼集め、
Kisha askari wa liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakamkusanyika.
28 其衣服を褫ぎて赤き袍を着せ、
Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu.
29 茨の冠を編みて其頭に冠らせ、右の手に葦を持たせ、其前に跪きて、ユデア人の王よ安かれ、と云ひて嘲り、
Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeri, wakisema, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi?”
30 又是に唾吐きかけ、葦を取りて其頭を打ち居れり。
Na walimtemea mate, na walitwaa mwanzi na kumpiga kichwani.
31 第十項 十字架上の犠牲 イエズスを嘲弄して後、其袍を褫ぎて原の衣服を着せ、十字架に釘けんとて引行きしが、
Wakati walipokuwa wakimkejeri, walimvua ile kanzu na kumvika nguo zake, na kumwongoza kwenda kumsulibisha.
32 街を出る時、シモンと名くるシレネ人に遇ひしかば、強て是に其十字架を擔はせたり。
Walipotoka nje, walimwona mtu kutoka Krene jina lake Simeoni, ambaye walimlazimisha kwenda nao ili apate kuubeba msalaba wake.
33 斯てゴルゴタ即ち髑髏と云へる處に至り、
Walipofika mahali paitwapo Galigotha, maana yake, “Eneo la fuvu la Kichwa.”
34 胆を和ぜたる葡萄酒をイエズスに飲ませんとせしに、之を嘗め給ひて、飲む事を肯じ給はざりき。
Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo anywe. Lakini alipoionja, hakuweza kuinywa.
35 彼等イエズスを十字架に釘けて後、籤を抽きて其衣服を分ちしが、是預言者に託りて云はれし事の成就せん為なり。曰く「彼等互に我衣服を分ち、我下着を抽鬮にせり」と。
Wakati walipokuwa wamemsulibisha, waligawana mavazi yake kwa kupiga kura.
36 彼等復坐してイエズスを守り居りしが、
Na waliketi na kumwangalia.
37 其頭の上に、是ユデア人の王イエズスなり、と書きたる罪標を置けり。
Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake yakisomeka, “Huyu ni Yesu, mfalme wa Wayahudi.”
38 然て是と共に二人の強盗、一人は其右に、一人は其左に十字架に釘けられしが、
Wanyang'anyi wawili walisulibiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto.
39 往來の人イエズスを罵り、首を振りて、
Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao
40 噫汝神殿を毀ちて三日の中に之を建直す者よ、自を救へ、若神の子ならば十字架より下りよ、と云ひ居たり。
na kusema, “Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!”
41 司祭長等も亦、律法學士、長老等と共に同じく嘲りて云ひけるは、
Katika hali ile ile wakuu wa makuhani walikuwa wakimkashifu, pamoja na waandishi na wazee, na kusema,
42 彼は他人を救ひしに自を救ふ能はず、若イスラエルの王ならば、今十字架より下るべし、然らば我等彼を信ぜん。
“Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi. Na ashuke chini toka msalabani, ndipo tutakapomwamini.
43 彼は神を頼めり、神若彼を好せば今救ひ給ふべし、其は「我は神の子なり」と云ひたればなり、と。
Alimtumaini Mungu. Acha Mungu amwokoe sasa kama anataka, kwa sababu alisema, 'Mimi ni Mwana wa Mungu.'”
44 イエズスと共に十字架に釘けられたる強盗等も、同じ様に罵り居たり。
Na wale wanyang'anyi waliokuwa wamesulibiwa pamoja naye pia walisema maneno ya kumdhihaki.
45 斯て十二時より三時まで、地上徧く黒暗となりしが、
Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.
46 三時頃、イエズス聲高く呼はりて曰ひけるは、エリ、エリ、ラマ、サバクタニ、と。是即、我神よ、我神よ、何ぞ我を棄て給ひしや、の義なり。
Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama thabakithan?” akimaanisha, “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”
47 其處に立てる者の中、或人々之を聞きて、彼エリアを呼ぶよ、と云ひ居りしが、
Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, “Anamwita Eliya.”
48 軈て其中の一人走行き、海綿を取りて酢を含ませ、葦に附けて彼に飲ませんとせるに、
Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa.
49 他の人、措け、エリア來りて彼を救ふや否やを見ん、と云ひ居たり。
Nao waliosalia wakasema, “Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.”
50 イエズス復聲高く呼はりて息絶え給へり。
Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake.
51 折しも[神]殿の幕、上より下まで二に裂け、地震ひ、盤破れ、
Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.
52 墓開け、眠りたる聖人の屍多く起上りしが、イエズスの復活の後、
Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.
53 墓を出でて聖なる都に至り、多くの人に現れたり。
Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi.
54 百夫長及是と共にイエズスを守れる人々、地震と起れる事とを見て甚怖れ、彼は實に神の子なりき、と云へり。
Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, “Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
55 然て此處に、ガリレアよりイエズスに從ひて事へつつありし多くの婦人、立離れて居りしが、
Wanawake wengi waliokuwa wakimfuata Yesu kutoka Galilaya ili kumhudumia walikuwa pale wakitazama kutoka kwa mbali.
56 マグダレナ、マリアと、ヤコボ、ヨセフの母なるマリアと、ゼベデオの子等の母と其中に在りき。
Miongini mwao walikuwa Mariamu Magdarena, Mariamu mama yake Yakobo na Joseph, na mama wa watoto wa Zebedayo
57 日暮に及びて、アリマテアの富者ヨゼフと云へる者來り、己もイエズスの弟子なりければ、
Ilipofika jioni, alikuja mtu tajiri kutoka Arimathayo, aliyeitwa Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
58 ピラトに至りてイエズスの屍を乞ひたるに、ピラト之を付す事を命ぜしかば、
Alimwendea Pilato na kuuomba mwili wa Yesu. Kisha Pilato aliagiza apate kupewa.
59 ヨゼフ屍を取りて浄き布に包み、
Yusufu aliuchukua mwili akaufunga na nguo ya sufi safi,
60 磐に鑿りたる新しき墳に納め、其の墳の入口に大なる石を転ばして去れり。
na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.
61 マグダレナ、マリアと他のマリアとは其處に在りて、墳に向ひて坐し居たり。
Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walikuwa pale, wamekaa kuelekea kaburi.
62 翌日、即ち用意日の次の日、司祭長ファリザイ人等、ピラトの許に集ひ至りて
Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku baada ya maandalio, wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikusanyika pamoja kwa Pilato.
63 云ひけるは、君よ、我等思出したり、彼僞者尚存命せし時、我三日の後復活せんと云ひしなり。
Wakamwambia, “Bwana, tunakumbuka kuwa wakati yule mdanganyifu alipokuwa hai, alisema, 'Baada ya siku tatu atafufuka tena.'
64 然れば命じて三日目まで墳を守らせよ、恐らくは其の弟子等來りて之を盗み、死より復活せりと人民に云はん、然らば後の惑は前よりも甚しかるべし、と。
Kwahiyo, agiza kwamba kaburi lilindwe salama mpaka siku ya tatu. Vinginevyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kumwiba na kusema kwa watu, 'Amefufuka kutoka wafu.' Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”
65 ピラト彼等に向ひ、汝等に番兵あり、往きて思ふ儘に守れと云ひければ、
Pilato akawaambia, “Chukueni walinzi. Nendeni mkafanye hali ya usalama kama muwezavyo.”
66 彼等往きて石に封印し、番兵に墳を守らせたり。
Hivyo walikwenda na kufanya kaburi kuwa salama, jiwe liligongwa mhuri na kuweka walinzi.

< マタイの福音書 27 >