< マタイの福音書 23 >

1 其時イエズス群衆と弟子とに語りて、
Baadaye aliongea na umati wa watu na wanafunzi wake. Akasema,
2 曰ひけるは、律法學士とファリザイ人とはモイゼの講座に坐せり。
“Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa.
3 然れば彼等の汝等に云ふ所は、悉く守りて行へ、然れど彼等の行に倣ひて行ふこと勿れ、彼等は言ひて而も行はざればなり。
Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya.
4 即彼等は、重く擔ひ難き荷を括りて人の肩に載すれど、己が指先にて之を動かす事をすら否む。
Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba.
5 其凡ての行は人に見られん為にして、即其経牌を闊くし、其繸を大くす。
Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao.
6 また宴席にては上席、會堂にては上座、
Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi,
7 衢にては人の敬禮、又ラビと呼ばるる事を好む。
na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa “Walimu” na watu.
8 汝等はラビと呼ばるる事勿れ、汝等の師は一個にして、汝等は皆兄弟なればなり。
Lakini ninyi hampaswi kuitwa “Walimu,” Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu.
9 又地上の人を汝等の父と稱ふること勿れ、汝等の父は天に在す一個のみなればなり。
Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni.
10 又指導師と稱へらるること勿れ、汝等の指導師は一個にして、即キリストなればなり。
Wala msije kuitwa 'walimu,' kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo.
11 汝等の中最大なる者は汝等の僕となるべし。
Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.
12 自驕る人は下げられ、自遜る人は上げらるべし。
Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.
13 禍なる哉汝等、僞善なる律法學士、ファリザイ人等よ、其は人の前に天國を閉ぢ じて、己も入らず、入りつつある人々をも入らしめざればなり。
Lakini ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnawafungia watu ufalme wa mbinguni. Nanyi hamwezi kuuingia, na hamwaruhusu wanaoingia kufanya hivyo.
14 禍なる哉汝等、僞善なる律法學士ファリザイ人等よ、其は長き祈を唱へて、寡婦等の家を食盡せばなり。汝等は是に由りて最厳しき審判を受けん。
(Zingatia: Msitari wa 14 hauonekani katika nakala bora za kale. Baadhi ya nakala huongeza msitari huu baada ya msitari wa 12. Msitari wa 14 “Ole wenu wandishi na Mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawameza wajane”).
15 禍なる哉汝等、僞善なる律法學士ファリザイ人等よ、其は一人の信者を作らんとて海陸を歴巡り、既に作れば、之を己に倍せる地獄の子と為せばなり。 (Geenna g1067)
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnavuka ngambo ya bahari na kufika kumfanya mtu mmoja aamini yale mnayoyafundisha, na anapokuwa kama ninyi, mnamfanya mara mbili mwana wa jehanamu kama ninyi wenyewe mlivyo. (Geenna g1067)
16 禍なる哉汝等、瞽者なる手引よ、汝等は云ふ、「総て人[神]殿を指して誓ふは事にも非ず、[神]殿の黄金を指して誓はば果さざるべからず」と。
Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Yeyote aapaye kwa hekalu, si kitu. Lakini anayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa na kiapo chake.
17 愚にして瞽なる者ども哉、孰か大なるぞ、黄金か、将黄金を聖ならしむる[神]殿か。
Enyi vipofu wapumbavu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhahabu au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu kwa Mungu?
18 [汝等は又云ふ]「総て人祭壇を指して誓ふは事にも非ず、其上なる供物を指して誓はば果さざるべからず」と。
Na, yeyote aapaye kwa madhabahu, si kitu. Bali anayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amefungwa na kiapo chake.
19 瞽者等よ、孰れか大なるぞ、供物か、将供物を聖ならしむる祭壇か。
Enyi watu vipofu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu?
20 然れば祭壇を指して誓ふ人は、祭壇と総て其上なる物とを指して誓ふなり。
Kwa hiyo, yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.
21 又総て[神]殿を指して誓ふ人は、[神]殿と其中に住み給ふものとを指して誓ふなり。
Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake.
22 又天を指して誓ふ人は、神の玉座と其上に坐し給ふ者とを指して誓ふなり。
Na yeye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketie juu yake.
23 禍なる哉汝等、僞善なる律法學士ファリザイ人等よ、汝等は薄荷茴香馬芹の十分の一を納めて、而も律法に於て尚重大なる、正義と慈悲と忠實とを遺せり、此事等を為してこそ彼の事をも怠らざるべかりしなれ。
Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka kwa bizali, mnaanaa na mchicha, lakini mnaacha mambo mazito ya sheria- haki, rehema, na imani. Lakini haya mnapaswa kuwa mmeyafanya, na siyo kuacha mengine bila kuyatekeleza.
24 蝐蠉を濾出だして駱駝を呑む瞽者なる手引等よ。
Enyi viongozi vipofu, ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia!
25 禍なる哉汝等、僞善なる律法學士ファリザイ人等よ、其は杯と盤との外を淨めて、内は貪と汚とに充ちたればなり。
Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya vikombe na nje ya sahani, lakini ndani pamejaa dhuluma na kutokuwa na kiasi.
26 汝瞽者なるファリザイ人よ、先杯と盤との内を淨めよ、然らば外も淨くなるべし。
Enyi Mafarisayo vipofu, safisheni kwanza ndani ya kikombe na ndani ya sahani, ili upande wa nje nao pia uwe safi.
27 禍なる哉汝等、僞善なる律法學士ファリザイ人等よ、其は白く塗りたる墓に似たればなり。外は人に麗しく見ゆれども、内は死人の骨と諸の汚とに充てり。
Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo kwa nje huonekana mazuri, lakini kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila kitu kilicho kichafu.
28 斯の如く、汝等も外は義人の如く人に見ゆれども、内は僞善と不義とに充てり。
Vivyo hivyo, nanyi kwa nje mwaonekana wenye haki mbele ya watu, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na udhalimu.
29 禍なる哉汝等、僞善なる律法學士ファリザイ人等よ、汝等は預言者等の墓を建て、義人等の記念碑を飾りて、
Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.
30 曰く、「我等若先祖の時代に在りしならば、預言者等の血[を流す]に與せざりしものを」と。
Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii.
31 斯て汝等は、預言者等を殺しし人の子孫たる事を自證するなり。
Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii.
32 然らば汝等も先祖の量を盈たせよ。
Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.
33 蛇等よ、蝮の裔よ、汝等爭でか地獄の宣告を遁れん。 (Geenna g1067)
Enyi nyoka, wana wa vipiribao, kwa namna gani mtaikwepa hukumu ya jehanamu? (Geenna g1067)
34 然れば看よ、我汝等に預言者、智者、律法學士等を遣はせども、汝等は其或者を殺し、十字架に釘け、或者を汝等の會堂に鞭ちて、街より街に遂迫めん。
Kwahiyo, tazama, nawatuma kwenu manabii, watu wenye hekima, na waandishi. Baadhi yao mtawaua na kuwasulibisha. Na baadhi yao mtawachapa ndani ya masinagogi yenu na kuwafukuza kutoka mji mmoja hadi mwingine.
35 斯て義人アベルの血より、汝等が[神]殿と祭壇との間にて殺ししパラキアの子ザカリアの血に至る迄、総て地上に流されたる義しき血は、汝等の上に歸すべし。
Matokeo ni kwamba juu yenu patatokea damu zote za wenye haki zilizomwagwa duniani, kuanzia damu ya Habili mwenye haki hadi kwa damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliye muua kati ya patakatifu na madhabahu.
36 我誠に汝等に告ぐ、此事皆現代の上に歸すべし。
Kweli, nawaambieni, mambo haya yote yatakipata kizazi hiki.
37 エルザレムよ、エルザレムよ、預言者等を殺し、且汝に遣はされたる人々に石を擲つ者よ、我牝鶏の其雛を翼の下に集むる如く、汝の子等を集めんとせしこと幾度ぞや、然れど、汝之を否めり。
Yerusalemu, Yerusalemu, wewe unayewaua manabii na kuwapiga mawe wale ambao wanatumwa kwako! mara ngapi nimewakusanya watoto wako pamoja kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mbawa zake, lakini haukukubali!
38 看よ、汝等の家は荒廃れて汝等に遺されん。
Tazama, nyumba yako imebaki ukiwa.
39 我汝等に告ぐ、汝等「主の名によりて來る者は祝せられ給へ」と云ふ迄は、今より我を見ざるべし、[と語り給へり]。
Nami nakuambia, Kuanzia sasa na kuendelea hautaniona, hadi utakaposema, 'Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana.”'

< マタイの福音書 23 >