< マタイの福音書 22 >

1 イエズス答へて、又喩を以て語り曰ひけるは、
Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema,
2 天國は恰其子の為に婚筵を開ける王の如し。
“Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe.
3 彼婚筵に招きたる人々を召ばんとて、僕等を遣はしたるに、彼等肯て來らざれば、
Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika.
4 復他の僕等を遣はすとて云ひけるは、招きたる人々に告げて、看よ我既に我が饗筵の準備を為せり、我牛と肥たる畜と、屠られて悉く具はれり、婚筵に臨まれよ、と云へ、と。
Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. “Waambieni wote walioalikwa, Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari, Njoni katika sherehe ya harusi.”
5 然れども彼等之を顧みず、一人は己が作家に、一人は己が商売に往き、
Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara.
6 其他は僕等を捕へ甚く辱めて殺ししかば、
Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadharirisha na kuwaua.
7 王之を聞きて怒り、軍勢を遣はして彼殺人等を亡ぼし、其街を焼払へり。
Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
8 時に王其僕等に云ひけるは、婚筵既に備はりたれども、招かれし人々は[客となるに]堪へざりし故、
Kisha aliwaambia watumishi wake, “Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili.
9 衢に往きて総て遇ふ人を婚筵に招け、と。
Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi.”
10 僕等途々に出でて、遇ふ人を善きも惡きも悉く集めしかば、客は婚筵の場に満ちたり。
Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni.
11 王客を見んとて入來り、一人婚禮の服を着けざる者あるを見て是に向ひ、
Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi!
12 友よ、如何ぞ婚禮の服を着けずして、此處に入りしや、と云ひけるに、彼黙然たりき。
Mfalme alimwuliza, 'Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?' Na mtu huyo hakujibu chochote.
13 王遂に給仕等に云ひけるは、彼の手足を縛りて之を外の暗に投出だせ、其處には痛哭と切歯とあらん、と。
Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, “Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
14 夫召されたる人は多けれども、選まるる人は少し、と。
Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache.”
15 此時ファリザイ人等出でて、イエズスの詞後を捉へんと相謀り、
Ndipo Mafarisayo waliondoka na kupanga jinsi ya kumkamata Yesu katika maneno yake mwenyewe.
16 己が弟子等をヘロデの党と共に遣はして、云はせけるは、師よ、汝が眞實にして、眞理によりて神の道を教へ、且人に依怙贔屓せざるを以て誰にも憚らざるは、我等の知れる所なり。
Ndipo walipowatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode. Na walimwambia Yesu, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu wa kweli, na kwamba unafundisha matakwa ya Mungu katika ukweli. Haujali maoni ya mtu mwingine na hauoneshi upendeleo kwa watu.
17 然ればセザルに貢を納むるは可や否や、思ふ所を我等に告げよ、と。
Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?”
18 イエズス彼等の狡猾を知りて曰ひけるは、僞善者よ、何ぞ我を試むる。
Yesu alifahamu uovu wao na akasema, “Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki?
19 貢の貨を我に見せよ、と。彼等デナリオを差出だしたるに、
Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi.” Ndipo wakamletea dinari.
20 イエズス曰ひけるは、此像と銘とは誰のなるか、と。
Yesu akawauliza, “Sura na jina hili ni vya nani?”
21 彼等セザルのなりと云ふ。時にイエズス曰ひけるは、然らばセザルの物はセザルに歸し、神の物は神に歸せ、と。
Wakamjibu, “Vya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu.”
22 彼等聞きて感嘆し、イエズスを離れて去れり。
Waliposikia hivyo walishangaa. Kisha walimwacha na kwenda zao.
23 復活なしと主張せるサドカイ人等、此日イエズスに近づき、問ひて、
Siku hiyo baadhi ya Masadukayo walikuja kwa Yesu, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu. Wakamwuliza,
24 云ひけるは、師よ、モイゼ曰く、「人若子なくして死なば、其兄弟彼が妻を娶りて、兄弟の為に子を挙ぐべし」と、
wakisema, “Mwalimu, Musa alisema, Ikiwa mtu amefariki bila kuzaa watoto, ndugu yake na amrithi huyo mwanamke na ampatie mtoto kwa ajili ya ndugu yake.
25 然るに我等の中七人の兄弟ありしに、兄妻を娶りて死し、子なかりしかば、其妻を弟に遺ししが、
Walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa na kisha akafariki bila kuzaa watoto. Akamwachia mke nduguye.
26 其第二第三より第七まで同じ様にして、
Kisha ndugu yake wa pili naye akafanya vivyo hivyo, kisha yule wa tatu, ikawa hivyo hadi kwa yule wa saba.
27 最後に婦も亦死せり。
Baada ya kufanya hivyo wote, yule mwanamke naye alifariki.
28 然れば復活の時に當りて、此婦は七人の中誰の妻たるべきか、其は皆彼を娶りたればなり。
Sasa katika ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani katika ndugu hao saba? Kwa sababu wote walimuoa.”
29 イエズス答へて曰ひけるは、汝等聖書をも神の力をも知らずして誤れり。
Lakina Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Mnakosea, kwa sababu hamjui Maandiko wala nguvu za Mungu.
30 復活の時、人は娶らず嫁がず、天に於る神の使等の如くならん。
Kwa kuwa katika ufufuo, watu hawaoi wala kuolewa. Badala yake watu huwa kama malaika huko mbinguni.
31 死人の復活に就きては、汝等神より云はれし所を読まざりしか。
Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjawahi kusoma kile ambacho Mungu alikisema kwenu, akisema,
32 即汝等に曰はく、「我はアブラハムの神、イザアクの神、ヤコブの神なり」と。死者の神には非ず、生者の[神]にて在す、と。
Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.”
33 群衆之を聞きて、其教を感嘆せり。
Wakati kusanyiko waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho yake.
34 然てファリザイ人等、イエズスがサドカイ人を閉口せしめ給ひしを聞きて相集まりしが、
Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja.
35 中に一人の律法學士イエズスを試みて問ひけるは、
Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu.
36 師よ律法に於て大なる掟は何れぞや。
“Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?”
37 イエズス曰ひけるは、「汝、心を盡し、霊を盡し、意を盡して汝の神にて在す主を愛すべし」、
Yesu akamjibu, “Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
38 是最大なる第一の掟なり。
Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.
39 第二も亦是に似たり、「汝の近き者を己の如く愛すべし」。
Na ya pili inafanana na hiyo- Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
40 凡ての律法と預言者とは此二の掟に據るなり。
Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili.”
41 ファリザイ人の集れるに、イエズス問ひて、
Na Mafarisayo walipokuwa bado wamejikusanya pamoja, Yesu aliwauliza swali.
42 曰ひけるは、汝等キリストに就きて如何に思ふぞ、誰の子なるか、と。彼等、ダヴィドの子なり、と云ひければ、
Akisema, “J! e, Mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?” Nao wakamjibu, “Ni mwana wa Daudi.”
43 イエズス曰ひけるは、然らばダヴィド[聖]霊によりて彼を主と稱ふるは如何、
Yesu akawajibu, “Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana, akisema,
44 曰く「主我主に曰へらく、我汝の敵を汝の足台と為すまで、我右に坐せよ」と、
'Bwana alimwambia Bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya maadui zako wawekwe chini ya miguu yako.”'?”
45 然ればダヴィド彼を主と稱ふるに、彼爭でか其子ならんや、と。
Kama Daudi anamwita Kristo “Bwana,” jinsi gani atakuwa mtoto wake?”
46 皆誰一言もイエズスに答ふること能はず、此日より復敢て問ふ者なかりき。
Hakuna aliyeweza kumjibu neno tena, na hakuna aliyethubutu tena kumwuliza maswali zaidi tangu siku hiyo na kuendelea.

< マタイの福音書 22 >