< マタイの福音書 17 >

1 六日の後イエズス、ペトロとヤコボと其兄弟ヨハネとを別に、高き山に連行き給ひしに、
Siku sita baadaye Yesu aliwachukua pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, na akawachukua mpaka juu ya mlima mrefu wao wenyewe.
2 彼等の前にて御容變り、御顔は日の如く輝き、其衣服は雪の如く白くなれり。
Alibadilishwa mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua, na nguo zake zilionekana zenye kung'aa kama nuru.
3 折しもモイゼとエリアと、彼等に現れてイエズスと語り居りしが、
Tazama, pale walitokea Musa na Eliya wakiongea naye.
4 ペトロ答へてイエズスに云ひけるは、主よ、善哉我等が此處に居る事。思召ならば、此處に三の廬を造り、一は汝の為、一はモイゼの為、一はエリアの為にせん、と。
Petro akajibu na kumwambia Yesu, “Bwana, ni vema kwetu sisi kuwepo mahali hapa. Kama ukitamani, nitajenga hapa vibanda vitatu - kimoja chako, na kimoja kwa ajili ya Musa, na kimoja kwa ajili ya Eliya.”
5 彼尚語れるに、折しも輝ける雲彼等を蔽ひ、雲より聲して曰はく、「是ぞ能く我心を安んぜる我愛子なる、是に聴け」、と。
Wakati anaongea, tazama wingu jeupe likawatia kivuli, na tazama, ikatokea sauti toka kwenye wingu, ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye. Msikilizeni yeye.”
6 弟子等聴きつつ倒伏し、懼るる事甚しかりき。
Wanafunzi waliposikia hayo, wakaanguka kifudifudi na wakaogopa sana.
7 イエズス近づきて彼等に触れ、起きよ、懼るること勿れ、と曰ひしかば、
Kisha Yesu akaja akawagusa na kusema, “Inukeni wala msiogope.”
8 彼等目を翹げしに、イエズスの外誰をも見ざりき。
Nao wakainua nyuso zao juu lakini hawakumwona mtu isipokuwa Yesu pekee.
9 彼等が山を下る時、イエズス是を戒めて、人の子死人の中より蘇る迄は、汝等が見し事を誰にも語ること勿れ、と曰ひしに、
Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akasema, “Msitoe habari ya maono hayo mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka katika wafu.”
10 弟子等問ひて云ひけるは、然らばエリア先に來るべし、と律法學士等の云へるは何ぞや。
Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, “Ni kwanini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza?
11 答へて曰ひけるは、實にエリアは來りて萬事を改むべし。
Yesu akawajibu na kusema, “Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote.
12 但我汝等に告ぐ、エリアは既に來れり、然れど人々之を識らず、而も縦に遇へり。斯の如く、人の子も亦彼等より苦を受けんとす、と。
Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao.”
13 是に於て弟子等、是洗者ヨハネを斥して曰ひしものなる事を暁れり。
Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji.
14 イエズス群衆の處に來り給ひしに、或人是に近づき、前に跪きて云ひけるは、
Walipofika katika umati wa watu, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia,
15 主よ、我子を憐み給へ、癲癇にて屡火の中に倒れ、苦しむこと甚し、
“Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji.
16 之を汝の弟子等に差出したれど、彼等は醫すこと能はざりき、と。
Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.
17 イエズス答へて、嗚呼不信邪惡の代なる哉。我何時まで汝等と共に居らんや、何時まで汝等を忍ばんや。彼を我に携へ來れ、と曰ひて、
Yesu akajibu akisema, “Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu.”
18 惡魔を戒め給ひしかば、惡魔出でて子は即時に痊えたり。
Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile.
19 時に弟子等竊にイエズスに近づきて、我等が之を逐出す能はざりしは何故ぞ、と云ひしに、
Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, “Kwanini hatukuweza kumfukuza?”
20 イエズス曰ひけるは、汝等の不信仰に由れり。我誠に汝等に告ぐ、汝等若芥種ほどの信仰だにあらば、此山に向ひて、此處より彼處に移れと云はんに、山移らん、斯て汝等に能はざる事なからん。
Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.
21 然れど此類は、祈祷と断食とに由らざれば逐出されざるなり、と。
(Zingatia: Maneno ya msitari wa 21 “Lakini, aina hii ya pepo haiwezekani kutoka, ila kwa maombi na Kufunga” hayaonekani katika nakala bora za kale).
22 弟子等ガリレアに居れるに、イエズス曰ひけるは、人の子は人々の手に付されんとす、
Wakati wakiwa bado Galilaya, Yesu akawaambia Wanafunzi wake, “Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu.
23 彼等は之を殺すべく、斯て三日目に蘇るべし、と。弟子等憂ふる事甚しかりき。
Na watamwua, na siku ya tatu atafufuka.” Wanafunzi walihuzunika sana.
24 彼等カファルナウムに來りし時、二ドラクマ銀貨を取立つる人々ペトロに近づき、汝等の師は二ドラクマ銀貨を納めざるか、と云ひしかばペトロ、
Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, “Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?”
25 納む、と云ひしが、頓て家に入りしに、イエズス先ちて之に曰ひけるは、シモンよ汝如何に思ふぞ、世の帝王は、貢又は税を誰より取るぞ、己が子等よりか、他人よりか、と。
Akasema, “Ndiyo” Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, “Unafikiria nini Simon? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawa kutoka kwa wageni?
26 ペトロ、他人より取るなり、と云ひしに、イエズス曰ひけるは、然らば子等は自由なり。
Na wakati Petro aliposema, “Kutoka kwa wageni” Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji.
27 然れど彼等を躓かせざる為に、汝湖に往きて釣を垂れよ、さて初に上る魚を取りて其口を開かば、スタテル銀貨を得べし、之を取りて我と汝との為に彼等に納めよ、と。
Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.

< マタイの福音書 17 >