< マタイの福音書 15 >

1 時に、エルザレムより律法學士とファリザイ人と來り、イエズスに近づきて云ひけるは、
Ndipo Mafarisayo na waadishi walikuja kwa Yesu kutoka Yerusalemu. Na kusema,
2 汝の弟子等は何故に古人の傳を犯すぞ。蓋麪を食する時に手を洗はざるなり、と。
“Kwa nini wanafunzi wanayahalifu mapokeo ya wazee? Kwa kuwa hawanawi mikono yao wanapokuwa wanakula chakula.''
3 答へて曰ひけるは、汝等も亦己が傳の為に神の掟を犯すは何ぞや、蓋神曰く、
Yesu akawajibu na kuwaambia, “Nanyi kwa nini mnaihalifu sheria ya Bwana kwa ajili ya mapokeo yenu?
4 「父母を敬へ。又父或は母を詛ふ人は殺さるべし」と。
Kwa kuwa Mungu alisema, 'Mheshimu baba yako na mama yako; na 'Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.'
5 然るに汝等は云ふ、誰にても父或は母に向ひて、我献物は皆汝の為ならんとだに云へば、
Lakini ninyi husema, 'Kila amwambiaye baba yake na mama yake, '“Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kutoka kwa Mungu,'''
6 其父或は母を敬はずして可なりと、斯て汝等は己が傳の為に神の掟を空しくせり。
“Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
7 僞善者よ、イザヤは汝等に就きて能く預言して、
Enyi wanafiki, ni vema kama Isaya alivyo tabiri juu yenu aliposema,
8 云らく「此人民は唇に我を敬へども、其心は我に遠ざかり、
'Watu hawa wananiheshimu mimi kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.
9 人の訓戒を教へて徒に我を尊ぶなり」と。
Wananiabudu bure, kwa sababu wanafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”'
10 イエズス群衆を召集めて曰ひけるは、
Ndipo akawaita makutano na kuwaambia,” Sikilizeni na mfahamu
11 汝等聞きて暁れ、
Hakuna kitu kiingiacho mdomoni mwa mtu na kumfanya najisi. Bali, kile kitokacho kinywani, hiki ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.''
12 口に入る物人を汚すに非ず、口より出づる者こそ人を汚すなれ、と。其時弟子等近づきて云ひけるは、ファリザイ人が此言を聞きて躓けるを知り給ふか。
Ndipo wanafunzi wakamwendea na kusema na Yesu, “Je!, Unafahamu Mafarisayo walipolisikia lile neno walikwazika?”
13 イエズス答へて曰ひけるは、総て我天父の植ゑ給はざる植物は抜かるべし、
Yesu aliwajibu na kusema, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hajaupanda utang'olewa.
14 汝等彼人々を措け、彼等は瞽者にして瞽者の手引なり、瞽者若瞽者を手引せば二人とも坑に陥るべし、と。
Waacheni pekee, wao ni viongozi vipofu. Kama mtu kipofu atamuongoza kipofu mwenzake, wote wawili wataanguka shimoni.”
15 ペトロ是に答へて、此喩を我等に釈き給へ、と云ひしかば、
Petro akajibu na kumwambia Yesu,” Tuelezee mfano huu kwetu,
16 イエズス曰ひけるは、汝等猶智恵なき者なるか、
Yesu akajibu, ''Nanyi pia bado hamuelewi?
17 総て口に入る物は腹に至りて厠に落つと暁らざるか、
Ninyi hamuoni kuwa kila kiendacho mdomoni hupitia tumboni na kwenda chooni?
18 然れど口より出づる物は、心より出でて人を汚すなり、
Lakini vitu vyote vitokavyo mdomoni hutoka ndani ya moyo. Ndivyo vitu vimtiavyo mtu unajisi.
19 即ち惡念人殺姦淫私通偸盗僞證冒涜は心より出づ、
Kwa kuwa katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi.
20 是等こそ人を汚すものなれ、然れど手を洗はずして食する事は人を汚さざるなり、と。
Haya ndiyo mambo yamtiayo mtu unajisi. Lakini kula bila kunawa mikono hakumfanyi mtu kuwa najisi.”
21 イエズス此處を去りて、チロとシドンとの地方に避け給ひしに、
Ndipo Yesu akatoka mahali pale na akajitenga kuelekea pande za miji ya Tiro na Sidoni.
22 折しもカナアンの或婦其地方より出で、叫びて、主よ、ダヴィドの子よ、我を憫み給へ、我が女甚く惡魔に苦しめらる、と云へるに、
Tazama akaja mwanamke Mkanani kutoka pande hizo. Akapaza sauti akisema, ''Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu anateswa sana na pepo.''
23 イエズス一言も答へ給はざれば、弟子等近づきて、彼婦我等の後に叫ぶ、彼を去らしめ給へ、と請へども、
Lakini Yesu hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakaja wakimsihi, wakisema, ''Muondoe aende zake, maana anatupigia kelele.''
24 イエズス答へて、我は唯イスラエルの家の迷へる羊に遣はされしのみ、と曰へり。
Yesu aliwajibu na kusema, Sikutumwa kwa mtu yeyoye isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.''
25 然るに婦來り禮拝して、主よ、我を助け給へ、と云ひしに、
Lakini alikuja na kuinama mbele yake, akisema, ''Bwana nisaidie.''
26 答へて、子等の麪を取りて犬に投與ふるは可からず、と曰ひしかば、
Alimjibu na kusema, “Siyo vema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa,”
27 婦云ひけるは、主よ、然り、然れども子犬も其主人の食卓より落つる屑を食ふなり、と。
Akasema, “Ndiyo, Bwana, hata hivyo mbwa wadogo hula chakula kiagukacho mezani mwa Bwana wao.”
28 イエズス遂に彼に答へて、嗚呼婦よ、大なる哉汝の信仰、望める儘に汝に成れと、曰ひければ、其女即時に痊えたり。
Ndipo Yesu akajibu na akisema “Mwanamke, imani yako ni kubwa. Na ifanyike kwako kama utakavyo.” Na binti yake alikuwa ameponywa katika wakati huo.
29 イエズス此處を過ぎて、ガリレアの湖辺に至り、山に登りて坐し給ひければ、
Yesu aliondoka mahali pale na kwenda karibu na bahari ya Galilaya. Kisha alienda juu ya mlima na kuketi huko.
30 夥しき群衆あり、唖者瞽者跛者不具者其外多くの者を携へて彼に近づき、其足下に放置きしに、イエズス是等を醫し給へり。
Kundi kubwa likaja kwake. Na kumletea viwete, vipofu, bubu, vilema na wengine wengi, waliokuwa wagonjwa. Waliwaweka katika miguu ya Yesu na akawaponya.
31 然れば群衆は唖者の言ひ、跛者の歩み、瞽者の見ゆるを見て感嘆し、光榮をイスラエルの神に歸し奉れり。
Nao umati wakashangaa walipoona mabubu wakiongea, na vilema wakifanywa wazima, viwete wakitembea, na vipofu wakiona. Walimsifu Mungu wa Israeli.
32 時にイエズス、弟子等を召集めて曰ひけるは、我[此]群衆を憐む、蓋忍びて我と共に居る事既に三日にして食すべき物なし、我之を空腹にして去らしむるを好まず、恐らくは途にて倒れん、と。
Yesu akawaita wanafunzi wake na kusema, “Nimewaonea huruma umati, kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu bila kula kitu chochote. Sitawaaga waende kwao bila kula, wasije wakazimia njiani.”
33 弟子等云ひけるは、然りとて此荒野にて、斯程の群衆を飽かすべき麪を、我等何處よりか求め得ん。
Wanafunzi wake wakamwambia, “Ni wapi tunaweza kupata mikate ya kutosha hapa nyikani kushibisha umati mkuwbwa hivi?”
34 イエズス曰ひけるは、汝等幾個の麪をか有てる、と。答へて、七と少しの小魚とあり、と云ひしかば、
Yesu akawaambia, “Mna mikate mingapi?” Wakasema, “Saba, na samaki wadogo wachache.”
35 イエズス命じて群衆を地に坐らせ、
Yesu akawaamuru umati uketi chini.
36 七の麪と其魚とを取り、謝して擘き、弟子等に與へ給ひ、弟子等之を人民に與へ、
Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati.
37 皆食して飽足れり。殘の屑を拾ひて七の筐に満ちしが
Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba.
38 食せし者は、婦女と幼童とを除きて四千人なりき。
Wote waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto.
39 イエズス群衆を去らしめ、小舟に乗りてマゲダンの地方に至り給へり。
Kisha Yesu akauaga umati waende zao na akaingia ndani ya mashua na kwenda sehemu za Magadani.

< マタイの福音書 15 >