< マタイの福音書 12 >

1 第一款 イエズスとファリザイ人 其頃、イエズス安息日に當りて[麦]畑を過ぎ給ひしが、弟子等飢ゑて穂を摘み食始めしかば、
Wakati huo Yesu alienda siku ya sabato kupitia mashambani. Wanafunzi wake walikuwa na njaa na wakaanza kuyavunja masuke na kuyala.
2 ファリザイ人之を見てイエズスに向ひ、看よ、汝の弟子等安息日に為すべからざる事を為すぞ、と云ひしに、
Lakini Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu “Angalia wanafunzi wako wanavunja sheria wanatenda siku yasiyo yuhusiwa siku ya Sabato''
3 イエズス曰ひけるは、ダヴィドが己及伴へる人々の飢ゑし時に為しし事を、汝等読まざりしか。
Lakini Yesu akawaambia, “Hamjasoma jinsi Daudi aliyoyafanya, wakati alipokuwa na njaa, pamoja na watu aliokuwa nao?
4 即彼は神の家に入り、司祭ならでは、彼も伴へる人々も食すべからざる、供の麪を食せしなり。
Namna alivyoingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate ya wonyesho, ambayo ilikuwa siyo halali kwake kuila na wale aliokuwa nao, ila halali kwa Makuhani?
5 又、安息日に司祭等[神]殿にて安息を犯せども罪なし、と律法にあるを読まざりしか。
Bado hamjasoma katika sheria, kwamba katika siku ya Sabato Makuhani ndani ya hekalu huinajisi Sabato, lakini hawana hatia?
6 我汝等に告ぐ、[神]殿よりも大なるもの此處に在り。
Lakini nasema kwenu kuwa aliye mkuu kuliko hekalu yuko hapa.
7 汝等若「我が好むは憫なり、犠牲に非ず」とは何の謂なるかを知らば、罪なき人を罪せざりしならん、
Kama mngalijua hii ina maanisha nini; nataka rehema na siyo dhabihu; msingaliwahukumu wasio na hatia,
8 其は人の子は亦安息日の主なればなり、と。
Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”
9 イエズス此處を去りて、彼等の會堂に至り給ひしに、
Kisha Yesu akatoka pale akaenda katika sinagogi lao.
10 折しも隻手痿たる人あり。彼等イエズスを訟へんとて、安息日に醫すは可きか、と問ひしかば、
Tazama kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Mafarisayo wakamuuliza Yesu, wakisema. “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?” ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi.
11 イエズス曰ひけるは、汝等の中一頭の羊有てる者あらんに、若其羊安息日に坑に陥らば、誰か之を取上げざらんや、
Yesu akawaambia, “Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja, na huyu kondoo akaanguka ndani ya shimo siku ya sabato, hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo?
12 人の羊に優れること幾何ぞや。然れば安息日に善を為すは可し、と。
Je, ni kipi chenye thamani, zaidi kwani, si zaidi ya kondoo! Kwa hivyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.''
13 頓て其人に、手を伸べよ、と曰ひければ、彼伸ばしたるに、其手痊えて他と齊しくなれり。
Kisha Yesu akamwambia yule mtu,” Nyoosha mkono wako” Akaunyoosha, na ukapata afya, kama ule mwingine.
14 斯てファリザイ人出でて、如何にしてかイエズスを亡ぼさんと謀り居るを、
Lakini Mafarisayo wakatoka njena wakapanga jinsi ya kumwangamiza walienda nje kupanga kinyume chake. Walikuwa wakitafuta jinsi ya kumuua.
15 イエズス知りて此處を去り給ひしが、多くの人從ひしかば、悉く彼等を醫し、
Yesu alipoelewa hili aliondoka hapo. Watu wengi walimfuata, na akawaaponya wote.
16 且我を言顕すこと勿れ、と戒め給へり。
Aliwaagiza wasije wakamfanya afahamike kwa wengine,
17 是預言者イザヤによりて云はれし事の成就せん為なり、
kwamba itimie ile kweli, iliyokuwa imesemwa na nabii Isaya, akisema,
18 曰く「是ぞ我選みし我僕、我心に能く適へる最愛の者なる、我彼の上に我霊を置けり。彼は異邦人に正義を告げん。
Tazama, mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, katika yeye nafsi yangu imependezwa. Nitaweka Roho yangu juu yake, na atatangaza hukumu kwa Mataifa.
19 争はず叫ばず、誰も衢に其聲を聞かず、
Hatahangaika wala kulia kwa nguvu; wala awaye yote kusikia sauti yake mitaani.
20 正義を勝利に至らしむるまで、折れたる葦を断たず、煙れる麻を熄す事なからん、
Hatalivunja tete lililochubuliwa; hatazima utambi wowote utoao moshi, mpaka atakapoleta hukumu ikashinda.
21 又異邦人は彼の名を仰ぎ望まん」と。
Na Mataifa watakuwa na ujasiri katika jina lake.
22 時に一人、惡魔に憑かれて瞽ひ口唖なるもの差出されしを、イエズス醫し給ひて、彼言ひ且見るに至りしかば、
Mtu fulani kipofu na bubu, aliyepagawa na pepo aliletwa mbele ya Yesu. Akamponya, pamoja na matokeo ya kwamba mtu bubu alisema na kuona.
23 群衆皆驚きて、是ダヴィドの子に非ずや、と云へるを、
Makutano wote walishangaa na kusema,”Yaweza mtu huyu kuwa mwana wa Daudi?”
24 ファイリザイ人聞きて、彼が惡魔を逐払ふは、唯惡魔の長ベエルゼブブに籍るのみ、と云へり。
Lakini pindi Mafarisayo waliposikia muujiza huu, walisema, “Huyu mtu hatoi pepo kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa kwa nguvu za Belzebuli, mkuu wa pepo.
25 イエズス彼等の心を知りて曰ひけるは、総て分れ争ふ國は亡びん、又総て分れ争ふ町と家とは立たじ。
“Lakini Yesu alifahamu fikra zao na kuwaambia, “Kila ufalme uliogawanyika wenyewe huharibika, na kila mji au nyumba inayogawanyika yenyewe haitasimama.
26 サタン若サタンを逐払はば、自分るるなり、然らば其國如何にしてか立つべき。
Ikiwa Shetani, atamwondoa Shetani, basi anajipinga katika nafsi yake mwenyewe.
27 我若ベエルゼブブに籍りて惡魔を逐払ふならば、汝等の子等は誰に籍りて逐払ふぞ、然れば彼等は汝等の審判者となるべし。
Ni namna gani ufalme wake utasimama? Na kama natoa pepo kwa nguvu za Belizabuli, wafuasi wenu huwatatoa kwa nija ya nani? Kwa ajili ya hili watakuwa mahakimu wenu.
28 然れど我若神の霊に籍りて惡魔を逐払ふならば、神の國は汝等に格れるなり。
Na kama natoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekjua kwenu.
29 又人先強き者を縛るに非ずんば、爭でか強き者の家に入りて其家具を掠むることを得ん、[縛りて]後こそ其家を掠むべけれ。
Na mtu atawezaje kuingia ndani ya nyumba ya mwenye nguvu na kuiba, bila kumfunga mwenye nguvu kwanza? Ndiyo atakapoiba mali yake kutoka ndani ya nyumba.
30 我に與せざる人は我に反し、我と共に歛めざる人は散らすなり。
Yeyote asiye kuwa pamoja nami yuko kinyume changu, naye asiye kusanya pamoja nami huyo hutawanya.
31 故に我汝等に告ぐ、凡ての罪及冒涜は人に赦されん、然れど[聖]霊に對する冒涜は赦されざるべし。
Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa.
32 又総て人の子に對して[冒涜の]言を吐く人は赦されん、然れど聖霊に對して之を吐く人は、此世、後世共に赦されざるべし。 (aiōn g165)
Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, hilo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao (aiōn g165)
33 或は樹を善しとし其果をも善しとせよ、或は樹を惡しとし其果をも惡しとせよ、樹は其果によりて知らるればなり。
Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake zuri, au uuharibu mti na tunda lake, kwa kuwa mti hutambulika kwa tunda lake.
34 蝮の裔よ、汝等惡しければ、爭でか善きを云ふを得ん、口に語るは心に充てる所より出ればなり。
Nyinyi kizazi cha nyoka, nyie ni waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? Kwa kuwa kinywa hunena kutoka katika akiba ya yaliyomo moyoni.
35 善き人は善き庫より善き物を出し、惡しき人は惡しき庫より惡しき物を出す。
Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoka mema, na mtu mwovu katika akiba ovu ya moyo wake, hutoa kilicho kiovu.
36 我汝等に告ぐ、総て人の語りたる無益な言は、審判の日に於て之を糺さるべし。
Nawaambia kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema.
37 其は汝其言によりて義とされ、又其言によりて罪せらるべければなり、と。
Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.”
38 其時數人の律法學士及ファリザイ人、彼に答へて云ひけるは、師よ、我等汝の為す徴を見んと欲す、と。
Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema” Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako.”
39 イエズス答へて曰ひけるは、奸惡なる現代は徴を求むれども、預言者ヨナの徴の外は徴を與へられじ。
Lakini Yesu alijibu na kuwaambia, “Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii.
40 即ヨナが三日三夜魚の腹に在りし如く、人の子も三日三夜地の中に在らん。
Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.
41 ニニヴの人々は、審判の時現代と共に立ちて之を罪に定めん、彼等はヨナの説教によりて改心したればなり、見よ、ヨナに優れるもの茲に在り。
Watu wa Ninawi watasimama mbele ya hukumu pamoja na kizazi cha watu hawa na watakihukumu. Kwa kuwa walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Yona yuko hapa.
42 南方の女王は、審判の時現代と共に立ちて之を罪に定めん、彼はサロモンの智恵を聴かんとて地の極より來りたればなり、見よ、サロモンに優れるもの茲に在り。
Malkia wa kusini atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki na kukihukumu. Alikuja toka miisho ya dunia kuja kusikia hekima ya Selemani, na tazama, mtu fulani mkuu kuliko Selemani yupo hapa.
43 汚鬼人より出でし時、荒れたる處を巡りて息を求むれども得ず、
Wakati pepo mchafu amtokapo mtu, hupita mahali pasipo na maji akitafuta kupumzika, lakini hapaoni
44 是に於て、出でし我家に歸らんと云ひて、來りて其家の既に空き、掃清められ飾られたるを見るや、
Kisha husema, 'nitarudi kwenye nyumba yangu niliyotoka.' Arudipo hukuta ile nyumba imesafishwa na iko tayari.
45 乃往きて己よりも惡き七の惡鬼を携へ、偕に入りて此處に住む。斯て彼人の末は、前よりも更に惡くなり増る。極惡なる現代も亦斯の如くならん、と。
Kisha huenda na kuwaleta wengine roho wachafu saba walio wabaya zaidi kuliko yeye, huja kuishi wote pale. Na hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa kizazi hiki kiovu.
46 イエズス尚群衆に語り給へる折しも、母と兄弟等と、彼に物語せんとて外に立ちければ、
Wakati Yesu alipokuwa akizungumza na umati tazama, mama yake na ndugu zake walisimama nje, wakitafuta kuongea naye.
47 或人云ひけるは、看よ、汝の母、兄弟汝を尋ねて外に立てり、と。
Mtu mmoja akamwambia, “Tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe”.
48 イエズス己に告げし人に答へて曰ひけるは、誰か我母、誰か我兄弟なるぞ、と。
Lakini Yesu alijibu na kumwambia aliyemjulisha, “Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?”
49 即手を弟子等の方に伸べて曰ひけるは、是ぞ我母我兄弟なる、
Naye alinyoosha mkono wake kwa wanafunzi na kusema, “Tazama, hawa ni mama na ndugu zangu!
50 其は誰にもあれ、天に在す我父の御旨を行ふ人、即是我兄弟姉妹母なればなり、と。
Kwa kuwa yeyote afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, mtu huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu”.

< マタイの福音書 12 >