< ルカの福音書 8 >

1 其後イエズス、説教し且神の國の福音を宣べつつ、町々村々を巡廻し給ひければ、十二使徒之に伴ひ、
Ilitokea muda mfupi baadaye kwamba Yesu alianza kusafiri katika miji na jiji mbalimbali, akihubiri na kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu na wale kumi wawili walikwenda pamoja naye,
2 又曾て惡鬼を逐払はれ、病を醫されたる數人の婦人、即ち七の惡魔の其身より出でたる、マグダレナと呼ばるるマリア、
vilevile wanawake fulani waliokuwa wameponywa kutoka kwa roho wachafu na magonjwa mbalimbali. Walikuwa ni Mariamu aliyeitwa Magdalena ambaye alikuwa ametolewa pepo saba.
3 ヘロデの家令クサの妻ヨハンナ及スザンナ、其他多くの婦人ありて、己が財産を以て彼等に供給し居たり。
Yoana mke wa Kuza na meneja wa Herode, Susana, na wanawake wengine wengi, waliotoa mali vyao kwa ajili yao wenyewe.
4 然て夥しき人、町々よりイエズスの許に走集りければ、イエズス喩を以て語り給ひけるは、
Nabaada ya umati wa watu kukusanyika pamoja, wakiwemo na watu waliokuja kwake kutoka miji mbalimbali, akazungumza nao kwa kutumia mifano.
5 種播く人其種を播きに出でしが、播く時或者は路傍に落ちしかば、踏着けられ、空の鳥之を啄めり。
“mpandaji alienda kupanda mbegu, alipokuwa apanda, baadhi ya mbegu hizo ziliangukia kando ya njia zikakanyagwa chini ya miguu, na ndege wa angani wakazila.
6 或者は石の上に落ちしかば、生出たれど、潤なきに由りて枯れたり。
Mbegu zingine zilianguka juu ya udongo wa miamba na zilipoota na kuwa miche zilipooza kwa sababu hakukuwa na unyevunyevu.
7 或者は茨の中に落ちしかば、茨共に長ちて之を蔽塞げり。
Mbegu zingine ziliangukia kwenye miti ya miiba, nayo hiyo miti ya miiba ikakua pamoja na zile mbegu na zikasongwa.
8 或者は沃壌に落ちしかば、生出でて百倍の實を結べり、と。イエズス此事を曰ひて、聞く耳を有てる人は聞け、と呼はり居給へり。
Lakini mbegu zingine ziliangukia kwenye udongo unaofaa na zikazaa mazao mara mia zaidi. “Baada ya Yesu kusema mambo haya, alipaza sauti,”Yeyote aliye na masikio ya kusikia na asikie.”
9 弟子等、此喩を如何にと問ひしに、
Tena wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo,
10 曰ひけるは、汝等は神の國の奥義を知る事を賜はりたれど、他の人は喩を以てせらる、是は彼等が見つつ視えず、聞きつつ暁らざらん為なり。
Yesu akawaambia, “Mmepewa upendeleo wa kujua siri ya ufalme wa Mungu, lakini watu wengine watafundishwa tu kwa mifano, ili kwamba 'wakiona wasione na wakisikia wasielewe.'
11 此喩は斯の如し、種は神の御言なり、
Na hii ndiyo maana ya mfano huu. Mbegu ni neno la Mungu.
12 路傍の者は聞く人々にして、彼等の信じて救はれざらん為、後に惡魔來りて言を其心より奪ふなり。
Mbegu zile zilizoanguka kando kando ya njia ndiyo wale watu wanaolisikia neno, na baadaye mwovu shetani hulichukua mbali kutoka moyoni, ili kwamba wasiamini na kuokolewa.
13 石の上の者は、聞く時に喜びて言を受くれど、己に根無く、暫く信じて、誘の時には退く人々なり。
Kisha na zile zilizoangukia kwenye mwamba ni watu wale wanaosikia neno na kulipokea kwa furaha lakini hawana mizizi yeyote, wanaamini tu kwa muda mfupi, na wakati wa majaribu huanguka.
14 茨の中に落ちしは、聞きたる後、往く往く世の慮と富と快樂とに蔽塞がれて、實を結ばざる人々なり。
Na mbegu zile zilizoangukia kwenye miiba ni watu wanaosikia neno, lakini wanapoendelea kukua husongwa na huduma na utajiri na ubora wa maisha haya na hawazai matunda.
15 然るに沃壌に落ちしは、善良なる心にて、言を聞きて之を保ち、忍耐を以て實を結ぶ人々なり。
Lakini zile mbegu zilizoangukia kwenye udongo mzuri ni wale watu, ambao ni wanyeyekevu na mioyo mizuri, baada ya kulisikia neno hulishikilia na likawa salama na kuazaa matunda ya uvumilivu.
16 誰も燈を點して、器を以て之を覆ひ、或は寝台の下に置く者はあらず、入來る者に明を見せん為に、之を燭台の上に置く。
Sasa, hakuna hata mmoja, anayewasha taa na kuifunika kwa bakuli au kuiweka chini ya kitanda. Badala ya kuiweka kwenye kinara cha taa ili kwamba kila mmoja anayeingia apate kuiona.
17 蓋秘して露れざるはなく、隠れて遂に知れず公にならざるはなし。
Kwa kuwa hakuna kitakachojificha ambacho hakitajulikana, au chochote kilicho sirini ambacho hakitajulikana kikiwa kwenye mwanga.
18 此故に汝等聞方に注意せよ。其は有てる人は尚與へられ、有たぬ人は其有てりと思ふ物をも奪はるべければなり、と。
kwa hiyo kuwa makini unapokuwa unasikiliza. Kwa sababu aliye nacho, kwake ataongezewa zaidi, lakini asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho kitachukuliwa.”
19 然てイエズスの母、兄弟、逢はんとて來りしかど、群衆の為に近づくこと能はざりしかば、
baadaye mama yake Yesu na ndugu zake wakaja kwake hawakaribia kwa sababu ya umati wa watu.
20 汝の母、兄弟汝に逢はんとて外に立てり、と告ぐる者ありしに、
Na akataarifiwa, “Mama yako na ndugu zako wako pale nje wanahitaji kukuona wewe.
21 イエズス答へて人々に曰ひけるは、神の御言を聴き且行ふ人、是我母、兄弟なり、と。
Lakini, Yesu akajibu akasema “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”
22 一日イエズス、弟子等と共に小舟に乗り給ひしに、我等湖の彼方に渡らん、と曰ひて軈て乗出せり。
Ilitokea siku moja kati ya siku zile Yesu na wanafunzi wake alipanda kwenye mtumbwi, na akawaambia, “Na tuvuke ng'ambo ya pili ya ziwa.” Wakaandaa mashua yao.
23 斯て渡る間にイエズス眠り給ひしが、暴風湖に吹下し來り、水舟に充ちて危かりければ、
Lakini walipoanza kuondoka, Yesu akalala usingizi, na dhoruba kali yenye upepo, na mashua yao ikaanza kujaa maji na walikuwa kwenye katika kubwa sana.
24 弟子等近づきて、師よ、我等亡ぶ、と云ひつつイエズスを覚ましたるに、起きて風と怒涛とを戒め給ひしかば、波風息みて凪となれり。
baadaye wanafunzi wake wakaja kwake na kumwamsha, wakisema, “Bwana mkubwa! Bwana mkubwa! tuko karibu kufa!” Akaamka na akaukemea upepo na mawimbi ya maji vikatulia na kukawa na utulivu.
25 然て、汝等の信仰何處に在る、と曰ひければ、彼等且怖れ且感嘆して、是を誰と思ふぞ、風も湖も、命じ給へば是に從ふよ、と云合へり。
Tena akawaambia, “Imani yenu iko wapi?” Wakaogopa, Walishangaa, wakasemezana kia mmoja na mwenzake,”Huyu ni nani, kiasi kwamba anaamuru hata upepo, na maji na humtii?”
26 又ガリレアに對へるゲラサ人の地方に渡りて、
Wakafika kwenye mji wa Gerasini iliyo upande wa nyuma ya Galilaya.
27 上陸し給ひしに、一箇の人ありて之を迎へたり。彼惡魔に憑かれたる事既に久しくして、衣服をも着ず家にも住まず、墓にのみ居りしが、
Yesu aliposhuka na kukanya kwenye ardhi, mtu fulani kutoka mjini, akakutana naye, na huyu mtu alikuwa na nguvu za giza. Kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, na alikuwa haishi kwenye Nyumba, lakini aliishi kwenye makaburi.
28 イエズスを見るや御前に平伏し、聲高く叫びて、最高き神の御子イエズスよ、我と汝と何の関係かあらん。願くは我を苦しむること勿れ、と云へり。
Alipomwona Yesu akalia kwa sauti, na akaanguka chini mbele yake. kwa sauti kubwa akisema, Nimefanya nini kwako, Yesu mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, Usiniadhibu mimi”
29 是イエズス惡鬼に、此人より出でよ、と命じ給へばなり。蓋彼惡鬼に執へらるる事既に久しく、鎖にて縛られ、桎にて護らるるも、繋を破り、惡魔に駆られて、荒野に往き居たりき。
Yesu akaamuru roho chafu imtoke mtu yule, kwa kuwa mara nyingi amepamgaa. hata kama alikuwa amefungwa minyororo na kubanwa na kuwekwa chini ya ulinzi, alivunja vifungo na kuendeshwa na mapepo mpaka jangwani.
30 イエズス之に問ひて、汝の名は何ぞ、と曰ひしに彼、軍団なり、と云へり、其は之に入りたる惡魔多ければなり。
Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” akajibu akisema, “Legioni” Kwa maana mapepo mengi yameingia kwake.
31 然てイエズスの命じて底なき淵に往かしめ給はざらん事を請ひたりしが、 (Abyssos g12)
Wakaendelea kumsihi usituamuru twende kwenye shimo. (Abyssos g12)
32 其處に多くの豚の群、山にて草を食み居しかば、惡魔等其豚に入るを允されん事を請ひけるに、イエズス之を允し給ひければ、
Kundi la Nguruwe lilikuwa likichunga juu ya kilima, wakamsihi awaruhusu wakaingie kwa hao nguruwe. Na akawaruhusu kufanya hivyo.
33 惡魔等其人より出でて豚に入り、其群周章しく崖より湖に飛入りて溺死せり。
kwa hiyo wale mapepo wakamtoka mtu yule na kuingia kwa wale nguruwe, na lile kundi likakimbia kwenye mwinuko wa mlima mpaka ziwani na wakazama humo.
34 牧者等其成行を見るや迯往きて、町に村に吹聴せしかば、
wale watu waliokuwa wanachunga wale nguruwe walipoona kilichotokea, wakakimbia na wakatoa taarifa pale mjini na nje katika miji iliyowazunguka.
35 人々事の様を見んとて出でしが、イエズスの許に來り、彼惡魔の出でたりし人の、既に衣服を纏ひ心確にして、イエズスの足下に坐せるを見て怖れたり。
Watu waliposikia hayo walienda kuona kilichotokea, na wakaja kwa Yesu na wakamwona mtu ambaye mapepo yalikuwa yamemtoka. alikuwa amevaa vizuri na mwenye akili timamu, amekaa kwenye miguu ya Yesu, na waliogopa.
36 斯て見し人々も亦、惡魔憑の救はれし次第を誰彼に告げしかば、
ndipo mmoja wao aliyeona kilichotokea alianza kuwasimlia wengine jinsi huyu mtu aliyekuwa anaongozwa na mapepo alivyoponywa.
37 ゲラサ地方の人民挙りて、己等より立去り給はん事をイエズスに請へり、是大いに怖れたればなり。然てイエズス船に乗りて歸り給ひしに、
Watu wote wa mkoa wa Wagerasi na maeneo yaliyozunguka walimwomba Yesu aondoke kwao kwa sababu walikuwa na hofu kuu. Na aliingia kwenye mtumbwi ili arudi.
38 惡魔の離れし男伴はん事を願ひしかど、イエズス之を去らして曰ひけるは、
Mtu yule aliyetokwa na pepo alimsihi Yesu kwenda naye, lakini Yesu alimwambia aende na kusema,
39 己が家に歸りて、神が如何ばかり大いなる事を汝に為し給ひしかを告げよ、と。斯くて彼は普く町を廻りて、イエズスの如何ばかり大いなる事を己に為し給ひしか言弘めたり。
“Rudi kwenye nyumba yako na uhesabu yale yote ambayo Mungu amekutendea” Huyu mtu aliondoka, akitangaza pote katika mji wote yale yote ambayo Yesu aliyofanya kwa ajili yake.
40 イエズス歸り給ひしに、人皆待居たりければ、群衆之を歓迎せり。
Na Yesu akarudi, makutano wakamkaribisha, kwa sababu wote walikuwa wanamngoja.
41 折しも名をヤイロと云える人來り、會堂の司なりしが、イエズスの足下に平伏して、己が家に入り給はん事を請へり、
Tazama akaja mtu mmoja anaitwa Yairo ni mmoja kati ya viongozi katika sinagogi. Yairo akaanguka miguuni pa Yesu na kumsihi aende nyumbani kwake,
42 其は己に十二歳ばかりの獨女ありて、将に死なんとすればなり。イエズス往き給ふ途にて、群衆に押蹙られ給へる中に、
kwa sababu alikuwa na mtoto msichana mmoja tu, mwenye umri wa miaka kumi na wibili, na alikuwa katika hali ya kufa. Na alipokuwa akienda, makutano walikuwa wakisongama dhidi yake.
43 十二年來血漏を患へる一人の女、曾て醫者の為に悉く其財産を費したれども、誰の手にも醫され得ざりしが、
Mwanamke mwenye kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili alikuwa pale na alitumia pesa zote kwa waganga, lakini hakuna aliyemponya hata mmoja,
44 後より近づきてイエズスの衣服の総に觸れしかば、其の出血忽止れり。
alikuja nyuma ya yesu na kugusa pindo la vazi lake, na ghafla kutokwa damu kukakoma.
45 イエズス、我に觸れし者は誰ぞ、と曰へば皆否めるを、ペトロ及び之に伴ひたる人々云ひけるは、師よ、群衆押蹙りて汝を煩はすに、猶誰か我に觸れし、と曰ふか。
Yesu akasema, “Nani ambaye kanigusa?” Walipokataa wote, Petro akasema, Bwana Mkubwa, umati wa watu wanakusukuma na wanakusonga.”
46 イエズス曰ひけるは、我に觸れし者あり、我霊能の我身より出でたるを覚ゆればなり、と。
Lakini Yesu akasema, “Mtu mmoja alinigusa, maana nilijua nguvu zimetoka kwangu.”
47 女其隠れざりしを見て慄きつつ、來りてイエズスの足下に平伏し、其觸れし理由と直に痊えたる次第とを公衆の前に明しければ、
Mwanamke alipoona ya kuwa hawezi kuficha alichokifanya, akaanza kutetemeka, akaanguka chini mbele za Yesu alitangaza mbele ya watu wote sababu zilizofanya amguse na vile alivyoponywa gafla.
48 イエズス之に曰ひけるは、女よ汝の信仰汝を救へり、安んじて往け、と。
Kisha akasema kwake, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa Amani.”
49 言未了らざるに、人會堂の司の許に來り、汝の女死せり、師を煩わすこと勿れ、と云ひしに、
Alipokuwa akiendelea kusema, mtu mmoja akaja kutoka kwenye nyumba ya kiongozi wa sinagogi, akisema, “Binti yako amefariki. Usimsumbue mwalimu.”
50 イエズス此言を聞きて女の父に答へ給ひけるは、懼るること勿れ、唯信ぜよ、然らば彼助かるべし、と。
Lakini Yesu aliposikia hivyo, alimjibu, “Usiogope. Amini tu, na ataokolewa.”
51 斯て其家に至り給ひて、ペトロ、ヤコボ、ヨハネ及び女の父母の外、共に入る事を誰にも許し給はず、
Kisha alipoingia kwenye hiyo nyumba, hakuruhusu mtu yeyote kuingia pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, baba yake binti, na mama yake.
52 人皆女の為に泣き且歎き居れるを、泣く勿れ、女は死したるに非ず、寝ねたるなり、と曰ひしに、
Sasa watu wote walikuwa wanaomboleza na kutoa sauti kwa ajili yake, lakini akasema, “Msipige kelele, hajafa, lakini amelala tu.”
53 人々は彼の死したるを知りて、之を嘲笑ひ居たり。
Lakini wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekufa.
54 然るにイエズス、女の手を取り、呼はりて、女起きよ、と曰へば、
Lakini Yeye, akimshika binti mkono, akaita kwa sauti, akisema, “Mtoto, inuka”
55 其霊還りて女直に起きしかば、之に食物を與ふる事を命じ給へり。
roho yake ikamrudia, na akainuka wakati huohuo. Akaamrisha kwamba, apewe kitu furani kwa ili ale.
56 兩親は甚く驚きしが、成りし事を誰にも語るな、とイエズス戒め給へり。
Wazazi wake wakashangaa, lakini aliwaamuru wasimwambie mtu kilichokuwa kimetokea.

< ルカの福音書 8 >