< ルカの福音書 2 >

1 第二項 イエズスキリストの御降誕 其頃、天下の戸籍を取調ぶべしとの詔、セザル、オグストより出しが、
Sasa katika siku hizo, ikatokea kwamba Kaisari Agusto alitoa agizo akielekeza kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi duniani.
2 此戸籍調は、シリノがシリアの総督たりし時に始めたるものなり。
Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio akiwa gavana wa Siria.
3 斯て人皆名を届けんとて、各其故郷に至りけるに、
Hivyo kila mmoja akaenda mjini kwake kuandikishwa sensa.
4 ヨゼフもダヴィド家に属し且其血統なれば、
Naye Yusufu aliondoka pia katika mji wa Nazareti huko Galilaya na akasafiri Yudea katika mji wa Bethlehemu, ujulikanao kama mji wa Daudi, kwa sababu alitokea katika ukoo ya Daudi.
5 既に懐胎せる聘定の妻マリアと共に名を届けんとて、ガリレアのナザレト町よりユデアのベトレヘムと云へるダヴィドの町に上れり。
Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa na alikuwa akitazamia mtoto.
6 其處に居りし程に、マリア産期満ちて、
Sasa ilitokea kwamba, wakiwa kule wakati wake wa kujifungua mtoto ukawadia.
7 家子を生み、布に包みて馬槽に臥させ置きたり。是、旅舎に彼等の居る所なかりし故なり。
Akajifungua mtoto wa kiume, mzaliwa wake wa kwanza, akamzungushia nguo mwilini kumkinga na baridi mtoto. Ndipo akamweka kwenye kihori cha kulishia wanyama, kwa sababu haikuwepo nafasi kwenye nyumba za wageni.
8 然るに此地方に牧者等ありて、夜中交代して己が群を守り居りしが、
Katika eneo hilo, walikuwapo wachungaji walioishi mashambani wakilinda makundi ya Kondoo wao usiku.
9 折しも主の使其傍に立ちて、神の榮光彼等を環照らしたれば、彼等大いに懼れたり。
Ghafla, malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Bwana ukang'aa kuwazunguka, na wakawa na hofu sana.
10 天使彼等に云ひけるは、懼るる事勿れ、其は我人民一般に及ぶべき大いなる喜の福音を汝等に告ぐればなり。
Ndipo malaika akwaambia, “Msiogope, kwasababu nawaletea habari njema ambayo italeta furaha kuu kwa watu wote.
11 蓋今日ダヴィドの町に於て、汝等の為に救主生れ給へり、是主たるキリストなり。
Leo Mwokozi kazaliwa kwaajili yenu mjini mwa Daudi! Yeye ndiye Kristo Bwana!
12 汝等之を以て徴とせよ、即ち布にて包まれ、馬槽に置かれたる嬰兒を見るべし、と。
Hii ndiyo ishara ambayo mtapewa, mtamkuta mtoto amefungwa nguo na amelala kwenye hori la kulishia wanyama.”
13 忽ち夥しき天軍天使に加はりて、神を賛美し、
Ghafla kukawa na jeshi kubwa la mbinguni likaungana na malaika huyo wakamsifu Mungu, wakisema,
14 「最高き處には神に光榮、地には御好意の人々に平安」と唱へたり。
“Utukufu kwa Mungu aliye juu sana, na amani iwe duniani kwa wote ambao anapendezwa nao.”
15 天使等天に去りて後、牧者等云ひけるは、将我等ベトレヘムまで行き、主の我等に示し給へる事の次第を見ん、と。
Ikawa kwamba malaika walipokwisha kuondoka kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezena wao kwa wao, “Twendeni sasa kule Bethlehemu, na tukaone hiki kitu ambacho kimetokea, ambacho Bwana ametufahamisha.”
16 乃ち急ぎ至りて、マリアとヨゼフと馬槽に置かれたる孩兒とに遇へり。
Wakaharakisha kule, na wakamkuta Mariamu na Yusufu, na wakamuona mtoto amelala kwenye hori la kulishia wanyama.
17 然て面りに見て、此孩兒に就きて云はれし事を知らせければ、
Na walipoona hivi, wakawajulisha watu kile walichokuwa wameambiwa kumhusu mtoto.
18 聞ける人皆牧者等より云はるる事を不思議に思ひしが、
Wote waliosikia habari hii wakashangazwa na kile kilichosemwa na wachungaji.
19 マリアは是等の事を悉く心に納めて考合せ居たり。
Lakini Mariamu akaendelea kufikiri kuhusu yote aliyokwisha kuyasikia, akiyatunza moyoni mwake.
20 斯て牧者等は、己に云はれしに違はず、見聞せし一切の事に就きて、神に光榮を歸し、且賛美し奉りつつ歸れり。
Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao.
21 孩兒の割禮を授かるべき八日目に至りて、未胎内に孕らざる前に天使より云はれし如く、名をイエズスと呼ばれ給へり。
Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.
22 第三項 キリスト御幼年 然てモイゼの律法の儘に、マリアが潔の日數満ちて後、[兩親]孩兒を主に献げん為、携へてエルザレムに往けり。
zao zilizotakiwa za utakaso zilipopita, kulingana na sheria ya Musa, Yusufu na Mariamu wakampeleka hekaluni kule Yerusalemu kumweka mbele za Bwana.
23 是主の律法に録して「総て初に生るる男子は、主の為に聖なる者と稱へらるべし」とあるが故にして、
Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, “Kila mwanaume anayefungua tumbo ataitwa aliyetolewa wakfu kwa Bwana.”
24 又主の律法に云はれたる如く、山鳩一雙か、鴿の雛二羽かを犠牲に献げん為なりき。
Wao vilevile walikuja kutoa sadaka kulingana na kile kinachosemwa katika sheria ya Bwana, “Jozi ya njiwa au makinda mawili ya njiwa.”
25 折しもエルザレムに、シメオンと云へる人あり。義人にして神を畏敬し、イスラエル[の民]の慰められん事を待ちて、聖霊の居給ふ所となり、
Tazama, palikuwa na mtu katika Yerusalemu ambaye jina lake alikuwa akiitwa Simeoni. mtu huyu alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Yeye alikuwa akisubiri kwa ajili ya mfariji wa Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 聖霊より、主のキリストを見ざるうちは、死せざる事を示されたりしが、
Ilikuwa imekwisha funuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu kwamba yeye hangelikufa kabla ya kuwomwona Kristo wa Bwana.
27 [聖]霊によりて、[神]殿に至りしに、恰も彼兩親孩兒イエズスを携へ、是が為に律法の慣例に從ひて行はんとて來りければ、
Siku moja alikuja ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ambapo wazazi walimleta mtoto, Yesu, kumfanyia yale yaliyopasa kawaida ya sheria,
28 シメオン孩兒を抱き、神を祝し奉りて云ひけるは、
ndipo Simeoni alimpokea mikononi mwake, na akamsifu Mungu na kusema,
29 主よ、今こそ御言に從ひて僕を安樂に逝かしめ給ふなれ、
“Sasa ruhusu mtumishi wako aende kwa amani Bwana, kulingana na Neno lako.
30 其は我目主の救を見たればなり。
Kwa kuwa macho yangu yameuona wakovu wako,
31 是ぞ主が萬民の前に備へ給ひし者にして、
ambao umeonekana kwa macho ya watu wote.
32 異邦人を照らすべき光、主の民たるイスラエルの光榮なる、と。
Yeye ni nuru kwa ajili ya ufunuo kwa Wamataifa na utukufu wa watu Israeli.”
33 イエズスの父母は、孩兒に就きて云はれたる事を驚嘆したりしが、
Baba na Mama wa mtoto walishangazwa kwa mambo ambayo yalizungumzwa juu yake.
34 シメオン彼等を祝して、母マリアに云ひけるは、此子は、是イスラエルに於て、多くの人の堕落と復活との為に置かれ、且反抗を受くる徴に立てられたり、
Ndipo Simeoni akawabariki na akasema kwa Mariamu mama yake, “Sikiliza kwa makini! Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli na ni ishara ambayo watu wengi wataipinga.
35 汝の魂も剣にて刺貫かるべく、而して多くの心の念顕るべし、と。
Pia ni upanga utakaochoma nafsi yako mwenyewe, ili kwamba mawazo ya mioyo ya wengi yadhihirike”.
36 又アゼル族なるファヌエルの女に、名はアンナ[と云ひて]、既に至極の老年に及べる女預言者あり。處女の時より七年の間、夫と共に在りしに、
Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana,
37 寡婦となりて、齢八十四に至り、[神]殿を離れず、断食と祈祷とを以て晝夜奉事し居りしが、
na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.
38 是も同時に來りて、主を稱賛し、エルザレムに於て、贖罪を待てる人々に孩兒の事を語り居たりき。
Na kwa wakati huo, alikuja pale walipo akaanza kumshukuru Mungu. Aliongea kumhusu mtoto kwa kila mtu ambaye alikuwa akisubiri ukombozi wa Yerusalemu.
39 [兩親は]主の律法の儘に何事をも果し、ガリレアのナザレトなる己が町に歸りしが、
Walipomaliza kila kitu walichotakiwa kufanya kuligana na na sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, mjini kwao, Nazareti.
40 孩兒漸く成長して、智恵に満ち、精神の力彌増し給ひ、神の恩寵其上に在りき。
Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
41 然て過越の大祝日には、兩親年毎にエルザレムに往き居りしが、
Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwaajili ya sikukuu ya Pasaka.
42 イエズス十二歳になり給ひし時、兩親祝日の慣例の儘にエルザレムに上りしに、
Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu.
43 祝日過ぎて歸る時、幼きイエズスはエルザレムに留り給へり。兩親は之を知らず、
Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili.
44 道連の中に在らんと思ひつつ、一日路を往き、然て親族知己の中を求めたれども、逢はざりしかば、
Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao.
45 尋ねつつエルザレムに立歸りしに、
Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo.
46 三日目に、イエズスが[神]殿にて學者の中に坐し、彼等に聞き且問ひ居給へるを見付けたり。
Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
47 聞く人皆其智恵と應答とに驚き居たりしが、
Wote waliomsikia walishangazwa na ufahamu wake na majibu yake.
48 兩親は之を見て感嘆せり。斯て母はイエズスに向ひ、子よ、何故我等に斯る事を為ししぞ。看よ、汝の父と我とは憂ひつつ汝を尋ね居たり、と云ひければ、
Walipomwona, walistaajabu. Mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivi? Sikiliza, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa.”
49 イエズス曰ひけるは、何ぞ我を尋ねたるや。我は我父の事を務むべきを知らざりしか、と。
Akawaambia, “Kwa nini mmekuwa mkinitafuta? Hamkujua kwamba lazima niwe kwenye nyumba ya Baba yangu?
50 兩親は此語給ひし御言を暁らざりき。
Lakini hawakuelewa nini alichomaanisha kwa maneno hayo.
51 然てイエズス彼等と共に下り、ナザレトに至りて彼等に從ひ居給ひしが、母は此総ての事を心に納め居たりき。
Ndipo akaenda pamoja nao mpaka nyumbani Nazareti na alikuwa mtii kwao. Mama yake alihifadhi mambo yote moyoni mwake.
52 斯てイエズス智恵も齢も、神と人とに於る寵愛も次第に彌増し居給へり。
Lakini Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimo, na akazidi kupendwa na Mungu na watu.

< ルカの福音書 2 >