< ヨハネの福音書 21 >

1 其後イエズス、又チベリアデの湖辺にて己を弟子等に現し給ひしが、其現し給ひし次第は次の如し。
Baada ya mambo hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi katika Bahari ya Tiberia; hivi ndivyo alivyojidhihirisha mwenyewe:
2 シモン、ペトロとチヂモと呼ばるるトマと、ガリレアのカナ生れなるナタナエルと、ゼベデオの子等と、尚外に二人の弟子共に在りけるに、
Simon Petro alikuwa pamoja na Thomaso aitwaye Didimas, Nathanaeli wa kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu.
3 シモン、ペトロ、我漁に往く、と云ひしかば彼等、我等も共に往く、と云ひて、皆出行きて船に乗りしに、其夜は何をも獲ざりき。
Simon Petro akawaambia, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Sisi, pia tutaenda nawe.” Wakaenda wakaingia kwenye mashua, lakini usiku huo wote hawakupata chochote.
4 然て天明に至りてイエズス濱に立ち給へり、然りながら弟子等は其イエズスなる事を認めざれば、
Na asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufukweni, nao wanafunzi hawakutambua kuwa alikuwa Yesu.
5 イエズス彼等に向ひ、子等よ肴あるか、と曰ひしに彼等、無しと答へたり。
Kisha Yesu akawambia, “Vijana, mna chochote cha kula?” Nao wakamjibu, “Hapana.”
6 イエズス、網を船の右に下せ、然らば獲物あらん、と曰ひければ、彼等下したるに、魚夥しくして、網を引くこと能はざれば、
Akawambia, “Shusheni wavu upande wa kuume wa mashua, nanyi mtapata kiasi.” Kwa hiyo wakashusha wavu nao hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa cha samaki.
7 イエズスの愛し給へる彼弟子ペトロに向ひて、主なり、と云ひしをシモン、ペトロ、主なりと聞くや、裸なりければ上衣を纏ひて湖に飛入り、
Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, “Ni Bwana.” Naye Simon Petro aliposikia kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa vizuri), kisha akajitupa baharini.
8 他の弟子等は魚の満てる網を引きつつ船にて來れり、陸を距る事遠からず、凡そ五十間許なりければなり。
Wale wanafunzi wengine wakaja kwenye mashua (kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni), nao walikuwa wakivuta zile nyavu zilizokuwa zimejaa samaki.
9 陸に上りて見れば既に炭火ありて、其上に一の魚の乗せられたるあり、又麪ありき。
Walipofika ufukweni, waliona moto wa mkaa pale na juu yake kulikuwa na samaki pamoja na mkate.
10 イエズス彼等に向ひ、汝等が今獲りたる魚を持來れと曰ひしかば、
Yesu akawambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua sasa hivi.”
11 シモン、ペトロ乗りて、大なる魚百五十三尾まで充満たる網を陸に引來りしが、斯くまで夥しかりしかど網は裂けざりき。
Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika.
12 イエズス彼等に、來りて食せよ、と曰ひしに、弟子等其主なることを知りて、汝は誰ぞと敢て問ふ者一人もなかりしが、
Yesu akawaambia, “Njoni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanfunzi aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua kuwa alikuwa ni Bwana.
13 イエズス近づき給ひ、麪を取りて彼等に與へ、魚も亦同じ様にし給へり。
Yesu akaja, akachukua ule mkate, kisha akawapa, akafanya vivyo hivyo na kwa wale samaki.
14 イエズスが死者の中より復活して、其弟子等に現れ給ひしは是にて既に三度目なりき。
Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Yesu kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka toka wafu.
15 然て彼等食したるに、イエズスシモン、ペトロに曰ひけるは、ヨハネの[子]シモン、汝は此人々に優りて我を愛するか、と。彼、主よ、然り、我が汝を愛するは汝の知り給ふ所なり、と云ひしかばイエズス、我羔を牧せよ、と曰へり。
Baada ya kuwa wamefungua kinywa, Yesu akamwambia Simon Petro, “Simon mwana wa Yohana je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana; “Wewe wajua kuwa mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wanakondoo wangu.”
16 又再び、ヨハネの[子]シモン、汝は我を愛するか、と曰ひしに、彼、主よ、然り、我が汝を愛するは汝の知り給ふ所なり、と云ひしかばイエズス我羔を牧せよ、と曰へり。
Akamwambia mara ya pili, “Simon mwana wa Yona, je, wanipenda?” Petro akamwambia, “Ndiyo, Bwana; wewe wajua kuwa nakupenda. “Yesu akamwambia, “Chunga kondoo wangu.”
17 三度之に向ひて、ヨハネの[子]シモン、汝は我を愛するか、と曰ひしかば、ペトロは、我を愛するかと三度まで言はれたるを憂ひしが、主よ、萬事を知り給へり、我が汝を愛するは汝の知り給ふ所なり、と云ひしに、イエズス之に曰ひけるは、我羊を牧せよ。
Akamwambia tena mara ya tatu, “Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?” Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, “Je Wewe wanipenda?” Naye akamwambia, “Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.
18 誠に實に汝に告ぐ、汝若かりし時、自ら帯して好む處を歩み居たりしが、老いたらん後は手を伸べん、而して他の者汝に帯して、其好まざる處に導かん、と。
Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda.”
19 是ペトロが如何なる死を遂げて神に光榮あらしむべきかを示して曰ひしなり。然て之を曰ひ果てて、我に從へ、とペトロが曰ひしが、
Yesu alisema haya ili kuonesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro angemtukuza Mungu. Baada ya kuwa amesema haya, akamwambia Petro, “Nifuate.”
20 ペトロ回顧りてイエズスの愛し居給ひし彼弟子、即ち晩餐の時イエズスの御胸に横はりて、主よ汝を付す者は誰なるぞ、と云ひし弟子の從へるを見たり。
Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”
21 ペトロ之を見てイエズスに向ひ、主よ、彼は如何に、と云ひしに、
Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, “Bwana, Huyu mtu atafanya nini?”
22 イエズスペトロに曰ひけるは、我が來るまでに彼の留らん事を命ずとも、汝に於て何かあらん、汝は我に從へ、と。
Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, hilo linakuhusu nini?” Nifuate.”
23 然れば彼弟子死せずとの説兄弟等の中に傳はりしが、彼死せず、とイエズスのペトロに曰ひしには非ず、唯我が來るまで彼の留らん事を命ずとも、汝に於て何かあらん、と曰ひしのみ。
Kwa hiyo habari hii ikaenea miongoni mwa wale ndugu, kwamba mwanafunzi huyo hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia Petro kuwa, mwanafunzi huyo hafi, “Kama nataka yeye abaki mpaka nitakapokuja yakuhusu nini?”
24 此等の事に就きて證明し、此等の事を書きし人は、即ち彼弟子にして、我等は其證明の眞實なる事を知る。
Huyu ndiye mwanafunzi atoaye ushuhuda wa mambo haya, na ndiye aliye andika mambo haya, na tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.
25 然れどイエズスの為し給ひし事尚此他にも夥しく、若之を一々書記さば、我思ふに書記すべき書籍は、世界すらも載盡すこと能はざるべし。
Kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya. Kama kila moja lingeandikwa, nadhani kwamba ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.

< ヨハネの福音書 21 >