< ヨハネの福音書 10 >

1 第三款 善き牧者 誠に實に汝等に告ぐ、羊の檻に入るに、門よりせずして他の處より越ゆるは、盗人なり強盗なり、
Amin, Amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
2 門より入るは羊の牧者なり。
Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.
3 門番は彼に戸を開き、羊は其聲を聴き、彼亦己が羊を一々に名指して引出す、
Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje.
4 斯て其羊を出せば、彼先ちて往き羊之に從ふ、其聲を知ればなり、
Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake.
5 然れども他人には從はず、却て之を避く、他人の聲を知らざればなり、と。
Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni.”
6 イエズス此喩を彼等に曰ひしかど、彼等は其語り給ふ所の何たるを暁らざりき。
Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao.
7 然ればイエズス再び彼等に曰ひけるは、誠に實に汝等に告ぐ、我は羊の門なり、
Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.
8 已に來りし人は皆盗人、強盗にして、羊之に聴從はざりき。
Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza.
9 我は門なり、人若我に由りて入らば救はれ、出入して牧場を得べし。
Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.
10 盗人の來るは盗み、殺し、亡さんとするに外ならざれども、
Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.
11 我が來れるは羊が生命を得、而も尚豊に得ん為なり。我は善き牧者なり、善き牧者は其羊の為に生命を棄つ、
Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
12 然れども牧者に非ずして羊吾物に非ざる被雇人は、狼の來るを見れば羊を棄てて逃げ、狼は羊を奪ひ且追散す。
Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija na huwaacha na kuwakimbia kondoo.
13 被雇人の逃ぐるは、被雇人にして羊を勞らざる故なり。
Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo.
14 我は善き牧者にして我羊を知り、我羊亦我を知る、
Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi.
15 恰も父我を知り給ひ、我亦父を知り奉るが如し、斯て我は我羊の為に生命を棄つ。
Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
16 我は又此檻に属せざる他の羊を有てり、彼等をも引來らざるべからず、然て彼等我聲を聞き、斯て一の檻、一の牧者となるべし。
Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
17 父の我を愛し給へるは、之を再び取らんが為に我生命を棄つるに因る、
Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.
18 誰も之を我より奪ふ者はあらず、我こそ自ら之を棄つるなれ。我は之を棄つるの権を有し、又再び之を取るの権を有す、是我父より受けたる命なり、と。
Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba.”
19 是等の談の為に、ユデア人の中に復諍論起れり、
Mgawanyiko tena ukatokea kati ya wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
20 其中には、彼は惡魔に憑かれて狂へるなり、汝等何ぞ之に聴くや、と云ふ人多かりしが、
Wengi wao wakasema, “Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?”
21 他の人は、是惡魔に憑かれたる者の言に非ず、惡魔豈瞽者の目を明くことを得んや、と云ひ居たり。
Wengine wakasema, “Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?”
22 第四款 イエズス奉殿記念祭に上り給ふ 然てエルザレムに奉殿記念祭行はれて、時は冬なりしが、
Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.
23 イエズス[神]殿に在りてサロモンの廊を歩み居給ふに、
Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
24 ユデア人之を取圍みて、汝何時まで我等の心を疑惑せしむるぞ、汝若キリストならば、明白に我等に告げよ、と云ひければ、
Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
25 イエズス彼等に答へ給ひけるは、我汝等に語れども汝等信ぜざるなり、我が父の御名を以て行へる業、是ぞ我を證明するものなるに、
Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
26 汝等尚之を信ぜず、是我羊の數に入らざればなり。
Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
27 我羊は我聲を聴き、我彼等を知り、彼等我に從ふ、
Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi.
28 斯て我永遠の生命を彼等に與ふ、彼等長久に亡びず、誰も彼等を我手より奪はじ、 (aiōn g165, aiōnios g166)
Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu. (aiōn g165, aiōnios g166)
29 之を我に賜ひたる我父は、一切に優れて偉大に在し、誰も我父の御手より之を奪ひ得る者なし、
Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
30 我と父とは一なり、と。
Mimi na Baba tu mmoja.”
31 是に於てユデア人石を取りてイエズスに擲たんとせしかば、
Wakabeba mawe ili wamponde tena.
32 イエズス彼等に曰ひけるは、我わが父に由れる善業を多く汝等に示ししが、汝等其孰の為に我に石を擲たんとはするぞ。
Yesu akawajibu, “Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kuniponda mawe?”
33 ユデア人答へけるは、我等が汝に石を擲つは善業の為に非ず、冒涜の為、且汝が人にてありながら己を神とする故なり。
Wayahudi wakamjibu, “Hatukupondi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu.”
34 イエズス彼等に答へ給ひけるは、汝等の律法に録して「我言へらく、汝等は神なり」とあるに非ずや、
Yesu akawajibu, “Haikuandikwa katika sheria yenu, 'Nilisema, “Ninyi ni miungu”'?”
35 斯く神の言を告げられたる人々を神と呼びたるに、而も聖書は廃すべからず、我は神の子なりと言ひたればとて、
Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa),
36 汝等は、父の聖成して世に遣はし給ひし者に向ひて、汝は冒涜すと謂ふか、
mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, 'Unakufuru,' kwa sababu nilisema, 'mimi ni Mwana wa Mungu'?
37 我もし我父の業を為さずば我を信ずること勿れ、
“Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini.
38 然れど我もし之を為さば、敢て我を信ぜずとも業を信ぜよ、然らば父の我に在し我の父に居る事を暁りて信ずるに至らん、と。
Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba.”
39 是に於て彼等イエズスを捕へんと謀れるを、彼等の手を遁れて、
Wakajaribu tena kumkamata Yesu, lakini alienda zake kutoka mikononi mwao.
40 ヨルダン[河]の彼方、ヨハネが初に洗しつつありし處に至り、其處に留り給ひしに、
Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko.
41 多くの人御許に來りて、ヨハネは何の奇蹟をも行はざりしかど、
Watu wengi wakaja kwa Yesu. Waliendelea kusema, “Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli.”
42 此人に就きて告げし事は悉く眞なりき、と云ひつつイエズスを信仰せる者多かりき。
Watu wengi wakamwamini Yesu hapo.

< ヨハネの福音書 10 >