< ヘブル人への手紙 8 >

1 第二款 キリストは其司祭職の執行を以て舊約の司祭に優り給ふ 今言ふ所の要點は是なり、即ち我等の有する大司祭は天に於て至大[なる稜威]の玉座の右に坐し給ひ、
Sasa jambo ambalo tunasema ni hili: tunaye kuhani mkuu aliyekaa chini katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi Mbinguni.
2 聖所の役者にして、人の立てしにはあらで主の立て給ひし、眞の幕屋の役者にて在す。
Yeye ni mtumishi katika mahali patakatifu, hema la kweli ambalo Bwana ameliweka, siyo mtu yeyote wa kufa.
3 夫総て大司祭の立てらるるは、供物と犠牲とを献げん為なれば、彼も亦必ず献ぐべき何者かを有し給はざるべからず。
Kwa maana kila kuhani mkuu huwekwa kutoa zawadi na dhabihu; kwa hiyo ni muhimu kuwa na kitu cha kutoa.
4 若地上に居給はば司祭と成り給はざるべし、其は律法に從ひて供物を献ぐる人々既にあればなり。
Sasa kama Kristo alikuwa juu ya nchi, yeye asingekuwa kuhani zaidi ya hapo. Kwa kuwa walikuwa tayari wale waliotoa vipawa kulingana na sheria.
5 此人々は、在天の事物の模、及び影に奉事するのみ、恰もモイゼが幕屋を造らんとせし時に告げられしが如し、曰く、「看よ、何事も山に於て汝に示されし模型に從ひて之を為せ」と。
Walihudumu kitu ambacho kilikuwa nakala na kivuli cha vitu vya mbinguni, sawa kama Musa alipoonywa na Mungu wakati alipotaka kujenga hema. “Ona,” Mungu akasema, “kwamba tengeneza kila kitu kulingana na muundo ulioonyeshwa juu ya mlima”.
6 然れど我等の大司祭が現に尚善き聖役を得給ひしは、尚善き約束を以て保證せられたる、尚善き契約の仲介者たるに應じてなり。
Lakini sasa Kristo amepokea huduma bora zaidi kwa sababu yeye pia ni mpatanishi wa agano zuri, ambalo limekwisha kuimarishwa kwa ahadi nzuri.
7 蓋彼第一の契約に缺點なかりせば、第二のものを立つる餘地なかるべしと雖も、
Hivyo kama agano la kwanza lisingekuwa na makosa, ndipo hakungekuwa na haja kutafuta agano la pili.
8 [神]人々を咎めて曰ひけるは、「主曰く、看よ、日來らんとす、而して我イスラエルの家の上、又ユダの家の上に新約を全うすべし、
Kwa kuwa wakati Mungu alipogundua makosa kwa watu alisema, “Tazama, siku zinakuja, 'asema Bwana, 'wakati nitakapotengeneza agano jipya pamoja na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
9 是我が彼等の先祖をエジプトの地より救出さんとて其手を取りし時、之に為しし約の如きものに非ず、蓋彼等は我約に止らざりしかば、我も亦彼等を顧みざりき、と主曰へり。
Halitakuwa kama agano nililofanya pamoja na baba zao siku ambayo niliwachukua kwa mkono kuwaongoza kutoka nchi ya Misri. Kwa kuwa hawakuendelea katika agano langu, nami sikuwajali tena,' asema Bwana.
10 即ち主曰はく、彼日の後、イスラエルの家に我が立てんとする約は斯なり、我律法を其精神に置き、之を其心に書記さん、而して我は彼等に神と成り、彼等は我に民と成るべし。
Kwa kuwa hili ndilo agano nitafanya kwa nyumba ya Israeli baada ya siku hizo,' asema Bwana. 'nitaweka sheria zangu mawazoni mwao, na nitaziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
11 又各其近き者、其兄弟に教へて、主を知れと言ふ事あらじ、其は小き者より大いなる者に至るまで悉く我を知るべければなり。
Hawatafundishana kila mmoja na jirani yake, na kila mmoja na ndugu, yake, akisema, “Mjue Bwana,” hivyo wote watanijua mimi, kutoka mdogo hadi mkubwa wao.
12 蓋我彼等の不義を憫み、曾て其罪を記憶せざるべし」と。
Hivyo nitaonyesha rehema kwa matendo yao yasiyo ya haki, na sizitazikumbuka dhambi zao tena.”
13 然て新と曰へば、前のものを舊とし給ひしなり、舊にして老衰せるものは亡に近し。
Kwa kusema “Mpya,” amelifanya agano la kwanza kuwa kuukuu. Na hilo ambalo amelitangaza kuwa kuukuu liko tayari kutoweka.

< ヘブル人への手紙 8 >