< エペソ人への手紙 5 >

1 然れば汝等至愛なる小兒の如く神に倣う者となり、
Kwa hiyo muwe watu wa kumfuata Mungu, kama watoto wake wapendwao.
2 又愛の中に歩みて、キリストも我等を愛し、我等の為に己を馨しき香の献物とし、犠牲として神に捧げ給ひしが如くにせよ。
Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.
3 私通及び凡ての淫亂貪欲は、其名すらも汝等の中に稱へらるべからざること、聖徒たる者に相應しかるべし。
Zinaa au uchafu wowote na tamaa mbaya lazima visitajwe kati yenu, kama inavyotakiwa kwa waaminio,
4 或は汚行、愚なる談話、惡き戯言、是皆相應しからず、寧感謝すべきなり。
wala machukizo yasitajwe, mazungumzo ya kipumbavu, au mizaha ya udhalilishaji, ambayo siyo sawa, badala yake iwepo shukrani.
5 汝等覚りて知らざるべからず、凡ての私通者、淫亂者、貪欲者は、偶像を崇拝するに等しき者にして、キリスト及び神の國に於て世嗣たらざるなり。
Mnaweza kuwa na uhakika ya kwamba kuna zinaa, uchafu, wala atamaniye, huyo nimwabudu sanamu, hana urithi wowote katika ufalme wa Kristo na Mungu.
6 誰も空言を以て汝等を欺くべからず、其は是等の事の為に、神御怒は不信の子等の上に降ればなり。
Mtu yote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.
7 故に汝等彼等に與する事勿れ。
Hivyo usishiriki pamoja nao.
8 蓋汝等曾ては暗黒なりしかど、今は主に在りて光なり、光の子の如くに歩め。
Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru.
9 光の結ぶ果は、凡ての慈愛と正義と眞實とに在り。
Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.
10 如何なる事の神の御意に適ふかを試し看よ。
Tafuta kile kinacho furahisha kwa Bwana.
11 且果を結ばざる暗黒の業に與する事なく、寧却て之を咎めよ。
Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.
12 蓋彼等の窃に行ふ所は、之を口にするすら耻なり。
Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea.
13 凡ての咎むべき事は光によりて顕る、凡て顕るるは光なればなり。
Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi,
14 是故に言へる事あり、「眠れる人よ起て、死者の中より立上れ、キリスト汝を照らし給はん」と。
kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, “Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka wafu na Kristo atang'aa juu yako.”
15 然れば兄弟等よ、如何に慎みて歩むべきかに心せよ。愚者の如くにせず、
Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.
16 智者の如くに歩みて、日惡しければ良き機會を求めよ、
Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.
17 是故に神の御旨の如何を覚りて、思慮なき者と成る事勿れ。
Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana.
18 又酒に酔ふ事勿れ、其中に淫亂あるなり。寧ろ(聖)霊に満たされて、
Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.
19 霊的の詩と讃美歌と歌とを以て語合ひ、又心の中に謳ひて主を讃美し奉り、
Zungumzeni na kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na nyimbo za rohoni. Imbeni na sifuni kwa moyo kwa Bwana.
20 常に我主イエズス、キリストの御名を以て、萬事に就きて父にて在す神に感謝し、
Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.
21 キリストを畏れ奉りつつ互に歸服せよ。
Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo.
22 第三項 家庭に於る信者の義務 妻たる者は己が夫に從ふ事、主に於るが如くにすべし、
Wake, jitoeni kwa waume zenu, kama kwa Bwana.
23 其は夫が妻の頭たる事、キリストが教會の頭にして、自ら其體の救主に在せるが如くなればなり、
Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili.
24 然れば教會のキリストに從ふが如く、妻も亦萬事夫に從ふべし。
Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo.
25 夫たる者よ、汝等の妻を愛する事、キリストも教會を愛して、之が為に己を付し給ひしが如くにせよ、
Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake.
26 己を付し給ひしは、(生命の)言により、水洗にて之を潔めて聖とならしめん為、
Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno.
27 光榮ある教會、即ち染なく、皺なく、然る類の事もなき教會を、自ら己が為に備へて、之をして聖なるもの、汚なきものたらしめん為なり。
Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala waa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa.
28 斯の如く、夫たるものも亦己が妻を我身として愛すべきなり、妻を愛する人は是己を愛する者なり。
Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe.
29 蓋曾て如何なる人も、己が肉身を嫌ひし事なく、却て之を養ひ守る事、猶キリストが教會に為し給ひしが如し、
Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huurutubisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa.
30 其は我等は其御體の肢にして、其肉より其骨より成りたればなり。
Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake.
31 故に人は父母を措きて己が妻に添ひ、而して二人一體と成るべし、
“Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja”.
32 是大いなる奥義なり、我はキリスト及び教會に就きて之を言ふ。
huu ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa.
33 然れば汝等も各己が妻を己として愛し、又妻は夫を畏敬すべし。
Walakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.

< エペソ人への手紙 5 >