< エペソ人への手紙 4 >

1 第一項 教會一致の必要 然れば主に在りて囚人たる我、汝等に希ふ、汝等召されたる所の召に相應しく、
Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita.
2 凡ての謙遜と温良とを以て歩み、忍耐して愛を以て相忍び、
Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo.
3 平和の繋にて精神の一致を保つ様注意せよ。
Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
4 體は一、精神は一、猶汝等が召されたる其召の希望の一なるが如し。
Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu.
5 主は一、信仰は一、洗禮は一、
Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,
6 一同の上に在し一同を貫き、一同の中に住み給へる一同の神及び父は一のみ。
na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote.
7 然るに我等面々に賜はりたる恩寵は、キリストの賜ひたる量に應ず、
Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo.
8 此故に[聖霊に]曰く、「上に昇りて俘を伴ひ行き、人々に賜を與へ給へり」と。
Ni kama maandiko yasemavyo: “Alipopaa juu sana, aliongoza mateka katika utumwa. Akatoa vipawa kwa watu.”
9 抑昇り給ひしは、前に地の低き處まで降り給ひし故に非ずして何ぞや。
Ni nini maana ya, “Alipaa,” isipokuwa kwamba alishuka pia pande za chini za dunia?
10 降り給ひしものは、亦萬物に充満たんとて、諸の天の上に昇り給ひしものなり。
Yeye ambaye alishuka ni mtu yuleyule ambae pia alipaa mbali juu ya mbingu zote. Alifanya hivi ili uwepo wake uwe katika vitu vyote.
11 又或人々を使徒とし、或人々を預言者とし、或人々を福音者とし、或人々を牧師及び教師として與へ給へり。
Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu.
12 是聖徒等の全うせられ、聖役の営まれ、キリストの御體の成立たん為めなり。
Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo.
13 即ち我等が悉く、信仰と神の御子を識る知識との一致に至りて完全なる人となり、キリストの全き成長の量に至らん為にして、
Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.
14 我等は最早小兒たらず、漂はさるる事なく、人の僞と誤謬の巧なる誘惑との為に、敦の教の風にも吹廻されず、
Hii ni ili kwamba tusiwe tena kama watoto, tusirushwerushwe huku na huko. Ili kwamba tusichukuliwe na kila aina ya upepo wa fundisho, kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka.
15 眞理に在りて、愛により萬事に就て頭に在す者即ちキリストに於て成長せん為なり。
Badala yake, tutaongea ukweli katika upendo na kukua zaidi katika njia zote ndani yake ambaye ndiye kichwa, Kristo.
16 彼によりてこそ體全體に固り且整ひ、各四肢の分量に應ずる働に從ひて、凡ての関節の助を以て相聨り、自ら成長し、愛によりて成立つに至るなれ。
Kristo ameunganisha, kwa pamoja, mwili wote wa waumini. Umeungamanishwa pamoja na kila kiungo ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.
17 第二項 キリスト教の聖徳は異教人の惡徳に反す 故に我之を言ひ、且主に於て希ふ、汝等最早異邦人の如く歩むこと勿れ、彼等は己が精神の空しきに任せて歩み、
Kwa hiyo, nasema hili, na nawasihi katika Bwana: Msitembee tena kama watu wa mataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao.
18 智恵を暗まされ、身に有てる不知の為に、其心の頑固によりて神の生命より遠ざかり、
Wametiwa giza katika mawazo yao. Wamefukuzwa kutoka katika uzima wa Mungu kwa ujinga ulio ndani yao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.
19 感ずる事なく、放蕩に、所有る淫亂の業に、貪欲に、己を委ねたるなり。
Hawajisikii aibu. Wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu, katika kila aina ya uchoyo.
20 然れど汝等がキリストを學びしは斯の如き事に非ず、
Lakini, hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo.
21 若之に聴きて、眞理のイエズスに在るが儘に、彼に就きて學びしならば、
Nadhani kwamba mmesikia kuhusu yeye. Nadhani kwamba mmekuwa mkifundishwa katika yeye, kama tu ukweli ulivyo ndani ya Yesu.
22 即ち以前の行状に就きては、迷の望に從ひて腐敗する舊き人を脱棄て、
Lazima mvue mambo yote yanayoendana na mwenendo wenu wa zamani, utu wa zamani. Ni utu wa zamani unaooza kwa sababu ya tamaa za udanganyifu.
23 精神の主義を一新し、
Vueni utu wenu wa zamani ili kwamba mfanywe upya katika roho ya akili zenu.
24 神に象りて眞理より出づる義と聖徳とに於て造られたる新しき人を着る事を學びしなり。
Fanyeni hivi ili muweze kuvaa utu mpya, unaoendana na Mungu. Umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli.
25 然れば汝等僞を棄てて、各近き人と共に眞を語れ、我等は互の肢なればなり。
Kwa hiyo, weka mbali udanganyifu. “Ongeeni ukweli, kila mmoja na jirani yake,” kwa sababu tu washirika kwa kila mmoja kwa mwenzake.
26 汝等怒るとも罪を犯す事勿れ、汝等の怒の間に日没るべからず。
Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.
27 惡魔に機會を與ふる事勿れ、
Msimpe Ibilisi nafasi.
28 盗める人は最早盗むべからず、寧困窮せる人々に物を施す事を得ん為に、働きて善き手業を為せ。
Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji.
29 不潔なる談話は一切汝等の口より出すべからず、善きものならば聞く人々に恩寵を與へん為、要する人の徳を立つる様に之を為せ。
Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.
30 救の日を期して證印せられ奉りたる神の聖霊をして憂へしむる勿れ、
Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.
31 総て苦き事、怒、憤、叫、罵をば一切の惡心と共に汝等の中より取除け。
Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi.
32 然て互に慈悲親切にして相恕す事、神もキリストに於て汝等を赦し給ひしが如くにせよ。
Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

< エペソ人への手紙 4 >