< コロサイ人への手紙 3 >

1 第一項 信徒一般に関する教訓 然れば汝等、若キリストと共に復活したるならば、上の事、即ち神御右にキリストの坐し居給ふ處の事を求めよ。
Ikiwa tena Mungu amewafufua pamoja na Kristo, yatafuteni mambo ya juu ambako Kristo anakaa mkono wa kuume wa Mungu.
2 地上の事ならで、上の事を慮れ、
Fikirini kuhusu mambo ya juu, sio kuhusu mambo ya duniani.
3 蓋汝等は死したる者にして、其生命は、キリストと共に神に於て隠れたるなり。
Kwa kuwa mmekufa, na maisha yenu yamefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
4 我等の生命にて在すキリストの顕れ給ふ時には、汝等も亦彼と共に光榮の中に顕るべし。
Wakati Kristo atakapoonekana, ambaye ni maisha yenu, ndipo nanyi pia mtaonekana naye katika utukufu.
5 故に汝等、地上に於る四肢五體、即ち私通、淫亂、情慾、邪慾及び偶像崇拝なる貪欲を殺すべし、
Kwa hiyo yafisheni mambo yaliyo katika nchi yaani, zinaa, uchafu, shauku mbaya, nia mbaya, na tamaa, ambayo ni ibada ya sanamu.
6 神御怒は、是等の事の為に不信の子等の上に來る。
Ni kwa ajili ya mambo haya ghadhabu ya Mungu inakuja juu ya wana wasio tii.
7 汝等も彼等の中に生活せし時は、斯る事の中に歩みたれど、
Ni kwa ajili ya mambo haya ninyi pia mlitembea kwayo mlipoishi kati yao.
8 今は汝等も是等の一切と、怒、憤、惡心、罵罾とを棄て、猥褻なる談話を其口より棄てよ。
Lakini sasa ni lazima myaondoe mambo haya yote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu yatokayo vinywani mwenu.
9 互いに僞る勿れ。舊き人と其業とを脱ぎて、
Msidanganyane ninyi kwa ninyi, kwa kuwa mmeuvua utu wenu wa kale na matendo yake.
10 新しき人、即ち之を造り給ひしものの御像に肖りて知識に進む様、新になる人を着るべし。
Mmevaa utu mpya, ambao unafanywa upya katika maarifa kutokana mfano wa yule aliye muumba.
11 茲に至りては、異邦人もユデア人も、割禮も無割禮も、夷もシタ人も、奴隷も自由の身もある事なく、唯萬民の中に萬事と成り給へるキリストの在せるのみ。
Katika maarifa haya, hakuna Myunani na Myahudi, kutahiriwa na kutokutahiriwa, msomi, asiye msomi, mtumwa, asiye mtumwa, lakini badala yake Kristo ni mambo yote katika yote.
12 然れば汝等、神に選まれ奉りたる聖にして且至愛なる者の如く、慈悲の腸、寛仁、謙遜、柔和、堪忍等を身に纏ひて、
Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
13 互に忍耐し、若人に對して苦情あらば互に宥恕し、主の汝等に赦し給ひし如く、汝等も亦然せよ。
Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ilele ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi.
14 尚此一切の事に加へて愛を有せよ、愛は完徳の結なればなり。
Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu.
15 而して汝等一體としてキリストの平和に召されたれば、其平和をして汝等の心を司らしむべし、汝等も亦感謝し奉れ。
Amani ya Kristo na iwaongoze mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii kwamba mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani.
16 キリストの御言汝等の中に豊に宿りて、凡ての知識に於て相教へ相勧め、恩寵によりて霊的の詩、讃美歌、歌を以て、心の中に神に謳ふべし。
Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa utajiri. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi, nyimbo, na nyimbo za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyo yenu kwa Mungu.
17 何事を為すも、或は言、或は行、悉く主イエズス、キリストの御名により、之を以て父にて在す神に感謝し奉りつつ為すべし。
Na chochote mfanyacho, katika maneno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye.
18 第二項 家庭に関する教訓 妻たる者よ、為すべき如く主に於て夫に從へ。
Wake, wanyenyekeeni waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.
19 夫たる者よ、其妻を愛して彼等に苦かること勿れ。
Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali dhidi yao.
20 子たる者よ、萬事に於て親に從へ、是主の御意に適ふが故なり。
Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana.
21 父たる者よ、汝等其子等の怒を買ふ事勿れ、恐らくは落胆せん。
Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.
22 奴隷たる者よ、萬事に於て肉身上の主人に從へ、人に喜ばれんとするが如くに、目前のみにて事へず、純朴なる心を以て主を畏れて事へよ。
Watumwa, watiini mabwana zenu katika mwili kwa mambo yote, sio kwa huduma ya macho kama watu wa kufurahisha tu, bali kwa moyo wa kweli. Mwogopeni Mungu.
23 汝等何事を為すも、人の為にすと思はず、主の為にすと思ひ、
Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu.
24 主より世嗣の報を得べしと覚りて之を心より行へ。主キリストに事へ奉れ、
Mnajua ya kwamba mtapokea tuzo ya umilkaji kutoka kwa Bwana. Ni Kristo Bwana mnayemtumikia.
25 蓋不義を為す人は其不義の報を得べし、且神に於ては人に偏り給ふ事あらざるなり。
Kwa sababu yeyote atendaye yasiyo haki atapokea hukumu kwa matendo yasiyo haki aliyoyafanya, na hakuna upendeleo.

< コロサイ人への手紙 3 >