< 使徒の働き 4 >

1 第三 ペトロ及びヨハネ衆議所に於てキリストを證す ペトロヨハネと人民に語りつつ居りしに、
Wakati Petro na Yohana walipokuwa wakizungumza na watu, makuhani na mlinzi wa hekalu na masadukayo waliwaendea.
2 司祭等と神殿の司とサドカイの人々と來り、彼等が人民を教へ、且イエズスに於る死者の復活を説くことを深く憂ひて、
Walikuwa wameudhika sana kwa sababu Petro na Yohana walikuwa wanawafundisha watu kuhusu Yesu na kutangaza juu ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.
3 彼等を捕へ、日既に暮れければ、翌日まで拘留したり。
Waliwakamata na kuwaweka gerezani hadi asubuhi iliyofuata, kwani tayari ilikuwa jioni.
4 然れど言を聴きたりし人々、多くは信仰して、男子の數五千人に及べり。
Lakini watu wengi waliokuwa wamesikia ujumbe waliamini; na idadi ya wanaume waliokuwa wameamini walikadiliwa kuwa elfu tano.
5 明日司祭長、長老、及び律法學士等、エルザレムに集會する事となりしが、
Hata ilipofika asubuhi siku iliyofuata, kwamba wakuu wao, wazee na waandishi, kwa pamoja walikusanyika Yerusalemu.
6 アンナ大司祭もカイファも、ヨハネもアレキサンデルも、又大司祭の族も悉く共に在りき。
Anasi kuhani mkuu alikuwepo, na Kayafa, na Yohana, na Iskanda, na wote waliokuwa ni ndugu wa kuhani mkuu.
7 斯てペトロとヨハネとを眞中に立たせて、汝等如何なる力如何なる名によりて此事を行ひしぞ、と問ひかけたり。
Walipokuwa wamewaweka Petro na Yohana katikati yao, waliwauliza, “Kwa uwezo gani, au kwa jina gani mmefanya hili?”
8 其時ペトロ聖霊に満たされて彼等に云ひけるは、聞けや民の司等、長老等、
Kisha, Petro, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akawaambia, “Ninyi wakuu wa watu, na wazee,
9 我等が癈疾者に對する善業に就き、其何に由りて醫されしかを尋問せらるるなれば、
kama sisi siku ya leo tunahojiwa kuhusu tendo jema lililofanywa kwa mtu huyu mgonjwa - kwa namna gani mtu huyu alifanywa mzima?
10 汝等一同及びイスラエルの人民挙りて之を知れ、彼人が壮健にして汝等の前に立てるは、是我等の主ナザレトのイエズス、キリスト、即ち汝等が之を殺し、神が之を死者の中より復活せしめ給ひし者の御名に由るなり。
Hebu lijulikane hilo kwenu na kwa watu wote katika Israel, kwamba kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye mlimsulibisha, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, ni kwa njia yake kwamba mtu huyu anasimama hapa mbele yenu akiwa mwenye afya.
11 是ぞ汝等家を建つる者に蔑にせられたる石にして、角の親石とせられたる者なる。
Yesu Kristo ni jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilidharau, lakini ambalo limefanywa kuwa jiwe kuu la pembeni.
12 其他の者によりては救霊ある事なし、其は我等が依て救かるべきものとして人に與へられし名は、天下に復之あらざればなり、と。
Hakuna wokovu katika mtu mwingine awaye yote. Kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa watu, ambalo kwa hilo tunaweza kuokolewa.”
13 會衆は彼等が無學の凡人なる事を豫て弁へたれば、ペトロ及びヨハネの泰然たるを見て之を怪しみ、また豫て彼等がイエズスに伴ひたりし事をも知り、
Sasa walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na wakagundua kwamba walikuwa ni watu wakawaida wasio na elimu, walishangaa, wakafahamu kwamba Petro na Yohana wamekuwa pamoja na Yesu.
14 醫されし人の現に彼等と共に立てるを見て、一言も之に對して云ふこと能はず、
Kwa sababu walimwona yule mtu aliyeponywa amesimama pamoja nao, hawakuwa na kitu cha kusema dhidi ya hili.
15 命じて彼等を衆議所より退け、共に評議して、
Lakini walipokuwa wamekwisha kuwaamuru mitume waondoke mbele ya mkutano wa baraza, walizungumza wao kwa wao.
16 云ひけるは、彼人々を如何に處分すべきぞ、蓋エルザレムの人民一同に知れ渡りたる奇蹟は彼等によりて行はれ、明白にして我等之を拒むこと能はず、
Walisema, tutawafanyaje watu hawa? Ni kweli kwamba muujiza wa ajabu umefanyika kupitia wao unajulikana na kila mmoja anayeishi Yerusalemu; hatuwezi kulikataa hilo.
17 然れど、其一層民間に弘まらざらん為に、彼等を脅かして、如何なる人にも再び彼名を以て語る事なからしむべし、とて、
Lakini, ili kwamba jambo hili lisienee miongoni mwa watu, hebu tuwaonye wasinene tena kwa mtu yeyote kwa jina hili.
18 彼等を呼び、一切イエズスの名を以て語り且教ふる事勿れ、と戒めたり。
Waliwaita Petro na Yohana ndani na kuwaamuru kamwe wasinene wala kufundisha kwa jina la Yesu.
19 然れどもペトロ、ヨハネは答へて、汝等に聴くは神に聴くよりも神の御前に正當なりや、汝等之を判ぜよ、
Lakini Petro na Yohana walijibu na kuwaambia, “Kama ni sahihi machoni pa Mungu kuwatii ninyi kuliko Mungu, hukumuni wenyewe.
20 蓋我等は見聞せし事を語らざるを得ず、と云へり。
Maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo ambayo tumeyaona na kuyasikia.”
21 然て彼行はれし事に就きて人皆神を崇め奉るに由り、彼等は人民に對して使徒等を罰するに便なく、脅かして之を還せり。
Baada ya kuwaonya sana Petro na Yohana, waliwaacha waende. Hawakuweza kupata sababu yoyote ya kuwaadhibu, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetendeka.
22 蓋彼全癒の奇蹟の行はれし人は四十歳以上なりき。
Mtu aliyekuwa amepokea muujiza wa uponyaji alipata kuwa na umri zaidi ya miaka arobaini.
23 二人は赦されて友の許に至り、司祭長、長老等の云ひし程の事を具に告げしかば、
Baada ya kuwaacha huru, Petro na Yohana walikuja kwa watu wao na kuwataarifu yote ambayo makuhani wakuu na wazee walikuwa wamewaambia.
24 彼等は之を聞きて神に向ひ、異口同音に聲を揚げて云ひけるは、主よ、天、地、海、及び其中の有らゆる物を造り給ひしは主なり。
Walipoyasikia, walipaza sauti zao kwa pamoja kwa Mungu na kusema, “Bwana, wewe uliyeumba mbingu na dunia na bahari na kila kitu ndani yake,
25 主は聖霊に由りて、主の僕にして我等の先祖なるダヴィドの口を以て、「何故に異邦人は振起り、人民等は徒事を謀りしぞ、
wewe ambaye, kwa Roho Mtakatifu, kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ulisema, “Kwanini watu wa mataifa wamefanya ghasia, na watu wametafakari mambo yasiyofaa?
26 地上の國王は立ち、諸侯は一致して主及び其キリストに逆らへり」、と曰ひしが、
Wafalme wa dunia wamejipanga pamoja, na watawala wamekusanyika kwa pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya masihi wake.”
27 果してヘロデ及びポンシオ、ピラトは、異邦人、イスラエルの諸族と共に此都に集りて、主の注油し給ひし聖なる御子イエズスに逆らひ、
Ni hakika, wote Herode na Pontio Pilato, pamoja na watu wa mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika kwa pamoja katika mji huu dhidi ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, ambaye ulimpaka mafuta.
28 御手及び御旨の定め給ひし事を為せり。
Walikusanyika kwa pamoja kufanya yote ambayo mkono wako na mapenzi yako yaliyaamuru tangu awali kabla hayajatokea.
29 主よ、今や彼等の脅喝を顧み、僕等に賜ふに、御言を憚らず語ることを以てし給ひ、
Sasa, Bwana, yaangalie matisho yao, na ukawajaalie watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri wote. Ili
30 御手を伸ばして、聖なる御子イエズスの御名によりて、治癒と徴と不思議とを行はせ給へ、と。
kwamba unaponyosha mkono wako kuponya, ishara na maajabu viweze kutokea kupitia jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.”
31 祈り畢れる時、彼等の集れる所震動し、皆聖霊に満たされて、憚る所なく神の御言を語り居たり。
Walipomaliza kuomba, eneo ambalo walikusanyika kwa pamoja likatikiswa, na wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, na walinena neno la Mungu kwa ujasili.
32 第一 初代信者の徳 第四款 神聖會を保護し給ふ 抑信者の群衆は、同心同意、一人も其有てる物を己が物と謂はず、何物をも皆共有にし、
Idadi kubwa ya wale walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja: na hakuna hata mmoja wao aliyesema kwamba chochote alichomiliki kilikuwa cha kwake mwenyewe; badala yake walikuwa na vitu vyote shirika.
33 使徒等も亦大いなる力を以て、我主イエズス、キリストの復活を證し、大いなる恩寵彼等一同の上に在りき。
Kwa nguvu kubwa mitume walikuwa wakiutangaza ushuhuda wao kuhusu ufufuo wa Bwana Yesu, na neema kubwa ilikuwa juu yao wote.
34 蓋彼等の中には一人も乏しき者あらず、其は総て、畑又は家を有てる人は之を売りて、其売れる物の價を持來り、
Hapakuwa na mtu yeyote miongoni mwao aliyepungukiwa na mahitaji, kwa sababu watu wote waliokuwa na hati za viwanja au nyumba, waliviuza na kuleta pesa ya vitu waliyokuwa wameuza
35 之を使徒等の足下に置きて、面々其用あるに随ひて分與へらるればなり。
na kuviweka chini ya miguu ya mitume. Na mgawanyo ulifanywa kwa kila muumini, kulingana na kila mmoja alivyokuwa na hitaji.
36 爰にクプロ[島]生れなるレヴィ族の人ヨゼフは、使徒等よりバルナバ、訳して慰の子、と呼ばれたるが、
Yusufu, mlawi, mtu kutoka Kipro, alipewa jina la Barnabasi na mitume (hiyo ikitafasiriwa, ni mwana wa faraja).
37 畑の有りしを売りて其價を持來り、之を使徒の足下に置けり。
Akiwa na shamba, aliliuza na akaleta fedha, akaziweka chini ya miguu ya mitume.

< 使徒の働き 4 >