< 使徒の働き 25 >

1 第八項 パウロ、フェストの法廷に出頭す フェスト赴任して三日の後、カイザリアよりエルザレムに上りければ、
Ndipo Festo alipoingia katika jimbo hilo na baada ya siku tatu alienda toka Kaisaria hadi Yerusalemu.
2 司祭長等及びユデア人の重立ちたる者、パウロを訴へんとて其許に至り、
Kuhani mkuu na Wayahudi mashuhuri walileta shutuma dhidi ya Paulo kwa Festo, na walizungumza kwa nguvu kwa Festo.
3 御恵には命じてパウロをエルザレムに連行かしめ給へ、と願へり。是途中に待伏して、彼を殺さんとすればなり。
Na walimwomba Festo fadhili juu ya habari za Paulo apate kumwita Yerusalemu ili waweze kumwua njiani.
4 フェスト答へて、パウロは守られてカイザリアに在り、我程なく出立すべければ、
Lakini Festo alijibu kwamba Paulo alikuwa mfungwa katika Kaisaria, na kwamba yeye mwenyewe atarudi huko haraka.
5 若彼人に罪あらば、汝等の中の然るべき人々、我と共に下りて之を訴ふべし、と言へり。
Alisema “Kwa hiyo, wale ambao wanaweza, wanaweza kwenda huko na sisi. Kama kuna kitu kibaya kwa mtu huyu, mnapaswa kumshtaki.”
6 斯てフェストは、八日か十日ばかり彼等の中に滞在してカイザリアに下り、翌日法廷に坐し、命じてパウロを引出させしが、
Baada ya kukaa siku nane au kumi zaidi, akarudi Kaisaria. Na siku iliyofuata akakaa katika kiti cha hukumu na kuamuru Paulo aletwe kwake.
7 パウロ召出されければ、エルザレムより下りたるユデア人等之を取圍みて、種々の重罪を負はせたれど、之を證する事能はざりき。
Alipofika, Wayahudi kutoka Yerusalemu wakasimama karibu, Wakatoa mashtaka mengi mazito ambayo hawakuweza kuyathibitisha.
8 パウロは自ら弁解して、我ユデア人の律法に對しても、神殿に對しても、セザルに對しても、何らの罪を犯したる事なし、と言へり。
Paulo alijitetea na kusema, 'Si dhidi ya jina la Wayahudi, si juu ya hekalu, na si juu ya Kaisari, nimefanya mabaya.'
9 フェストユデア人を喜ばせんとて、パウロに答へて、汝エルザレムに上り、彼處にて我前に裁判を受けん事を欲するか、と云ひしかば、
Lakini Festo alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, na hivyo akamjibu Paulo kwa kusema, 'Je, unataka kwenda Yerusalemu na kuhukumiwa na mimi kuhusu mambo haya huko?'
10 パウロ云ひけるは、我はセザルの法廷に立てり、此處にて裁判せらるべし。汝の能く知れるが如く、我はユデア人に害を加へたる事なし、
Paulo alisema, 'ninasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari ambapo napaswa kuhukumiwa. Sijawakosea Wayahudi, kama wewe ujuavyo vema.
11 若害を加へたるか、或は死刑に當る何事をか為したらんには、我死を辞せず、然れど彼等が我に負はする事一も立たずば、誰も我を彼等に交付し得べからず、我セザルに上告す、と。
Ikiwa nimekosa na kama nimefanya kinachostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama shutuma zao si kitu, hakuna mtu anaweza kunikabidhi kwao. Ninamwomba Kaisari. '
12 是に於てフェスト、陪席と談じて後答へけるは、汝セザルに上告したればセザルの許に往くべし、と。
Baada ya Festo kuongea na baraza akajibu, “unamwomba Kaisari; utaenda kwa Kaisari.”
13 數日を経てアグリッパ王及びベルニケは、フェストの安否を問はんとてカイザリアに下り、
Baada ya siku kadhaa, mfalme Agripa na Bernike walifika Kaisaria kufanya ziara rasmi kwa Festo.
14 數日間滞在しければ、フェストパウロの事を王に告げて云ひけるは、茲にフェリクスより遺し置かれたる一人の囚人あり、
Baada ya kukaa hapo kwa siku nyingi, Festo aliwasilisha kesi ya Paulo kwa mfalme; Akasema, 'Mtu mmoja aliachwa hapa na Feliki kama mfungwa.
15 我エルザレムに居りし時、司祭長、ユデア人の長老等、我許に來りて、之が宣告を願ひしかど、
Nilipokuwa Yerusalemu makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka juu ya mtu huyu kwangu, nao waliuliza juu ya hukumu dhidi yake.
16 我、何人にもあれ、被告人が原告人と對面して罪を弁解する機を得ざる中に、之を刑罰するは、ロマ人の慣例に非ず、と答へたり。
Kwa hili mimi niliwajibu kwamba si desturi ya Waroma kumtoa mtu kwa upendeleo badala yake, mtuhumiwa anapaswa kuwa na nafasi ya kuwakabili washitaki wake na kujitetea dhidi ya tuhuma hizo.
17 是に由て彼等、時を移さず此處に集來りたれば。翌日我法廷に坐し、命じて彼人を引出さしめ、
Kwa hiyo, walipokuja pamoja hapa, sikuweza kusubiri, lakini siku iliyofuata niliketi katika kiti cha hukumu na kuamuru mtu huyo aletwe ndani.
18 原告人等之に立會ひしに、我が嫌疑を懸けたる如き罪をば一點も負はせず、
Wakati washitaki waliposimama na kumshtaki, nilifikiri kwamba hakuna mashtaka makubwa yaliyoletwa dhidi yake.
19 己が宗教及び活き居れりとパウロが断言せる一人の死者イエズスに関する問題を提出したるのみ、
Badala yake, walikuwa na mabishano fulani pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu Yesu ambaye alikuwa amekufa, lakini Paulo anadai kuwa yu hai.
20 我斯る問題には當惑したれば彼人に向ひて、汝エルザレムに至り、是に就きて裁判を受くる事を望むか、と云ひしに、
Nilikuwa nimefumbwa jinsi ya kuchunguza suala hili, na nikamwuliza kama angeenda Yerusalemu kuhukumiwa kuhusu mambo haya.
21 パウロはオグストの裁判に保留せらるる様上告せしかば、我命じて、セザルの許に送るまで守らせ置けり、と。
Lakini Paulo alipoitwa awekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uamuzi wa Mfalme, niliamuru awekwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari. '
22 アグリッパ、我も彼人に聞きたし、とフェストに謂ひしかば、汝明日之に聞くべし、と云へり。
Agripa alizungumza na Festo, “ningependa pia kumsikiliza mtu huyu.” “Festo, akasema, “kesho utamsikiliza.”
23 翌日アグリッパとベルニケと華美を盡して來り、千夫長及び市の重立ちたる人々と共に公判廷に入りしかば、フェストの命令の下にパウロ引出されたり。
Hivyo kesho yake, Agripa na Bernike walifika na sherehe nyingi; walifika katika ukumbi na maafisa wa kijeshi, na watu mashuhuri wa mji. Na Festo alipotoa amri, Paulo aliletwa kwao.
24 斯てフェスト云ひけるは、アグリッパ王及び此處に我等と列席せる人等よ、汝等の見る此人は、ユデア人の群衆挙りて我に訴へ、最早活くべき者に非ず、と叫びつつ願ひし者なり。
Festo akasema, “Mfalme Agripa, na watu wote ambao wapo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu; jumuiya yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wametaka niwashauri, na wao wakapiga kelele kwangu kwamba asiishi.
25 然して我は死に値する何等の罪なき事を彼に認めたれど、彼オグストに上告せしにより、之を送付すべしと決せり。
Naliona kwamba hakufanya lolote linalostahili kifo; lakini kwa sababu amemwita Mfalme, niliamua kumpeleka kwake.
26 我君に上書せんとするに確乎なる事實なきを以て、之を汝等の前、殊にアグリッパ王よ、御前に引出し、尋問して上書すべき事柄を得んとす、
Lakini sina kitu dhahiri cha kuandika kwa Mfalme. Kwa sababu hii, nimemleta kwako, hasa kwako wewe, Mfalme Agripa, ili nipate kuwa na kitu cha kuandika kuhusu kesi.
27 其は囚人を送りて其罪案を書添へざる事の無理なるを惟へばなり、と。
kwa kuwa naona haina maana kumpeleka mfungwa na bila kuonyesha mashitaka yanayomkabili.

< 使徒の働き 25 >