< 使徒の働き 2 >

1 第一 聖霊降臨 ペンテコステの日至りしかば、皆一所に集り居けるに、
Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja sehemu moja.
2 忽ちにして天より烈しき風の來るが如き響ありて、彼等が坐せる家に充ち渡り、
Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
3 又火の如き舌彼等に顕れ、分れて各の上に止れり。
Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao.
4 斯て皆聖霊に満たされ、聖霊が彼等に言はしめ給ふに從ひて、種々の言語にて語り出でたり。
Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema.
5 然るに敬虔なるユデア人等の、天下の諸國より來りてエルザレムに住める者ありしが、
Sasa walikuwapo wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu.
6 此音の響き渡るや、群集集り來りて、何れも使徒等が面々の國語にて語るを聞きければ、一同心騒ぎ惘果て、
Ngurumo hizi ziliposikiwa, kundi la watu likaja pamoja na wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe.
7 驚き嘆じて云ひけるは、看よ彼語る人は皆ガリレア人ならずや、
waliduwaa na kushangazwa, wao walisema, “Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya?
8 如何にして我等各、我生國の語を聞きたるぞ、と。
Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo?
9 パルト人、メド人、エラミト人、又メソポタミア、ユデア、カパドキア、ポント、[小]アジア、
Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia,
10 フリジア、パムフィリア、エジプト、クレネに近きリビア地方に住める者、及びロマ寄留人、即ち、
katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi,
11 ユデア人もユデア教に歸依せし人も、クレタ人も、アラビア人も、彼等が我國語にて神の大業を語るを聞きたるなり。
Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu.”
12 然れば皆驚き嘆じて、是は何事ぞと語合ひけるが、
Wote walikuwa wameduwaa na kutatanishwa; walisemezana wao kwa wao, “Hii ina maana gani?”
13 或は嘲笑ひて、彼等は酒に酔へり、と謂ふ人々もありき。
Lakini wengine walidhihaki wakisema, “Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya.”
14 第二 ペトロの説教 是に於てペトロ十一人と共に立上り、聲を揚げて人々に語りけるは、ユデア人及び総てエルザレムに住める人々よ、汝等之を知らざるべからず、耳を傾けて我言を聞け。
Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti, akawaambia, “Watu wa Yudea na wote mnaoishi hapa Yerusalemu, hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.
15 時は尚朝の第九時なれば、此人々は汝等の思へる如く酔ひたるに非ず、
Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu.
16 是預言者ヨエルを以て言はれし事なり、曰く「主曰はく、末の日頃に至らば、我霊を凡ての人の上に注がん、
Lakini hili lilikuwa limesemwa kupitia kwa nabii Yoeli:
17 斯て汝等の子女は預言し、汝等の青年等は幻を見、汝等の老人等は夢みるべし、
Itakuwa katika siku za mwisho; Mungu asema, nitamwaga Roho wangu kwa watu wote. Wana wenu na binti zenu watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
18 又我僕、婢等の上にも、彼日頃に至りて我霊を注がん、斯て彼等は預言すべし。
Vilevile juu ya watumishi wangu na watumishi wangu wa kike katika siku hizo, nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.
19 我又上は天に不思議を、下は地に徴を與へん、即ち血と火と烟の柱とあるべし、
Nitaonesha maajabu juu angani na ishara chini duniani, damu, moto, na mafusho ya moshi.
20 主の大いにして明白なる日の來らざる前に、日は暗黒と成り、月は血と成らん、
Na jua litabadilishwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja siku kuu na ya ajabu ya Bwana.
21 斯て主の御名を呼頼まん人皆救はるべし」と。
itakuwa ya kwamba kila mmoja ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.'
22 イスラエル人よ、是等の言を聞け。ナザレトのイエズスは、汝等も知れる如く、神が之を以て汝等の中に行ひ給ひし奇蹟と不思議と徴とを以て、神より汝等の中に證明せられたる人にして、
Watu wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mwanadamu aliyethibitishwa na Mungu kwenu kwa matendo ya uweza na maajabu, na ishara ambazo Mungu kupitia Yeye katikati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua-
23 神の豫定の思召と豫知とによりて付されしを、汝等不法人の手を以て之を磔にして殺したるなり。
Kwa sababu ya mpango uliokusudiwa tangu mwanzo, na maarifa ya Mungu, alitolewa, na ninyi, kwa mikono ya watu wahalifu, mlimsulibisha na kumuua,
24 彼冥府に止めらるること能はざりければ、神冥府の苦を解きて之を復活せしめ給へり。
ambaye Mungu alimwinua, akauondoa uchungu wa mauti kwake, kwasababu haikuwezekana kwake kumilikiwa na huo.
25 蓋ダヴィド之を斥して曰く、「我は絶えず我前に主を見奉りたり、其は我が動かざらん為に、主我右に在せばなり。
Hivyo Daudi anasema kuhusu yeye, 'Nilimwona Bwana daima mbele ya uso wangu, yeye yuko mkono wangu wa kulia hivyo basi sitasogezwa.
26 故に我心は嬉しく、我舌は喜びに堪へず、加之我肉體も亦希望の中に息まん。
Kwa hiyo moyo wangu ulikuwa na furaha na ulimi wangu ulifurahishwa. Pia mwili wangu utaishi katika ujasiri.
27 其は汝我魂を冥府に棄置き給はず、汝の聖なる者に腐敗を見せ給ふ事なかるべければなり、 (Hadēs g86)
Hutaiacha nafsi yangu iende kuzimu, wala hutaruhusu Mtakatifu wako kuona uozo. (Hadēs g86)
28 汝生命の道を我に知らせ給へり、又御顔を以て我を喜に満たせ給ふべし」と。
Wewe umedhihirisha kwangu njia za uzima; utanifanya nijae furaha mbele ya uso wako.'
29 兄弟の人々よ、大祖ダヴィドに就きて憚らず之を云はしめよ。彼は死して葬られ、其墓は今日に至るまで我等の中に存す。
Ndugu, ninaweza kuzungumza kwenu kwa ujasiri kuhusu baba yetu Daudi: yeye alikufa na akazikwa, na kaburi lake liko pamoja nasi hata hivi leo.
30 即ち彼は預言者にして、神之に誓を立て、其子孫の中より一人其座に着くべし、と約し給ひし事を知り居たれば、
Hivyo, alikuwa nabii na alijua kuwa Mungu alishaapa kwa kiapo kwake, kwamba ataweka mmoja katika uzao wake kwenye kiti cha enzi.
31 先見してキリストの復活を示し、其冥府に棄置かれざりし事と、其肉體の腐敗を見ざりし事とを語りたるなり。 (Hadēs g86)
Aliliona hili mapema, na akasema kuhusu ufufuo wa Kristo, 'wala alikuwa hakuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuoza.' (Hadēs g86)
32 神は此イエズスを復活せしめ給へり、我等は皆其證人なり。
Huyu Yesu - Mungu alimfufua, ambaye sisi wote ni mashahidi.
33 然ればこそ神の右の御手を以て上げられ、且父より聖霊の約束を受けて、汝等の見且聞ける此聖霊を注ぎ給ひたるなれ。
Kwa hiyo, akiwa ameinuliwa katika mkono wa kuume wa Mungu, na akiwa amepokea ahadi ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Baba, yeye amemimina hii ahadi, ambaye ninyi mnaona na kusikia.
34 蓋ダヴィドは天に昇りしに非ざれども、自ら曰へらく「主我主に曰へらく、
Kwani Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini anasema, 'BWANA alisema kwa Bwana wangu,
35 我汝の敵を汝の足台とならしむるまで我右に坐せ」と。
“keti mkono wangu wa kulia, mpaka nitakapowafanya adui zako kigoda kwa ajili ya miguu yako.
36 然れば汝等が十字架に磔けし此イエズスをば、神が主となしキリストと為し給ひし事を、イスラエルの家挙りて最も確に知らざるべからず、と。
Kwa hiyo nyumba yote ya Israeli na ijue kwa hakika kwamba Mungu amemfanya Yeye kuwa Bwana na Kristo, huyu Yesu ambaye mlimsulibisha.”
37 第三 其説教の結果 人々是等の事を聞きて心を刺され、ペトロ及び他の使徒等に向ひ、兄弟の人々よ、我等何を為すべきぞ、と云ひければ、
Sasa waliposikia hivyo, wakachomwa katika mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, “Ndugu, tufanyeje?”
38 ペトロ云ひけるは、汝等改心せよ、且罪を赦されん為に、各イエズス、キリストの御名によりて洗せらるべし、然らば聖霊の賜を得ん。
Na Petro akawaambia, “Tubuni na Mbatizwe, kila mmoja wenu, katika jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zenu, na mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu.
39 蓋約束は汝等の為にして、又汝等の子等、及び総て遥に遠ざかれる人、我等の神たる主の召し給へる一切の人の為なり、と。
Kwani kwenu ni ahadi na kwa watoto wenu na kwa wale wote walioko mbali, watu wengi kwa kadri Bwana Mungu wetu atakavyowaita.”
40 ペトロ此他尚多くの言を以て、人々を服せしめ且勧めて、汝等此邪の時代より救ひ出されよ、と云ひ居たり。
Kwa maneno mengi alishuhudia na kuwasihi; alisema, “Jiokoeni mtoke katika kizazi hiki kiovu.”
41 斯て彼の言を承けし人々洗せられしが、即日弟子の數に加はりし者約三千人なりき。
Ndipo wakayapokea maneno yake na wakabatizwa, hapo wakaongezeka katika siku hiyo kama nafsi elfu tatu.
42 然て堪忍びて、使徒等の教と共同生活と、麪を擘く事と祈祷とに從事し居たりしが、
Wakaendelea katika mafundisho ya mitume na ushirikiano, katika kuumega mkate na katika maombi.
43 軈て人皆心に懼を生じ、又使徒等に籍りて、多くの不思議と徴と、エルザレムに行はれければ、一般の人々大いに懼れを懐き居たり。
Hofu ikaja juu ya kila nafsi, na maajabu mengi na ishara zikafanyika kupitia mitume.
44 斯て信仰せる人々、総て一所に在りて何物をも共有にし、
Wote walioamini walikuwa pamoja na kuwa na vitu vyao kwa pamoja,
45 動産不動産を売り、面々の用に應じて一同に分ちつつ、
na waliuza vitu na milki zao na kugawanya kwa wote kulingana na hitaji la kila mmoja.
46 尚毎日心を同じくして長時間[神]殿に居り、家々に麪を擘きて喜悦と眞心とを以て食事を為し、
Hivyo siku baada ya siku waliendelea wakiwa na lengo moja katika hekalu, na walimega mkate kwenye kaya, na walishiriki chakula kwa furaha na unyenyekevu wa moyo;
47 諸共に神を賛美し奉りて、人民一般の心を獲たり。然て斯の如くに、救はるる人を、主日々増加せしめ給ひつつありき。
walimsifu Mungu na wakiwa na kibali na watu wote. Bwana aliwaongeza siku kwa siku ambao walikuwa wakiokolewa.

< 使徒の働き 2 >