< テモテへの手紙第一 5 >

1 第二項 種々の人に對する法 老人を譴責せず、父の如くにして希へ、若き人を兄弟の如く、
Usimkemee mwanamume mzee. Bali mtiye moyo kama baba yako. Uwatiye moyo vijana wa kiume kana kwamba ni ndugu zako.
2 老いたる女を母の如く、若き女を姉妹の如くにして完全に節操を守りつつ勧めよ。
Uwatiye moyo wanawake wazee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako kwa usafi wote.
3 眞に寡婦たる寡婦を敬へ、
Waheshimu wajane, wale walio wajane kweli kweli.
4 然れど寡婦にして子或は孫あらば、彼等は先家に孝行し、親に恩を報ゆる事を學ぶべし、是神の御前に嘉納せらるればなり。
Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu.
5 眞に寡婦にして寄辺なき者は神に寄頼み、晝夜祈願祈祷に從事すべし、
Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana.
6 蓋快樂に在る寡婦は、生きながらにして死したる者なり、
Hata hivyo, mwanamke yule aishiye kwa anasa amekufa, ingawaje yu hai.
7 彼等の科なからん為に是等の事を命ぜよ。
Na uyahubiri haya mambo ili kwamba wasiwe na lawama.
8 己が家族、殊に家人を顧みざる人は、信仰を棄てて不信者に劣れる者なり。
Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mmbaya kuliko mtu asiye amini.
9 寡婦の籍に録さるるは、一夫の妻たりし者にして六十才より下らず、
Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja.
10 善業の好評ある者、即ち子女を育て、若くは客を接待し、若くは聖徒の足を洗ひ、若くは困難に遇へる人々を助けし等、凡ての善業を為しし者たらざるべからず。
Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au alimesaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.
11 若き寡婦等を辞れ、蓋彼等はキリストに背きて行亂るれば嫁ぐ事を好み、
Lakini kwa wale wajane vijana, kataa kuwaandikisha kwenye orodha ya wajane. Kwa kuwa wakiingia kwenye matamanio ya kimwili dhidi ya Kristo, wanataka kuolewa.
12 最初の信を破りたる故に罪に定められ、
Kwa njia hii huingia kwenye hatia kwa kuwa huvunja kujitoa kwao kwa awali.
13 又亂惰にして家々を遊廻り、啻に亂惰なるのみならず、言多く又指出でて言ふまじき事を語る。
Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.
14 然れば我は若き寡婦の、嫁ぎて子を挙げ家事を理め、反對者をして聊も惡口の機會を有たざらしめん事を欲す、
Kwa hiyo mimi nataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, wasimamie nyumba zao, ili kutokumpa adui nafasi ya kutushitaki kwa kufanya dhambi.
15 其はサタンに立歸りたる者既に數人あればなり。
Kwa sababu baadhi yao wameshamgeukia Shetani.
16 信徒たる者、若[親族に]寡婦あらば、教會を煩はさずして自ら之を扶くべし、是教會をして眞の寡婦を扶くるに不足なからしめん為なり。
Kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane, basi na awasaidie, ili kanisa lisilemewe, ili liweze kuwasaidia wale walio wajane kweli kweli.
17 長老にして善く司る人、殊に言と教とに勞する人は、倍して尊ばるべき者とせらるべし。
Basi wazee wale watawalao vyema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima maradufu, hasa wale wanaojishughulisha na kufundisha neno la Mungu.
18 蓋聖書に曰く、「汝穀物を踏碾す牛の口を結ぶ勿れ」と、又曰く、「働く人は宜しく其報を得べし」と。
Kwa kuwa maandiko yanasema, “Usimfumbe ng'ombe kinywa apulapo nafaka,” na “Mfanya kazi anastahili mshahara wake.”
19 長老に對する訴訟は、二三の證人あるに非ずば之を受理すること勿れ。
Usipokee mashitaka dhidi ya mzee isipokuwa kuna mashahidi wawili au watatu.
20 罪を犯す者は、他の人をも懼れしめん為に、一同の前に之を咎めよ。
Waonye wakosaji mbele ya watu wote ili wengine waliobaki labda wataogopa.
21 我神とキリスト、イエズスと擇まれし天使等の御前に證して、汝が偏頗なく是等の事を守り、贔屓を以て何事をも為さざらん事を命ず。
Nakuagiza kwa dhati mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na malaika wateule, kwamba uzitunze maagizo haya bila ubaguzi wowote, na kwamba usifanye jambo lolote kwa upendeleo.
22 誰にも早く按手する事なく、又他人の罪に與る事なく、貞操にして己が身を守れ。
Usimwekee mtu yeyote mikono haraka. Usishiriki dhambi ya mtu mwingine. Yakupasa kujitunza mwenyewe uwe usafi.
23 最早水を飲まずして、胃の為又は度度の病の為に、少しく葡萄酒を用いよ。
Hakupasi kunywa maji pekee. Badala yake, unywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo na magonjwa yako ya mara kwa mara.
24 或人々の罪は審判にも先ちて明に、或人々の罪は後にて顕る、
Dhambi za baadhi ya watu hujulikana kwa uwazi, na huwatangulia hukumuni. Lakini baadhi ya dhambi hufuata baadaye.
25 善き行の顕るるも亦斯の如し、然らざるものは[終に]隠るる能はず。
Vivyo hivyo, baadhi ya kazi njema hujulikana kwa uwazi, lakini hata zingine hazitafichika.

< テモテへの手紙第一 5 >