< テモテへの手紙第一 3 >

1 第三項 聖職者の選抜 人ありて監督の務を欲するは善き業を欲するなりとは眞の談なり、
Usemi huu ni wakuaminika: Kama mtu anatamani kuwa Msimamizi, anatamani kazi njema.
2 然れば監督は、咎むべき所なく、唯一婦の夫たり、謹慎、怜悧、端正、貞潔にして旅人を接待し、善く教を施し、
Kwa hiyo msimamizi ni lazima asiwe na lawama. Ni lazima awe mume wa mke mmoja. Ni lazima awe na kiasi, busara, mwenye utaratibu, mkarimu. Ni lazima awe uwezo wa kufundisha.
3 酒を嗜まず、人を打たず、柔和にして争はず、利を貪らず、
Asiwe anatumia mvinyo, asiwe mgomvi, bali mpole, mwenye amani. Ni lazima asiwe mwenye kupenda fedha.
4 善く其家を治め、其子女の謹みて之に服從する人たらざるべからず。
Inampasa kuwasimamia vema watu wa nyumbani mwake mwenyewe, na watoto wake imewapasa kumtii kwa heshima zote.
5 人若己が家を治むるを知らずば、如何にしてか神の教會に奮励せん。
Maana ikiwa mtu hajui kuwasimamia watu wa nyumbani mwake mwenyewe, atalileaje kanisa la Mungu?
6 監督は新信徒たるべからず、恐くは驕りて惡魔に等しき審判に陥らん。
Asiwe mwamini mpya, ili kwamba asije akajivuna na kuanguka katika hukumu kama yule mwovu.
7 又外の人々に好評ある人たるべし、是耻辱と惡魔の罠とに陥らざらん為なり。
Lazima pia awe na sifa njema kwa wote walioko nje, ili asije akaanguka kwenye aibu na mtego wa mwovu.
8 執事等も斯の如く、尊くして兩舌ならず、酒を嗜まず、耻づべき利を貪らず、
Mashemasi, vilevile wanapaswa kuwa wenye kustahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili. Wasitumie mvinyo kupita kiasi au kuwa na tamaa.
9 潔き良心を以て信仰の奥義を保てる者たるべし。
Waweze kuitunza kwa dhamiri safi ile kweli ya imani iliyofunuliwa.
10 彼等も先試を受けて、咎むべき所なくば務むべきなり。
Wawe pia wamethibitishwa kwanza, halafu waweze kuhudumu kwa sababu hawana lawama.
11 婦人等も斯の如く、尊くして譏らず、節制して萬事に忠實なる者たるべし。
Wanawake vivyo hivyo wawe wenye heshima. Wasiwe wasingiziaji. Wawe na kiasi na waaminifu kwa mambo yote.
12 執事等は、一婦の夫にして善く其子女と家とを治むる者たるべし、
Mashemasi ni lazima wawe waume wa mke mmoja mmoja. Lazima waweze kuwasimamia vema watoto wao na wa nyumbani mwao.
13 其は善く務めたる者は善き階級を得て、キリスト、イエズスに於る信仰に就きて大いなる勇氣を得べければなり。
Kwa kuwa wale wanaotumika vizuri hupata msimamo mzuri na ujasiri mkubwa katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
14 我早く汝に至らん事を望みつつ是等の事を書遣るは、
Ninaandika mambo haya kwako, na ninatumaini kuja kwako hivi karibuni.
15 若遅からん時、汝をして神の家に於て如何に行ふべきかを知らしめん為なり、神の家とは活き給へる神の教會なり、眞理の柱にして且基なり。
Lakini ikiwa nitachelewa, ninaandika ili upate kujua namna ya kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambalo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msaada wa kweli.
16 實にも大いなる哉敬虔の奥義、即ち[キリストは]肉に於て顕はされ、霊によりて證せられ、天使等に顕れ、異邦人に傳へられ、世に信ぜられ、光榮に上げられ給ひしなり。
Na haipingiki kwamba kweli ya Uungu uliyofunuliwa ni mkuu: “Alionekana katika mwili, akathibitishwa na Roho, akaonekana na malaika, akatangazwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akachukuliwa juu katika utukufu.”

< テモテへの手紙第一 3 >