< ペテロの手紙第一 5 >

1 第二項 牧師及び信徒に関する特別の勧告。 汝等の中の長老には、我も共に長老として、又キリストの苦難の證人として、将來顕るべき光榮に與る者として希ふ。
Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, mimi, niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso ya Kristo, na ambaye vile vile ni mshirika katika utukufu utakaodhihirika.
2 汝等の中に在る所の神の羊の群を牧せよ、之を監督するに、強ひられてせずして喜びて神の御為にし、耻かしき利の為にせずして特志を以て行ひ、
Kwa hiyo, ninawatia moyo ninyi wazee, lichungeni kundi la Mungu lililo miongoni mwenu. Liangalieni, sio kwa sababu mnapaswa, lakini kwa sababu mnatamani hivyo, kulingana na Mungu. Liaangalieni, sio kwa kupenda pesa za aibu, lakini kwa kupenda.
3 托せられたる人々を壓制せずして、心より群の模範と成るべし。
Msijifanye mabwana juu ya watu waliyochini ya uangalizi wenu, lakini iweni mfano katika kundi.
4 然らば大牧者の顕れ給はん時、汝等凋まざる光榮の冠を得べし。
Pale Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu isiyopoteza uthamani wake.
5 若き者よ、汝等も亦長老に服せよ、皆互に謙遜を帯びよ、神は傲慢なる者に逆らひて、謙遜なる者に恩寵を賜へばなり。
Vilevile, nanyi vijana wadogo, nyenyekeni kwa wakubwa wenu. Ninyi nyote, uvaeni unyenyekevu na kuhudumiana ninyi kwa ninyi, kwani Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wanyenyekevu.
6 然れば汝等、神の全能なる御手の下に謙れ、然せば時至りて彼汝等を高め給はん。
Kwa hiyo nyenyekeni chini ya mkono wa Mungu uliyo hodari ili kwamba awainue kwa wakati wake.
7 思ひ煩ふ所を悉く神に委ね奉れ、神は汝等の為に慮り給へばなり。
Mwekeeni fadhaa zenu juu yake, kwa sababu anawajali.
8 汝等節制して警戒せよ、其は汝等の仇なる惡魔は、吼ゆる獅子の如く、食盡すべきものを探しつつ行廻ればなり、
Iweni na busara, iweni waangalifu. Yule adui yenu, ibilisi, kama simba aungurumaye ananyatia, akisaka mtu wa kumrarua.
9 汝等此世に在る兄弟等の同じく苦しめる事を知りて、信仰に心を堅めて之に抵抗せよ。
Simameni kinyume chake. Kuweni na nguvu katika imani yenu. Mkijua kwamba ndugu zenu walioko ulimwenguni wanapitia mateso kama hayo.
10 一切の恩寵の神はキリスト、イエズスによりて其永遠の光榮に汝等を呼び給ひしものなれば、聊苦しみたる上は、御自ら完全にし堅うし強からしめ給はん、 (aiōnios g166)
Baada ya kuteseka kwa muda kitambo, Mungu wa neema yote, aliyewaita katika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atawakamilisha, atawaimarisha na kuwatia nguvu. (aiōnios g166)
11 光榮と主権と世々之に歸す、アメン。 (aiōn g165)
Enzi iwe kwake milele na milele. Amina. (aiōn g165)
12 結末。 忠信なる兄弟シルヴァノを以て我が汝等に書贈りし所は、我思ふに簡単なり。是此神の恩寵の眞なる事を勧告し、且保證するもののにして、汝等宜しく之に立つべし。
Namthamini Silwano kama ndugu mwaminifu, na nimewaandikia ninyi kwa ufupi kupitia kwake. Ninawatia moyo na ninashuhudia kwamba nilichokiandika ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni ndani yake.
13 汝等と共に選まれてバビロンに在る教會、及び我子マルコは汝等に宜しくと言へり。
Waamini waliloko Babeli, waliochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu, na Marko mwanangu, anawasalimu.
14 愛の接吻を以て互に宜しく傳へよ。願はくは、キリストに在る汝等一同に平安あらん事を、アメン。
Salimianeni kila mmoja kwa busu la upendo. Na amani iwe kwenu mliondani ya Kristo.

< ペテロの手紙第一 5 >