< コリント人への手紙第一 13 >

1 我假令人間と天使との言語を語るとも、愛なければ鳴る鐘、響く鐃鈸の如くなりたるのみ。
Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
2 我假令預言する事を得て、一切の奥義一切の學科を知り、又假令山を移す程なる一切の信仰を有すとも、愛なければ何物にも非ず。
Tena, naweza kuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, nikafahamu siri zote na kujua kila kitu; naweza kuwa na imani yote hata nikaweza kuihamisha milima, lakini kama sina upendo mimi si kitu.
3 我假令わが財産を悉く(貧者の食物として)分與へ、又我身を焼かるる為に付すとも、愛なければ聊も我に益ある事なし。
Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.
4 愛は堪忍し、情あり、愛は妬まず、自慢せず、驕らず、
Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
5 非禮を為さず、己の為に謀らず、怒らず、惡を負はせず、
Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya,
6 不義を喜ばずして眞實を喜び、
hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.
7 何事をも包み、何事をも信じ、何事をも希望し、何事をも怺ふるなり。
Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.
8 預言は廃り、言語は止み、知識は亡ぶべきも、愛は何時も絶ゆる事なし。
Upendo hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita.
9 蓋我等の知る事は不完全に、預言する事は不完全なれども、
Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili.
10 完全なるところ來らば不完全なるところは廃らん。
Lakini kile kilicho kikamilifu kitakapofika, vyote visivyo vikamilifu vitatoweka.
11 我が小兒たりし時は、語る事も小兒の如く、判断する事も小兒の如く、考ふる事も小兒の如くなりしかど、大人となりては小兒の事を棄てたり。
Nilipokuwa mtoto mchanga nilisema kitoto, nilifahamu kitoto, nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtu mzima, mambo ya kitoto nimeyaacha.
12 今我等の見るは鏡を以てして朧なれども、彼時には顔と顔とを合せ、今我が知る所は不完全なれども、彼時には我が知らるるが如くに知るべし。
Tunachoona sasa ni kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapo baadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapo baadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua mimi.
13 今存するものは信、望、愛此三なれども、就中最大いなるものは愛なり。
Sasa yanadumu haya matatu: imani, tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.

< コリント人への手紙第一 13 >