< コリント人への手紙第一 10 >

1 兄弟等よ我汝等の之を知らざるを好まず、即ち我等の祖先は皆曾て雲の下に在り、皆海を過り、
Nataka ninyi mjue kaka na dada zangu, ya kuwa baba zetu walikuwa chini ya wingu na wote walipita katika bahari.
2 皆モイゼに属きて雲と海とを以て洗せられ、
Wote walibatizwa wawe wa Musa ndani ya wingu na ndani ya bahari,
3 皆同じ霊的食物を食し、
na wote walikula chakula kile kile cha roho.
4 皆同じ霊的飲料を飲めり。蓋彼等に随ひつつありし霊的盤石より飲み居りしが、其盤石は即ちキリストなりき。
Wote walikunywa kinywaji kile kile cha roho. Maana walikunywa kutoka katika mwamba wa roho uliowafuata, na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5 然れども彼等の多くは神の御旨に適はず、荒野にて斃れたり。
Lakini Mungu hakupendezwa sana na wengi wao, na maiti zao zilisambazwa jangwani.
6 是等の事は我等に於る前兆にして、彼等が貪りし如く我等が惡事を貪らざらん為なり。
Basi mambo haya yote yalikuwa mifano kwetu, ili sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya kama na wao walivyofanya.
7 汝等は又、彼等の中なる或人々の如く偶像崇拝者となる事勿れ、録して、「民は坐して飲食し、立ちて樂しめり」、とあるが如し。
Msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa. Hii ni kama ilivyoandikwa, “Watu walikaa chini wakila na kunywa, na waliinuka kucheza kwa tamaa za mapenzi.”
8 又彼等の中に私通する人々ありて、死する者一日に二萬三千人に及びしが、我等は彼等の如く私通すべからず。
Tusifanye uasherati kama wengi wao walivyofanya. Wakafa siku moja watu ishirini na tatu elfu kwa sababu hiyo.
9 又彼等の中にキリストを試むる人々ありて、蛇に亡ぼされしが、我等は彼等の如くキリストを試むべからず。
Wala tusimjaribu Kristo, kama wengi wao walivyofanya na wakaharibiwa kwa nyoka.
10 又彼等の中に呟く人々ありて、亡ぼす者に亡ぼされしが、汝等は彼等の如く呟くべからず。
Na pia msinung'unike, kama wengi wao walivyonung'unika na kuharibiwa na malaika wa mauti.
11 是等の事は皆前兆として彼等に起りつつありしが、其録されたるは、世の末が身に及べる我等の誡とならん為なり。 (aiōn g165)
Basi mambo hayo yalitendeka kama mifano kwetu. Yakaandikwa ili kutuonya sisi - tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (aiōn g165)
12 然れば自ら立てりと思ふ人は倒れじと注意すべし。
Kwa hiyo kila ajionaye amesimama awe makini asije akaanguka.
13 汝等に係る試みは人の常なるもの耳、神は眞實にて在せば、汝等の力以上に試みらるる事を許し給はず、却て堪ふることを得させん為に、試と共に勝つべき方法をも賜ふべし。
Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
14 第七項 再び供物の問題を説く 然れば我至愛なる者よ、偶像崇拝を避けよ。
Kwa hiyo, wapendwa wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.
15 我は智者に對する心にて語れば、汝等自ら我が言ふ所を判断せよ。
Nasema nanyi kama watu wenye akili, ili muamue juu ya ninalosema.
16 我等が祝する祝聖の杯は、キリストの御血を相共に授かるの義に非ずや。又我等が擘く所の麪は、相共に主の御體に與るの義に非ずや。
Kikombe cha baraka tubarikicho, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
17 蓋総て一の麪を授かる我等は、多人數なりと雖も、一の麪一の體なり。
Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja. Sisi sote twapokea mkate mmoja kwa pamoja.
18 肉に由れるイスラエル人を看よ、犠牲を食する人々は、祭壇の分配に與るに非ずや。
Watazameni watu wa Israeli: Je! Wale wote walao dhabihu si washiriki katika madhabahu?
19 然らば何事ぞ、偶像に献げられし犠牲は何物かなり、偶像は何物かなり、と我は言へるか、(然らず)。
Nasema nini basi? Ya kuwa sanamu ni kitu? Au ya kuwa chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?
20 然れども異邦人の献ぐる犠牲は、神に献ぐるに非ずして惡鬼に献ぐるなり、我汝等が惡鬼の友となる事を禁ず。汝等主の杯と惡鬼の杯とを飲む事能はず、
Lakini nasema juu ya vitu vile wavitoavyo sadaka watu wapagani wa Mataifa, ya kuwa wanatoa vitu hivi kwa mapepo na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi kushirikiana na mapepo!
21 主の祭壇と惡鬼の祭壇とに與る事能はざるなり。
Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo. Hamwezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo.
22 我等は主の妬を惹起こさんとするか、主よりも強き者なるか。何事も我に可なりと雖も、皆益あるには非ず、
Au twamtia Bwana wivu? Tuna nguvu zaidi yake?
23 何事も我に可なりと雖も、皆徳を立つるには非ず、
“Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote vifaavyo. “Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote viwajengavyo watu.
24 誰も己が為に謀らずして人の為を求むべし。
Hakuna hata mmoja angetafuta mazuri yake tu. Badala yake, kila mmoja angetafuta mazuri ya mwenzake.
25 凡肉屋にて売る物は、良心の為に何事をも問はずして食せよ、
Mnaweza kula kila kitu kiuzwacho sokoni bila kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri.
26 蓋地及び之に満てる物は主の物なり。
Maana “dunia ni mali ya Bwana, na vyote viijazavyo.”
27 汝等若不信者の中より招かれ、諾して趣く事あらば、供せらるる一切の物を、良心の為に何事をも問はずして食せよ。
Na mtu asiyeamini akiwaalika kula, na mnataka kwenda, kuleni chochote awapacho pasipo kuuliza maswali ya dhamiri.
28 人ありて是偶像に献げられたる物なりと云はば、汝等之を告げたる人に對し、また良心に對して之を食する勿れ。
Lakini mtu akiwaambia, “Chakula hiki kimetokana na sadaka ya wapagani,” msile. Hii ni kwa ajili yake aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.
29 我が所謂る良心は汝のには非ずして其人の良心なり。蓋何為ぞ人の良心に由りて我自由を是非せらるるや。
Nami simaanishi dhamiri zenu, bali dhamiri ya yule mwingine. Maana kwanini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?
30 若我感謝して食せば、何為ぞ我が感謝する所の物に就きて罵らるるや。
Ikiwa mimi natumia chakula kwa shukrani, kwanini nitukanwe kwa kitu ambacho nimeshukuru kwacho?
31 然れば汝等食ふも飲むも又何事を為すも、総て神の光榮の為にせよ。
Kwa hiyo, chochote mnachokula au kunywa, au chochote mfanyacho, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
32 汝等ユデア人にも、異邦人にも、神の教會にも、躓かするものとなる事勿れ。
Msiwakoseshe Wayahudi au Wayunani, au kanisa la Mungu.
33 猶我が己の利益となる事を求めず、多數の人の救はれん為に其有益なる事を求めて、萬事に其心を得んとするが如くせよ。
Jaribuni kama mimi ninavyojaribu kuwapendeza watu wote kwa mambo yote. Sitafuti faida yangu mwenyewe, bali ya wengi. Nami nafanya hivi ili wapate kuokolewa.

< コリント人への手紙第一 10 >