< ヨブ 記 20 >

1 そこでナアマびとゾパルは答えて言った、
Ndipo Sofari, Mnaamathi alijibu na kusema,
2 「これによって、わたしは答えようとの思いを起し、これがために心中しきりに騒ぎ立つ。
“Mawazo yangu yananifanya mimi nijibu kwa haraka kwa sababu ya mashaka yaliyomo ndani yangu mimi.
3 わたしはわたしをはずかしめる非難を聞く、しかし、わたしの悟りの霊がわたしに答えさせる。
Mimi ninasikia kukemewa ambako kunaniondolea heshima mimi, lakini roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.
4 あなたはこの事を知らないのか、昔から地の上に人の置かれてよりこのかた、
Je, unafahamu kwamba ukweli huu kutoka enzi za kale, wakati Mungu alipomweka mwanadamu juu ya nchi:
5 悪しき人の勝ち誇はしばらくであって、神を信じない者の楽しみはただつかのまであることを。
ushindi wa mtu mwovu ni mfupi, na furaha ya mtu asiyemcha Mungu hudumu kwa kitambo tu?
6 たといその高さが天に達し、その頭が雲におよんでも、
Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu, na kichwa chake yeye kufikia kwenye mawingu,
7 彼はおのれの糞のように、とこしえに滅び、彼を見た者は言うであろう、『彼はどこにおるか』と。
bado mtu huyo atapotea siku zote kama mavi yake yeye mwenyewe; wale waliokuwa wamemuona yeye watasema, 'Yuko wapi yeye'?
8 彼は夢のように飛び去って、再び見ることはない。彼は夜の幻のように追い払われるであろう。
Yeye atapaa mbali kama ndoto na hataonekana; ndivyo ilivyo, yeye atakuwa amefukuzwa mbali kama ono la
9 彼を見た目はかさねて彼を見ることがなく、彼のいた所も再び彼を見ることがなかろう。
usiku. Jicho ambalo lilimuona yeye halitamuona yeye tena; mahali pake hapatamuona yeye tena.
10 その子らは貧しい者に恵みを求め、その手は彼の貨財を償うであろう。
Watoto wake wataomba msamaha kwa watu maskini, mikono yake itaweza kurudisha utajiri wake.
11 その骨には若い力が満ちている、しかしそれは彼と共にちりに伏すであろう。
Mifupa yake imejaa nguvu za ujanani, lakini zitalala naye chini katika mavumbi.
12 たとい悪は彼の口に甘く、これを舌の裏にかくし、
Japokuwa uovu ni mtamu katika mdomo wake yeye, japokuwa yeye anauficha chini ya ulimi wake yeye,
13 これを惜しんで捨てることなく、口の中に含んでいても、
japokuwa anaushikilia pale na hauruhusu kwenda lakini bado huushikilia katika mdomo wake yeye -
14 その食物は彼の腹の中で変り、彼の内で毒蛇の毒となる。
chakula katika koromeo lake yeye hugeuka kuwa uchungu; hugeuka kuwa sumu ya majoka ndani yake yeye.
15 彼は貨財をのんでも、またそれを吐き出す、神がそれを彼の腹から押し出されるからだ。
Yeye humeza chini utajiri, lakini yeye atautapika tena; Mungu atautoa nje kutoka katika tumbo lake yeye.
16 彼は毒蛇の毒を吸い、まむしの舌は彼を殺すであろう。
Yeye atamumunya sumu ya majoka; ulimi wa nyoka mwenye sumu utamwua yeye.
17 彼は蜜と凝乳の流れる川々を見ることができない。
Yeye hatafurahia vijito vya maji, wingi wa asali na siagi.
18 彼はほねおって獲たものを返して、それを食うことができない。その商いによって得た利益をもって楽しむことができない。
Yeye atayarudisha matunda ya kazi yake na hataweza kuyala; yeye hatafurahia utajiri alioupata kwa biashara zake yeye.
19 彼が貧しい者をしえたげ、これを捨てたからだ。彼は家を奪い取っても、それを建てることができない。
Kwa kuwa yeye amewakandamiza na kuwasahau watu maskini; yeye kwa uonevu, amezichukua mbali nyumba ambazo hakuzijenga yeye.
20 彼の欲張りは足ることを知らぬゆえ、その楽しむ何物をも救うことができないであろう。
Kwa sababu yeye mwenyewe hakujua utoshelevu wowote, yeye hataweza kuokoa kitu chochote katika kile ambacho alijifurahisha.
21 彼が残して食べなかった物とては一つもない。それゆえ、その繁栄はながく続かないであろう。
Hakuna chochote kilichoachwa ambacho yeye hakukimeza; kwa hiyo mafanikio yake yeye hayatakuwa ya kudumu.
22 その力の満ちている時、彼は窮境に陥り、悩みの手がことごとく彼の上に臨むであろう。
katika wingi wa utajiri wake yeye ataanguka katika mahangaiko; mkono wa kila mmoja ambaye yuko katika umaskini utakuja kinyume chake yeye.
23 彼がその腹を満たそうとすれば、神はその激しい怒りを送って、それを彼の上に降り注ぎ、彼の食物とされる。
Wakati akiwa katika kulijaza tumbo lake, Mungu atatupa hasira ya ghadhabu yake juu yake yeye; Mungu ataunyeshea chini juu yake yeye wakati yeye anakula.
24 彼は鉄の武器を免れても、青銅の矢は彼を射通すであろう。
Ingawa mtu huyo atakimbia kutoka katika silaha ya chuma, upinde wa shaba utampiga yeye.
25 彼がこれをその身から引き抜けば、きらめく矢じりがその肝から出てきて、恐れが彼の上に臨む。
Mshale utatoboa kupitia mgongoni mwake na utatokezea; ni dhahiri, ncha inayong'ra itatokezea nje kupitia ini lake yeye; watesi huja tena juu yake.
26 もろもろの暗黒が彼の宝物のためにたくわえられ、人が吹き起したものでない火が彼を焼きつくし、その天幕に残っている者を滅ぼすであろう。
Giza lliilo kamilika limetunzwa kwa akiba zake; moto usiopulizwa utamla yeye kwa haraka; utameza kile kilichoachwa katika hema yake.
27 天は彼の罪をあらわし、地は起って彼を攻めるであろう。
Mbingu zitauweka wazi uovu wake, na nchi itainuka juu dhidi yake yeye kama shahidi.
28 その家の財産は奪い去られ、神の怒りの日に消えうせるであろう。
Utajiri wa nyumba yake utatoweka; bidhaa zake zitamwagika mbali siku ya ghadhabu ya Mungu.
29 これが悪しき人の神から受ける分、神によって定められた嗣業である」。
Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kutoka kwa Mungu, urithi uliotunzwa akiba na Mungu kwa ajili yake yeye.”

< ヨブ 記 20 >