< エレミヤ書 15 >

1 主はわたしに言われた、「たといモーセとサムエルとがわたしの前に立っても、わたしの心はこの民を顧みない。彼らをわたしの前から追い出し、ここを去らせよ。
Kisha Bwana akaniambia, “Hata kama Musa au Samweli walisimama mbele yangu, bado sitawafikiria watu hawa. Watoe mbele yangu, ili waweze kuondoka.
2 もし彼らが、『われわれはどこに行けばよいのか』とあなたに尋ねるならば、彼らに言いなさい、『主はこう仰せられる、疫病に定められた者は疫病に、つるぎに定められた者はつるぎに、ききんに定められた者はききんに、とりこに定められた者はとりこに行く』。
Ikiwa watakuambia, 'Tunapaswa kwenda wapi?' Kisha uwaambie, 'Bwana asema hivi Wale wanaotakiwa kufa wanapaswa kufa; wale waliotayarishwa kwa upanga wanapaswa kwenda kwa upanga. Wale waliopelekwa kwa njaa wanapaswa kwenda kwa njaa; na wale waliopelekwa uhamisho wanapaswa kuhamishwa.'
3 主は仰せられる、わたしは四つの物をもって彼らを罰する。すなわち、つるぎをもって殺し、犬をもってかませ、空の鳥と地の獣をもって食い滅ぼさせる。
Kwa kuwa nitawapa kwa makundi manne-hili ndilo tamko la Bwana-upanga wa kuua wengine, mbwa wararue, ndege wa angani na mnyama mkali wale na kuangamiza.
4 またユダの王ヒゼキヤの子マナセが、エルサレムでした行いのゆえに、わたしは彼らを地のすべての国が見て恐れおののくものとする。
Nitawafanyia jambo lenye kutisha kwa falme zote za dunia, kwa sababu Manase mwana wa Hezekia, mfalme wa Yuda, alifanya huko Yerusalemu.
5 エルサレムよ、だれがあなたをあわれむであろうか。だれがあなたのために嘆くであろうか。だれがふり返って、あなたの安否を問うであろうか。
Kwa maana ni nani atakayewahurumia, Yerusalemu? Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako? Nani atakayegeuka kuuliza kuhusu ustawi wako?
6 主は言われる、あなたはわたしを捨てた。そしてますます退いて行く。それゆえ、わたしは手を伸べてあなたを滅ぼした。わたしはあわれむことには飽きた。
Umeniacha-hili ndilo tamko la Bwana-umerudi nyuma. Kwa hiyo nitawapiga kwa mkono wangu na kukuangamiza. Nimechoka kuwahurumia.
7 わたしはこの地の門で、箕で彼らをあおぎ分けた。彼らがその道を離れなかったので、わたしは彼らの子を奪い、わが民を滅ぼした。
Kwa hiyo nitawapepea kwa kipepeo katika milango ya nchi. Nitawafukuza. Nitawaangamiza watu wangu kwani hawakurudi na kuziacha njia zao.
8 わたしは彼らの寡婦の数を浜べの砂よりも多くした。わたしは真昼に、滅ぼす者を連れてきて、若者らの母たちをせめ、驚きと恐れを、にわかに母たちにおこした。
Nitawafanya wajane wao kuwa zaidi ya mchanga wa bahari. Dhidi ya mama wa vijana nitamtuma mwangamizi mchana. Nitafanya mshtuko na hofu ghafla kuanguka juu yao.
9 七人の子を産んだ女は、弱り衰えて、息絶え、まだ昼であったが、彼女の日は没した。彼女は恥じ、うろたえた。その残りの者は、これを敵のつるぎに渡すと主は言われる」。
Mama aliyezaa watoto saba ataharibika. Atashuka. Jua lake limekuchwa wakati bado ni siku. Yeye atakuwa na aibu na kufedheheka, kwa kuwa nitawatoa wale waliosalia kwa upanga mbele ya maadui zao-hili ndilo tamko la Bwana.”
10 ああ、わたしはわざわいだ。わが母よ、あなたは、なぜ、わたしを産んだのか。全国の人はわたしと争い、わたしを攻める。わたしは人に貸したこともなく、人に借りたこともないのに、皆わたしをのろう。
Ole wangu, mama yangu! Kwa maana umenizaa, mimi ambaye ni mtu wa kushindana na hoja katika nchi yote. Sijakopesha, wala hakuna mtu aliyenikopesha, lakini wote wananilaani.
11 主よ、もしわたしが彼らの幸福をあなたに祈り求めず、また敵のため、その悩みのときと、災のときに、わたしがあなたにとりなしをしなかったのであれば、彼らののろいも、やむをえないでしょう。
Bwana akasema “Je sitakuokoa kwa manufaa? Kwa hakika nitawafanya maadui wako waombe msaada wakati wa msiba na dhiki.
12 人は鉄を、北からくる鉄や青銅を砕くことができましょうか。
Je, mtu anaweza kusaga chuma? Hasa chuma kutoka kaskazini iliyochanganywa na shaba?
13 「わたしはあなたの富と宝を、ぶんどり物として他に与える。代価を受けることはできない。それはあなたのすべての罪によるので、領域内のいたる所にこのことが起る。
Nitawapa adui zako utajiri wako na hazina yako kama nyara za bure. Nitafanya hili kwa sababu ya dhambi zako zote zilizofanywa ndani ya mipaka yako yote.
14 わたしはあなたの知らない地で、あなたの敵に仕えさせる。わたしの怒りによって火は点じられ、いつまでも燃え続けるからである」。
Ndipo nitakufanya utumikie adui zako katika nchi ambayo huijui, maana moto utawaka, ukawaka katika ghadhabu yangu juu yako.”
15 主よ、あなたは知っておられます。わたしを覚え、わたしを顧みてください。わたしを迫害する者に、あだを返し、あなたの寛容によって、わたしを取り去らないでください。わたしがあなたのために、はずかしめを受けるのを知ってください。
Wewe mwenyewe wajua, Bwana! Unikumbuke na kunisaidia. Ukanilipie kisasi kwa ajili ya wanaonifuata. Katika uvumilivu wako usiniondoe. Utambue kwamba nimekuwa na aibu kwa ajili yako. Maneno yako yamepatikana, na nikayala.
16 わたしはみ言葉を与えられて、それを食べました。み言葉は、わたしに喜びとなり、心の楽しみとなりました。万軍の神、主よ、わたしは、あなたの名をもってとなえられている者です。
Maneno yako yalikuwa furaha kwangu, furaha yangu kwa moyo wangu; kwa maana jina lako linatangazwa juu yangu, Bwana, Mungu wa majeshi.
17 わたしは笑いさざめく人のつどいにすわることなく、また喜ぶことをせず、ただひとりですわっていました。あなたの手がわたしの上にあり、あなたが憤りをもってわたしを満たされたからです。
Sikuketi katika mkutano wa wale waliosherehekea au waliofurahi. Nimeketi kwa faragha kwa sababu ya mkono wako wenye nguvu, kwa maana umenijaza na hasira.
18 どうしてわたしの痛みは止まらず、傷は重くて、なおらないのですか。あなたはわたしにとって、水がなくて人を欺く谷川のようになられるのですか。
Kwa nini maumivu yangu yanaendelea na jeraha langu halitibiki, linakataa kuponywa? Je, utakuwa kama maji ya udanganyifu kwangu, maji yanayokauka?
19 それゆえ主はこう仰せられる、「もしあなたが帰ってくるならば、もとのようにして、わたしの前に立たせよう。もしあなたが、つまらないことを言うのをやめて、貴重なことを言うならば、わたしの口のようになる。彼らはあなたの所に帰ってくる。しかしあなたが彼らの所に帰るのではない。
Kwa hiyo Bwana asema hivi, “Yeremia, Ikiwa utatubu, nitakurejesha, nawe utasimama mbele yangu na kunitumikia. Kwa maana ukitenganisha mambo ya kipumbavu kwa vitu vya thamani, utakuwa kama kinywa changu. Watu watakuja kwako, lakini wewe mwenyewe usirudi kwao.
20 わたしはあなたをこの民の前に、堅固な青銅の城壁にする。彼らがあなたを攻めても、あなたに勝つことはできない。わたしがあなたと共にいて、あなたを助け、あなたを救うからであると、主は言われる。
Nitakufanya kama ukuta wa shaba usioweza kuingilika kwa watu hawa, nao watapigana vita dhidi yako. Lakini hawatakushinda, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe ili kuokoa na kukuponya-hili ndilo tamko la Bwana-
21 わたしはあなたを悪人の手から救い、無慈悲な人の手からあがなう」。
kwa maana nitakuokoa mikononi mwa waovu na kukukomboa katika mkono wa mshindani.”

< エレミヤ書 15 >