< エゼキエル書 4 >

1 人の子よ、一枚のかわらを取って、あなたの前に置き、その上にエルサレムの町を描きなさい。
“Lakini wewe, mwana wa adamu, chukua tofali wewe mwenyewe na uliweke mbele yako. Kisha chonga mji wa Yerusalemu juu yake.
2 そしてこれを取り囲み、これにむかって雲梯を設け、塁を築き、陣を張り、その回りに城くずしを備えてこれを攻めなさい。
Kisha laza kuizunguka, ngome juu yake. Anza kushambulia juu yake na weka makambi kuizunguka. Weka shambulio la ghasia kuizunguka.
3 また鉄の板をとり、それをあなたと町の間に置いて鉄の壁となし、あなたの顔をこれに向けなさい。町をこのように囲んで、その包囲を押し進めなさい。これがイスラエルの家のしるしである。
Kisha chukua kwa ajili yako mwenyewe sufuria ya chuma na itumie kama ukuta wa chuma kati yako mwenyewe na mji na weka uso wako dhidi yake. Kwa kuwa utazingirwa, na utaweka ukombozi juu yake. Hii itakuwa alama kwa nyumba ya Israeli.
4 あなたはまた自分の左脇を下にして寝なさい。わたしはあなたの上にイスラエルの家の罰を置く。あなたはこのようにして寝ている日の間、彼らの罰を負わなければならない。
Kisha, lala juu upande wako wa kushoto na weka dhambi ya nyumba ya Israeli juu yake; utazibeba dhambi zao kwa hesabu za siku ambazo ulizolala juu ya nyumba ya Israeli.
5 わたしは彼らの罰の年数に等しいその日数、すなわち三百九十日をあなたのために定める。その間あなたはイスラエルの家の罰を負わなければならない。
Mimi mwenyewe nakuagiza kwako siku moja kuwakilisha kila mwaka wa adhabu yao: siku 390! Katika njia hii, utachukua dhambi ya nyumba ya Israeli.
6 あなたはその期間を終ったなら、また右脇を下にして寝て、ユダの家の罰を負わなければならない。わたしは一日を一年として四十日をあなたのために定める。
Wakati utakapomaliza hizi siku, kisha lala chini kwa mara ya pili kwa upande wako wa kulia, kwa kuwa utabeba dhambi ya nyumba ya Yuda kwa siku arobaini. Nakuteua wewe siku moja kwa kila mwaka.
7 あなたは自分の顔をエルサレムの包囲の方に向け、腕をあらわし、町に向かって預言しなければならない。
Weka uso wako chini kuelekea Yerusalemu ambayo ni chini ya ngome, na kwa mkono wako funua unabii dhidi
8 見よ、わたしはあなたに、なわをかけて、あなたの包囲の期間の終るまで、左右に動くことができないようにする。
yake. Tazama! naweka vifungo juu yako hivyo hutarudi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine hadi utakapoliza siku zako za kuzingirwa kwako.
9 あなたはまた小麦、大麦、豆、レンズ豆、あわ、はだか麦を取って、一つの器に入れ、これでパンを造り、あなたが横になって寝る日の数、すなわち三百九十日の間これを食べなければならない。
Chukua ngano kwa ajili yako, shayiri, dengu, mtama, kusemethi; viweke kwenye chombo kimoja na tengeneza mkate kwa ajili yako kulingana na hesabu ya siku ambazo utakazo lala katika ya upande wako. Kwa siku 390 utaula.
10 あなたが食べる食物は量って一日に二十シケルである。あなたは一日に一度これを食べなければならない。
Chakula utakachokula kitapimwa, shekeli ishirini kwa siku, na utakila kwa mda uliopangwa kila siku.
11 また水を量って一ヒンの六分の一を一日に一度飲まなければならない。
Kisha utakunywa maji, kwa kuyapima sehemu ya sita ya hini, na utayanywa kwa mda uliopangwa.
12 あなたは大麦の菓子のようにしてこれを食べなさい。すなわち彼らの目の前でこれを人の糞で焼かなければならない」。
Utakila kama keki za shayiri, lakini utaioka kwenye kinyesi kikavu cha mwanadamu mbele ya macho yao!”
13 そして主は言われた、「このようにイスラエルの民はわたしが追いやろうとする国々の中で汚れたパンを食べなければならない」。
Kwa kuwa Yahwe asema, “Hii inamaana kwamba ule mkate ambao watu wa Israeli watakula kitakuwa kinajisi, huko miongoni mwa mataifa ambapo nitakaowafukuza.”
14 そこでわたしは言った、「ああ、主なる神よ、わたしは自分を汚したことはありません。わたしは幼い時から今日まで、自然に死んだものや、野獣に裂き殺されたものを食べたことはありません。また汚れた肉がわたしの口にはいったことはありません」。
Lakini nikasema, “Ee, Bwana Yahwe! Sijawahi kuwa najisi! sijawahi kula kitu chochote ambacho kimekufa au kitu chochote kilichouawa na wanyama, kutoka mdomoni mwangu hadi sasa, wala nyama ya kunuka haijawahi kuingia kinywani mwangu!”
15 すると彼はわたしに言われた、「見よ、わたしは牛の糞をもって人の糞に換えることをあなたにゆるす。あなたはそれで自分のパンを整えなさい」。
Ndivyo alivvyo niambia, “Tazama! Nimekupa mbolea ya ng'ombe badala ya kinyesi cha mwanadamu ili uweze kuandaa mkate wako juu ya hayo.”
16 またわたしに言われた、「人の子よ、見よ、わたしはエルサレムで人のつえとするパンを打ち砕く。彼らはパンを量って、恐れながら食べ、また水を量って驚きながら飲む。
Pia akanambia, “Mwana wa adamu! Tazama! Nalivunja gongo la mkate katika Yerusalemu, na watakula mkate ukiwa umepimwa katika wasiwasi na kunywa maji kwa kuyapima katika hofu.
17 これは彼らをパンと水とに乏しくし、互に驚いて顔を見合わせ、その罰のために衰えさせるためである。
Kwa sabau watapungukiwa na mkate na maji, kila mtu atafadhaishwa na ndugu yake na kumpoteza kwa sababu ya udhalimu wao.”

< エゼキエル書 4 >