< エゼキエル書 12 >

1 主の言葉がわたしに臨んだ、
Neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 「人の子よ、あなたは反逆の家の中にいる。彼らは見る目があるが見ず、聞く耳があるが聞かず、彼らは反逆の家である。
“Mwana wa adamu, unaishi kwenye nyumba ya uasi, wana macho ya kuona lakini hawaoni; na wana masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa sababu wao ni nyumba iliyoasi.
3 それゆえ、人の子よ、捕囚の荷物を整え、彼らの目の前で昼のうちに移れ、彼らの目の前であなたの所から他の所に移れ。彼らは反逆の家であるが、あるいは彼らは顧みるところがあろう。
Kwa hiyo wewe mwanadamu, andaa mambo yako kwa ajili ya uhamisho, na anza kuondoka mchana usoni kwao, kwa kuwa nitakuhamisha kwenye uso wao kutoka sehemu yao kwenda sehemu nyingine. Labda wataanza kuona, kuwa wao ni nyumba ya uasi.
4 あなたは、捕囚の荷物のようなあなたの荷物を、彼らの目の前で昼のうちに持ち出せ。そして捕囚に行くべき人々のように、彼らの目の前で夕べのうちに出て行け。
Utatoa vitu vyako kwa ajili ya kuhamisha mchana katika macho yao; toka jioni kwenye macho yao kama ambavyo uendavyo kwenye uhamisho.
5 すなわち彼らの目の前で壁に穴をあけ、そこから出て行け。
Chimba shimo ukutani kwenye uso wa macho yao, na ingia ndani yake.
6 あなたは彼らの目の前でその荷物を肩に負い、やみのうちにそれを運び出せ。あなたの顔をおおって地を見るな。わたしはあなたをしるしとなして、イスラエルの家に示すのだ」。
Kwenye macho yao, chukua vitu vyako kwenye mabega yako, na uwalete kwenye giza. Funika uso wako kama ishara kwenye nyumba ya Israeli.”
7 そこでわたしは命じられたようにし、捕囚の荷物のような荷物を昼のうちに持ち出し、夕べにはわたしの手で壁に穴をあけ、やみのうちに彼らの目の前で、これを肩に負って運び出した。
Hivyo nikafanya hivyo, kama nilivyokuwa nimeamriwa. Nikatoa vitu vya uhamisho wakati wa mchana, na katika jioni nikachimba shimo hata kwenye ukuta kwa mkono. Nikachukua vitu vyangu kwenye giza, na kuviweka juu kwenye bega langu katika macho yao.
8 次の朝、主の言葉がわたしに臨んだ、
Kisha neno la Yahwe likanijia asubuhi, likisema,
9 「人の子よ、反逆の家であるイスラエルの家は、あなたに向かって、『何をしているのか』と言わなかったか。
Mwanadamu, je nyumba ya Israeli, ile ni nyumba ya uasi, hawakukwambia, 'Unafanya nini?'
10 あなたは彼らに言いなさい、『主なる神はこう言われる、この託宣はエルサレムの君、およびその中にあるイスラエルの全家にかかわるものである』と。
Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: hili tendo la kinabii linamhuusu mwana wa mfalme wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao.'
11 また言いなさい、『わたしはあなたがたのしるしである。わたしがしたとおりに彼らもされる。彼らはとりこにされて移される』と。
Sema, 'Mimi ni ishara kwenu. Kama nilivyofanya, itafanyika kwao; watakwenda uhamishoni na kuwa wafungwa.
12 彼らのうちの君は、やみのうちにその荷物を肩に載せて出て行く。彼は壁に穴をあけて、そこから出て行く。彼は顔をおおって、自分の目でこの地を見ない。
Yule mwana wa mfalme aliye miongoni mwao atavibeba vitu vyake kwenye bega lake katika giza, na ataenda zake kupitia kwenye ukuta. Watachimba kwenye ukuta na kutoa vitu vyao nje. Atafunika uso wake, hivyo hataona nchi kwa macho yake.
13 わたしはわたしの網を彼の上に打ちかける。彼はわたしのわなにかかる。わたしは彼をカルデヤびとの地のバビロンに引いて行く。しかし彼はそれを見ないで、そこで死ぬであろう。
Nitausambaza wavu wangu juu yake naye atanaswa kwenye mtego wangu; kisha nitamleta Babeli, ncha ya Wakaldayo, lakini hataiona. Atafia huko.
14 またすべて彼の周囲にいて彼を助ける者および彼の軍隊を、わたしは四方に散らし、つるぎを抜いてそのあとを追う。
Pia nitatawatawanya katika kila mwelekeo wale wote waliomzunguka wanaomsaidia na jeshi lake lote, na nitaufuata upanga nyuma yao.
15 わたしが彼らを諸国民の中に散らし、国々にまき散らすとき、彼らはわたしが主であることを知る。
Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakapo watawanya kwenye nchi zote.
16 ただし、わたしは彼らのうちに、わずかの者を残して、つるぎと、ききんと、疫病を免れさせ、彼らがおこなったもろもろの憎むべきことを、彼らが行く国びとの中に告白させよう。そして彼らはわたしが主であることを知るようになる」。
Lakini nitaacha kuwaangamiza watu wachache kutoka miongoni mwao kutoka kwenye upanga, njaa, na tauni, hivyo wanaweza kukumbuka maovu yao yote katika nchi zao nilipowachukulia, hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe.”'
17 主の言葉がまたわたしに臨んだ、
Neno la Yahwe likanijia, likisema,
18 「人の子よ、震えてあなたのパンを食べ、おののきと恐れとをもって水を飲め。
“Mwanadamu, kula mkate wako kwa kutetemeka, na kunywa maji yako kwa mtetemo na hofu.
19 そしてこの地の民について言え、主なる神はイスラエルの地のエルサレムの民についてこう言われる、彼らは恐れをもってそのパンを食べ、驚きをもってその水を飲むようになる。これはその地が、すべてその中に住む者の暴虐のために衰え、荒れ地となるからである。
Kisha waambie watu wa nchi, 'Bwana Yahwe asema hivi kuhusiana na wale wakaao Yerusalemu, na nchi ya Israeli: Watakula mikate yao kwa kutetemeka na kunywa maji yao wakiwa wanatetemeka, kwa kuwa nchi itaporwa vitu vyote viijazavyo kwa sababu ya kuwa kinyume na waishio huko.
20 人の住んでいた町々は荒れはて、地は荒塚となる。そしてあなたがたは、わたしが主であることを知るようになる」。
Hivyo ile miji iliyokuwa wenyeji itachukuliwa, na nchi itakuwa ukiwa; hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe.”'
21 主の言葉がわたしに臨んだ、
Tena neno la Yahwe likanijia, likisema,
22 「人の子よ、イスラエルの地について、あなたがたが『日は延び、すべての幻はむなしくなった』という、このことわざはなんであるか。
“Mwanadamu, je ni mithali gani hii mlio nayo katika nchi ya Israeli mliyoisema, 'Siku zimerefushwa, na kila ono linaanguka'?
23 それゆえ、彼らに言え、『主なる神はこう言われる、わたしはこのことわざをやめさせ、彼らが再びイスラエルで、これをことわざとしないようにする』と。しかし、あなたは彼らに言え、『日とすべての幻の実現とは近づいた』と。
Kwa hiyo, waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Nitaweka mwisho wa hii mithali, na watu wa Israeli hawataitumia tena.' Waambie, 'Siku zi karibu wakati kila ono litatimizwa.
24 イスラエルの家のうちには、もはやむなしい幻も、偽りの占いもなくなる。
Kwa kuwa hakutakuwa na maono ya uongo yoyote wala upendeleo wa mgawanyiko kati ya nyumba ya Israeli.
25 しかし主なるわたしは、わが語るべきことを語り、それは必ず成就する。決して延びることはない。ああ、反逆の家よ、あなたの日にわたしはこれを語り、これを成就すると、主なる神は言われる」。
Kwa kuwa mimi Yahwe! Nimesema, na nitayatiza yale maneno nilyoyasema. Hakuna kitu kitakacho chelewesha. Kwa kuwa nitaongea hili neno katika siku zenu, nyumba ya uasi, na nitalitimiza! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.””
26 主の言葉がまたわたしに臨んだ、
Tena neno la Yahwe likanijia, likisema,
27 「人の子よ、見よ、イスラエルの家は言う、『彼の見る幻は、なお多くの日の後の事である。彼が預言することは遠い後の時のことである』と。
“Mwanadamu! Tazama, nyumba ya Israeli imesema, 'Lile ono alionalo ni kwa siku nyingi kutoka sasa, na ametabiri kipindi kilicho mbali sana.'
28 それゆえ、彼らに言え、主なる神はこう言われる、わたしの言葉はもはや延びない。わたしの語る言葉は成就すると、主なる神は言われる」。
Kwa hiyo waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Neno langu halitacheleweshwa sana, lakini lile neno nililoliongea litatimizwa-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.'”

< エゼキエル書 12 >