< 申命記 12 >

1 これはあなたの先祖たちの神、主が所有として賜わる地で、あなたがたが世に生きながらえている間、守り行わなければならない定めと、おきてである。
Hizi ni amri na sheria ambazo mtazishika katika nchi ambayo, Yahwe Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, siku zote mnazoishi kwenye ardhi.
2 あなたがたの追い払う国々の民が、その神々に仕えた所は、高い山にあるものも、丘にあるものも、青木の下にあるものも、ことごとくこわし、
Hakika mtaharibu maeneo yote ambapo mataifa mtakayofukuza miungu yao walioabudu, kwenye milima mirefu, kwenye vilima, na chini ya kila mti wa kijani.
3 その祭壇をこぼち、柱を砕き、アシラ像を火で焼き、また刻んだ神々の像を切り倒して、その名をその所から消し去らなければならない。
Na mtazivunja madhabahu zao chini, mtaharibu kwa vipandepande nguzo zao za mawe, na kuchoma ncha za Asherahi, mtazikata sanaa za kuchongwa za miungu yao na kuangamiza jina lao nje ya eneo hilo.
4 ただし、あなたがたの神、主にはそのようにしてはならない。
Hamtamwabudu Yahwe Mungu wenu kama hivyo.
5 あなたがたの神、主がその名を置くために、あなたがたの全部族のうちから選ばれる場所、すなわち主のすまいを尋ね求めて、そこに行き、
Lakini kwa eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kutoka makabila yenu kuweka jina lake, hapo patakuwa ni eneo analoishi na huko ndiyo mtaenda.
6 あなたがたの燔祭と、犠牲と、十分の一と、ささげ物と、誓願の供え物と、自発の供え物および牛、羊のういごをそこに携えて行って、
Ni huko ndiko mtaleta sadaka ya kutekeketezwa, dhabihu zenu, zaka zenu, na sadaka zinazotolewa kwa mkono wenu, sadaka zenu za viapo, sadaka za utayari na mzao wa kwanza wa mifugo na wanyama.
7 そこであなたがたの神、主の前で食べ、あなたがたも、家族も皆、手を労して獲るすべての物を喜び楽しまなければならない。これはあなたの神、主の恵みによって獲るものだからである。
Ni huko mtakula mbele za Yahwe Mungu wenu na kufurahi kuhusu kila kitu ambacho mmeweka mkono, nyie na jamaa zenu, ambapo Yahwe Mungu wenu amewabariki.
8 そこでは、われわれがきょうここでしているように、めいめいで正しいと思うようにふるまってはならない。
Hamtafanya mambo yote ambayo tunafanya hapa leo; sasa kila moja anafanya chochote kile kizuri machoni pake,
9 あなたがたはまだ、あなたがたの神、主から賜わる安息と嗣業の地に、はいっていないのである。
kwa kuwa bado hamjapumzika, kwa urithi ambao Yahwe Mungu wenu anawapa.
10 しかし、あなたがたがヨルダンを渡り、あなたがたの神、主が嗣業として賜わる地に住むようになり、さらに主があなたがたの周囲の敵をことごとく除いて、安息を与え、あなたがたが安らかに住むようになる時、
Lakini pindi mnaenda ng'ambo ya pili ya Yordani na kuishi ndani ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anasababisha ninyi kurithi, na wakati awapa pumziko kutoka kwa maadui zenu wanaowazunga karibu, ili kusudi muishi kwa usalama,
11 あなたがたの神、主はその名を置くために、一つの場所を選ばれるであろう。あなたがたはそこにわたしの命じる物をすべて携えて行かなければならない。すなわち、あなたがたの燔祭と、犠牲と、十分の一と、ささげ物およびあなたがたが主に誓ったすべての誓願の供え物とを携えて行かなければならない。
kisha itakuwa eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kusababisha jina lake kuishi, huko mtaleta yote ninayowaamuru; sadaka za kuteketezwa, dhabihu zenu, zaka zenu, sadaka zilizotolewa kwa mkono wenu, na sadaka za chaguo lenu kwa ajili ya nadhiri mtakazotoa kwa Yahwe.
12 そしてあなたがたのむすこ、娘、しもべ、はしためと共にあなたがたの神、主の前に喜び楽しまなければならない。また町の内におるレビびととも、そうしなければならない。彼はあなたがたのうちに分け前がなく、嗣業を持たないからである。
Mtafurahi mbele za Yahwe Mungu wenu-nyie, watoto wenu, binti zenu, wajakazi wa kiume, wajakazi wa kike, na Walawi walio ndani ya lango lenu, kwa sababu hana sehemu au urithi miongoni mwenu.
13 慎んで、すべてあなたがよいと思う場所で、みだりに燔祭をささげないようにしなければならない。
Uwe makini mwenyewe kwamba usitoe sadaka zako za kuteketezwa kila eneo unaloona;
14 ただあなたの部族の一つのうちに、主が選ばれるその場所で、燔祭をささげ、またわたしが命じるすべての事をしなければならない。
lakini ni katika eneo hilo ambalo Yahwe atawachagua miongoni moja kati ya makabila yenu ambalo litatoa sadaka ya kuteketezwa, na huko mtafanya kila kitu ninachokuamuru.
15 しかし、あなたの神、主が賜わる恵みにしたがって、すべて心に好む獣を、どの町ででも殺して、その肉を食べることができる。すなわち、かもしかや雄じかの肉と同様にそれを、汚れた人も、清い人も、食べることができる。
Hata hivyo, mtaweza kuua na kula wanyama ndani ya malango yenu, kama mnavyotaka, kupokea baraka ya Yahwe Mungu wenu kwa ajili ya yote amewapa; na watu wasio safi na safi wote wanaweza kula, wanyama kama vile paa na kulungu.
16 ただし、その血は食べてはならない。水のようにそれを地に注がなければならない。
Lakini hamtakula damu, mtaimwaga kwenye ardhi kama maji.
17 あなたの穀物と、ぶどう酒と、油との十分の一および牛、羊のういご、ならびにあなたが立てる誓願の供え物と、自発の供え物およびささげ物は、町の内で食べることはできない。
Mnaweza msile ndani ya malango kutoka kwenye zaka ya nafaka zenu, mvinyo wenu mpya, mafuta yenu au mzao wa kwanza wa mifugo au wanyama; na mnaweza msile nyama yoyote mnayoitoa dhabihu pamoja na viapo vyovyote vyenu mnafanya, wala sadaka yenu ya utayari, wala sadaka mnayotoa kwa mkono wenu.
18 あなたの神、主が選ばれる場所で、あなたの神、主の前でそれを食べなければならない。すなわちあなたのむすこ、娘、しもべ、はしため、および町の内におるレビびとと共にそれを食べ、手を労して獲るすべての物を、あなたの神、主の前に喜び楽しまなければならない。
Badala yake, mtakula mbele ya Yahwe Mugu wenu katika eneo ambalo Yahwe Mungu atachagua- nyie, mtoto wenu, binti yenu, mjakazi wa kiume, mjakazi wa kike, na Mlawi aliye malangoni mwenu; mtafurahi mbele ya Yahwe Mungu wenu kuhusu kila kitu ambacho mnaweka mkono wenu.
19 慎んで、あなたが世に生きながらえている間、レビびとを捨てないようにしなければならない。
Muwe makini wenyewe ili kwamba msimwache Mlawi maadamu mnaishi kwenye nchi yenu.
20 あなたの神、主が約束されたように、あなたの領域を広くされるとき、あなたは肉を食べたいと願って、『わたしは肉を食べよう』と言うであろう。その時、あなたはほしいだけ肉を食べることができる。
Wakati Yahwe Mungu wenu apanua mipaka yenu, kama alivyowaahidi, na kusema, “Nitakula nyama,” kwa sababu ya tamaa zenu mnakula nyama, mnaweza kula nyama, kama tanmaa za roho zenu.
21 もしあなたの神、主がその名を置くために選ばれる場所が、遠く離れているならば、わたしが命じるように、主が賜わる牛、羊をほふり、門の内で、ほしいだけ食べることができる。
Kama eneo ambalo Yahwe Mungu wenu achagua kuliweka jina lake ni mbali kutoka kwenu, basi mtaua baadhi ya mifugo yenu na wanyama wenu ambao Yahwe amewapa, kama nilivyowaamuru: hivyo mnaweza kula ndani ya malango yenu, kama tamaa za roho zenu.
22 かもしかや、雄じかを食べるように、それを食べることができる。すなわち汚れた人も、清い人も一様にそれを食べることができる。
Kama paa na Kulungu wanaliwa, hivyo mtakula watu wasio safi na wasafi wanaweze kula kadhalika.
23 ただ堅く慎んで、その血を食べないようにしなければならない。血は命だからである。その命を肉と一緒に食べてはならない。
Lakini muwe na uhakika kwamba hamtumii damu, kwa kuwa damu ni uhai, hamtakula uhai pamoja na nyama.
24 あなたはそれを食べてはならない。水のようにそれを地に注がなければならない。
Hamtakula, mtaimwaga nje kwenye ardhi kama maji.
25 あなたはそれを食べてはならない。こうして、主が正しいと見られる事を行うならば、あなたにも後の子孫にも、さいわいがあるであろう。
Hamtakula, ili kwamba iweze kuwa vizur kwenu, na watoto wenu baada yenu, wakati mtafanya kile kilicho sahihi machoni pa Yahwe.
26 ただあなたのささげる聖なる物と、誓願の物とは、主が選ばれる場所へ携えて行かなければならない。
Lakini mambo ambayo ni ya Yahwe ambayo mnayo na sadaka za viapo vyenu-mtachukua hizi na kwenda eneo ambalo Yahwe achagua.
27 そして燔祭をささげる時は、肉と血とをあなたの神、主の祭壇の上にささげなければならない。犠牲をささげる時は、血をあなたの神、主の祭壇にそそぎかけ、肉はみずから食べることができる。
Hapo mtatoa sadaka ya kuteketekezwa, nyama na damu, kwenye madhabahu ya Yahwe Mungu wenu, damu ya dhabihu zenu itamwangwa nje kwenye madhabahu ya Yahwe Mungu wenu, na mtakula nyama.
28 あなたはわたしが命じるこれらの事を、ことごとく聞いて守らなければならない。こうしてあなたの神、主が見て良いとし、正しいとされる事を行うならば、あなたにも後の子孫にも、長くさいわいがあるであろう。
Mchunguze na msikilize haya maneno yote ambayo - ninawaamuru, ili iwe uzuri kwenu na watoto wenu baada yenu milele, wakati mnafanya kile kilicho kizuri na sawa machoni pa Yahwe Mungu wenu.
29 あなたの神、主が、あなたの行って追い払おうとする国々の民を、あなたの前から断ち滅ぼされ、あなたがついにその国々を獲て、その地に住むようになる時、
Wakati Yahwe Mungu wenu anapunguza mataifa kutoka kwenu, wakati mnaingia kuwafukuza, na mnawafukuza na kuishi katika nchi yao,
30 あなたはみずから慎み、彼らがあなたの前から滅ぼされた後、彼らにならって、わなにかかってはならない。また彼らの神々を尋ね求めて、『これらの国々の民はどのようにその神々に仕えたのか、わたしもそのようにしよう』と言ってはならない。
muwe makini wenyewe ili kwamba msinaswe kwa kuwafuata, baada ya kuangamizwa kutoka kwenu kunaswa katika kuchunguza miungu yao, katika kuuliza, “Kwa namna gani haya mataifa yanaabudu muingu yao? Nitafanya hivyo hivyo.
31 あなたの神、主に対しては、そのようにしてはならない。彼らは主の憎まれるもろもろの忌むべき事を、その神々にむかって行い、むすこ、娘をさえ火に焼いて、神々にささげたからである。
Hautafanya hivyo katika kumheshimu Yahwe Mungu wako, kwa kuwa kila kitu ambacho ni chukizo kwa Yahwe, mambo ambayo anayachukia- wamefanya haya na miungu yao, hata mnateketeza vijana wao na binti zao kwenye moto kwa ajili ya miungu yao.
32 あなたがたはわたしが命じるこのすべての事を守って行わなければならない。これにつけ加えてはならない。また減らしてはならない。
Chochote ninakuamuru, chunguza. Usiongeze juu yake au kupunguza.

< 申命記 12 >