< 列王記Ⅱ 20 >

1 そのころ、ヒゼキヤは病気になって死にかかっていた。アモツの子預言者イザヤは彼のところにきて言った、「主はこう仰せられます、『家の人に遺言をなさい。あなたは死にます。生きながらえることはできません』」。
Katika siku hizo Hezekia aliugua akawa kwenye hatari ya kufa. Hivyo Isaya mwana wa Amozi, akaja, na kumwambia, “Yahwe asema, 'Weka nyumba yako kwenye mpangilio; kwa kuwa utakufa, na hutapona.'”
2 そこでヒゼキヤは顔を壁に向けて主に祈って言った、
Kisha Ahazi akageuza uso wake kwenye ukuta na kumuomba Yahwe, akisema,
3 「ああ主よ、わたしが真実を真心をもってあなたの前に歩み、あなたの目にかなうことをおこなったのをどうぞ思い起してください」。そしてヒゼキヤは激しく泣いた。
“Tafadhali, Yahwe, ukumbuke jinsi nilivyo mwaminifu kutembea mbele yako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya yaliyo mazuri usoni kwako.” Kisha Hezekia akalia kwa sauti.
4 イザヤがまだ中庭を出ないうちに主の言葉が彼に臨んだ、
Kabla ya Isaya hajatoka nje kwenye mji wa kati, neno la Yahwe likamjia, kusema,
5 「引き返して、わたしの民の君ヒゼキヤに言いなさい、『あなたの父ダビデの神、主はこう仰せられる、わたしはあなたの祈を聞き、あなたの涙を見た。見よ、わたしはあなたをいやす。三日目にはあなたは主の宮に上るであろう。
'“Rudi, na umwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, 'Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yako, asemavyo: “Nimesikia maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Nitakuponya katika siku ya tatu, na utapanda juu kwenye nyumba ya Yahwe.
6 かつ、わたしはあなたのよわいを十五年増す。わたしはあなたと、この町とをアッスリヤの王の手から救い、わたしの名のため、またわたしのしもべダビデのためにこの町を守るであろう』」。
Nitakuongeza miaka kumi na tano ya maisha yako, na nitakulinda na huu mji kwa ajili yangu na kwa ajili ya mtumishi wangu."”'
7 そしてイザヤは言った、「干しいちじくのひとかたまりを持ってきて、それを腫物につけさせなさい。そうすれば直るでしょう」。
Hivyo Isaya akasema, “Chukueni mkate wa tini.” Walifanya hivyo na kuweka kwenye jipu lake, na akapona.
8 ヒゼキヤはイザヤに言った、「主がわたしをいやされる事と、三日目にわたしが主の家に上ることについて、どんなしるしがありましょうか」。
Hezekia akamwambia Isaya, “Je kutakuwa na alama gani ambayo Yahwe ataniponya, na kwamba nitapanda juu hadi kwenye hekalu la Yahwe katika siku ya tatu?”
9 イザヤは言った、「主が約束されたことを行われることについては、主からこのしるしを得られるでしょう。すなわち日影が十度進むか、あるいは十度退くかです」。
Isaya akajibu, “Hii ndiyo itakuwa ishara kwako kutoka kwa Yahwe, kwamba Yahwe atafanya kitu amacho alichokisema. Je kivuli kitaenda mbele hatua saba, au kurudi nyuma hatua saba?”
10 ヒゼキヤは答えた、「日影が十度進むことはたやすい事です。むしろ日影を十度退かせてください」。
Hezekia akajibu, “Ni kitu chepesi kwa kivuli kwenda mbele hatua kumi. Hapana, hicho kivuli kirudi nyuma hatua kumi.”
11 そこで預言者イザヤが主に呼ばわると、アハズの日時計の上に進んだ日影を、十度退かせられた。
Hivyo Isaya nabii akamlilia Yahwe, na akaleta kivuli hatua kumi nyuma, kutoka pale ambapo zilikuwa zimevuka kwenye ngazi za Ahazi.
12 そのころ、バラダンの子であるバビロンの王メロダクバラダンは、手紙と贈り物を持たせて使節をヒゼキヤにつかわした。これはヒゼキヤが病んでいることを聞いたからである。
Katika kipindi hicho Merodak Baladani mfalme wa Babeli alituma barua na zawadi kwa Hezekia, kwa kuwa alisikia kwamba Hezekia alikuwa anaumwa.
13 ヒゼキヤは彼らを喜び迎えて、宝物の蔵、金銀、香料、貴重な油および武器倉、ならびにその倉庫にあるすべての物を彼らに見せた。家にある物も、国にある物も、ヒゼキヤが彼らに見せない物は一つもなかった。
Hezekia akasikiliza hizo barua, na kisha kuwaonyesha wajumbe sehemu zote na sehemu zake za thamani, fedha, dhahabu, manukato na marhamu na nyumba yenye ghala la silaha zake, na yote yaliyokutwa kwenye ghala za nyumba zake. Hapakuwa na kitu kwenye nyumba, wala kwenye ufalme wake wote, ambao Hezekia hakuwaonyesha.
14 その時、預言者イザヤはヒゼキヤ王のもとにきて言った、「あの人々は何を言いましたか。どこからきたのですか」。ヒゼキヤは言った、「彼らは遠い国から、バビロンからきたのです」。
Kisha Isaya akaja kwa Hezekia na kumuuliza, “Hawa watu walikuwa wanakwambiaje? Wanatokea wapi?” Hezekia aksema, “Wamekuja kutoka nchi ya mbali ya Babeli.
15 イザヤは言った、「彼らはあなたの家で何を見ましたか」。ヒゼキヤは答えて言った、「わたしの家にある物を皆見ました。わたしの倉庫のうちには、わたしが彼らに見せない物は一つもありません」。
Isaya akauliza, “Wameona nini kwenye nyumba yako?” Hezekia akajibu, “Wameona kila kitu kwenye nyumba yangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.”
16 そこでイザヤはヒゼキヤに言った、「主の言葉を聞きなさい、
Basi Isaya akamwambia Hezekia, “Sikiliza neno la Yahwe:
17 『主は言われる、見よ、すべてあなたの家にある物、および、あなたの先祖たちが今日までに積みたくわえた物の、バビロンに運び去られる日が来る。何も残るものはないであろう。
'Tazama siku zinakuja wakati kila kitu kwenye kwenye nyumba yako ya kifalme, vitu ambavyo babu zako walivitunza huko hadi leo, vitabebwa kwenda Babeli. Hakuna kitakachobakia, Yahwe asema.
18 また、あなたの身から出るあなたの子たちも連れ去られ、バビロンの王の宮殿で宦官となるであろう』」。
Watoto waliozaliwa na wewe, ambao umewazaa wewe mwenyewe-watawachukua mbali, na watakuwa matowashi kwenye nyumba ya kifalme ya mfalme wa Babeli.'”
19 ヒゼキヤはイザヤに言った、「あなたが言われた主の言葉は結構です」。彼は「せめて自分が世にあるあいだ、平和と安全があれば良いことではなかろうか」と思ったからである。
Hezekia akamwambia Isaya, “neno la Yahwe uliloliongea ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, Je sivyo ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?”
20 ヒゼキヤのその他の事績とその武勇および、彼が貯水池と水道を作って、町に水を引いた事は、ユダの王の歴代志の書にしるされているではないか。
Kama kwa mambo mengine yanamuhusu Hezekia, na ushujaa wake wote, na jinsi alivyotengeza bwawa la maji na mfereji, na kuleta maji kwenye mji-hayakuandikwa kwenye kitabu cha ya matukio ya wafalme wa Yuda?
21 ヒゼキヤはその先祖たちと共に眠って、その子マナセが代って王となった。
Hezekia akalala na babu zake, na Manase mwanae akawa mfalme katika sehemu yake.

< 列王記Ⅱ 20 >