< 歴代誌Ⅱ 8 >

1 ソロモンは二十年を経て、主の家と自分の家とを建て終った。
Ikawa karibu ya mwisho wa miaka ishirini, kipindi ambacho Selemani alikuwa ameijenga nyumba ya Yahwe na ya kwake mwenye,
2 またソロモンはヒラムから送られた町々を建て直して、そこにイスラエルの人々を住ませた。
kwamba Selemani akaiajenga miji ambayo Hiramu alikuwa amempa, na ndani yake akawaweka watu wa Israeli.
3 ソロモンはまたハマテ・ゾバを攻めて、これを取った。
Selemani akauavamia Hamathzoba, akaushinda.
4 彼はまた荒野にタデモルを建て、もろもろの倉の町をハマテに建てた。
Akaijenga Tadmori katika nyika, na miji yote ya hazina, ambayo aliijenga katika Hamathi.
5 また城壁、門、貫の木のある堅固な町、上ベテホロンと下ベテホロンを建てた。
Pia akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji iliyozungushiwa kwa ukuta, malango, na makomeo.
6 ソロモンはまたバアラテと自分のもっていたすべての倉の町と、すべての戦車の町と、騎兵の町、ならびにエルサレム、レバノンおよび自分の治める全地方に建てようと望んだものを、ことごとく建てた。
Akaujenga Baalathi na miji yote ya hazina aliyoimiliki, na miji yote kwa ajili ya magari yake na miji kwa ajili ya wapanda farasi wake, na chochote alichotamani kujenga kwa ajili ya starehe zake katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika nchi zote zilizokuwa chini ya utawala wake.
7 すべてイスラエルの子孫でないヘテびと、アモリびと、ペリジびと、ヒビびと、エブスびとの残った民、
Kuhusu watu wengine wote ambao walikuwa wamesalia wa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, Wayebusi, ambao hawakuwa wa Israeli,
8 その地にあって彼らのあとに残ったその子孫、すなわちイスラエルの子孫が滅ぼし尽さなかった民に、ソロモンは強制徴募をおこなって今日に及んでいる。
watoto wao ambao waliachwa baada yao katika nchi, ambaoa watu wa Israeli hawakuwaangamiza—Selemani akawafanyisha kazi kwa nguvu, ndivyo walivyo hata leo.
9 しかし、イスラエルの人々をソロモンはその工事のためには、ひとりも奴隷としなかった。彼らは兵士となり、将校となり、戦車と、騎兵の長となった。
Vile vile, Selemani hakuwafanyisha kazi kwa nguvu watu wa Israeli. Badala yake, wakawa wanajeshsi wake, maakida wake, wakuu wake, na maakida wa magari ya majeshi yake na wapanda farasi wake.
10 これらはソロモン王のおもな官吏で、二百五十人あり、民を治めた。
Pia hawa walikuwa wakuu wa wakuu wakisimamia wasimamizi waliokuwa wa mfalme Selemani, walikuwa 250, waliowasimamia watu walioifanya kazi.
11 ソロモンはパロの娘をダビデの町から連れ上って、彼女のために建てた家に入れて言った、「主の箱を迎えた所は神聖であるから、わたしの妻はイスラエルの王ダビデの家に住んではならない」。
Selemani akamleta binti Farao nje ya mji wa Daudi kwenye nyumba aaliyokuwa amemjengea, kwa maana alisema, “Mke wangu lazima asiishi kataika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu kila linapokuja sanduku la Yahwe ni takatifu”.
12 ソロモンは廊の前に築いておいた主の祭壇の上で主に燔祭をささげた。
Kisha Selemani akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu yake ambayo alikuwa ametengeza mbele ya ukumbi.
13 すなわちモーセの命令に従って、毎日定めのようにささげ、安息日、新月および年に三度の祭、すなわち種入れぬパンの祭、七週の祭、仮庵の祭にこれをささげた。
Akatoa sadaka kama ilivyohitaka katika ratiba ya kila siku; akazitoa, kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa katika amari ya Musa, katika siku za Sabato, miezi mipya, na katika siku zilizopangwa mara tatu kila mwaka: Sikukuu ya mikate isiyochachwa, sikukuu ya majuma, na sikuku ya vibanda.
14 ソロモンは、その父ダビデのおきてに従って、祭司の組を定めてその職に任じ、またレビびとをその勤めに任じて、毎日定めのように祭司の前でさんびと奉仕をさせ、また門を守る者に、その組にしたがって、もろもろの門を守らせた。これは神の人ダビデがこのように命じたからである。
Katika kuyatunza maagizo ya baba yake Daudi, Selemani akayapanga makundi ya makuhani kwenye kazi yao, na Walawi kwenye nafasi zao, ili kumsisfu Mungu na kuhudumu mbele za makuhani, kama ilivyotakiwa katika ratiba ya kila siku. Pia akawateua walinda lango kwa zamu zao kwa kila lango, kwa maana Daudi, mtu wa Mungu, alikuwa ameagiza hivyo pia.
15 祭司とレビびとはすべての事につき、また倉の事について、王の命令にそむかなかった。
Watu hawa hawakupotea kutoka kwenye amri ya mfalme kwa makuhani na Walawi kuhusu jambo lolote, au kuhusu vyumba vya hazina.
16 このようにソロモンは、主の宮の基をすえた日からこれをなし終えたときまで、その工事の準備をことごとくなしたので、主の宮は完成した。
Kazi yote aliyoagizwa na Selemani ikakamilika, kutoka siku msingi wa nyumba ya Yahwe ulipowekwa hadi ilipokamilika. Nyumba ya Yahwe ikamalizika.
17 それからソロモンはエドムの地の海べにあるエジオン・ゲベルおよびエロテへ行った。
Kisha Selemani akaenda Esion geberi, na Elothi, juu ya pwani katika nchi ya Edomu.
18 時にヒラムはそのしもべどもの手によって船団を彼に送り、また海の事になれたしもべどもをつかわしたので、彼らはソロモンのしもべらと共にオフルへ行き、そこから金四百五十タラントを取って、これをソロモン王のもとに携えてきた。
Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri na Selemani na watumishi wa Semani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Selemani.

< 歴代誌Ⅱ 8 >