< 歴代誌Ⅰ 12 >

1 ダビデがキシの子サウルにしりぞけられて、なおチクラグにいた時、次の人々が彼のもとに来た。彼らはダビデを助けて戦った勇士たちのうちにあり、
Hawa walikuwa wanaume walio kuja kwa Daudi huko Zikilagi, wakati akiwa bado amefukuzwa katika uwepo wa Sauli mwana wa Kishi. Walikuwa miongoni mwa wanajeshi, wasaidizi wake katika mapambano.
2 弓をよくする者、左右いずれの手をもってもよく矢を射、石を投げる者で、ともにベニヤミンびとで、サウルの同族である。
Walikuwa wana upinde na waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto kurusha mawe na manati na kupiga mishale kutoka kwenye upinde. Walikuwa Wabenjamini, ndugu wa kabila moja na Sauli.
3 そのかしらはアヒエゼル、次はヨアシで、ともにギベア出身のシマアの子たちである。またエジエルとペレテで、ともにアズマウテの子たちである。またベラカおよびアナトテ出身のエヒウ。
Kiongozi alikuwa Ahi Eza, halafu Yoashi, Wana wote wa Shemaa Mgibeathi. Kulikuwa na Yezieli na Peleti, wana wa Azimavethi. Kulikuwa pia na Beraka, Yehu Waanathothi,
4 またギベオン出身のイシマヤ、彼は三十人のうちの勇士で、その三十人の長である。またエレミヤ、ヤハジエル、ヨハナン、ゲデラ出身のヨザバデ、
Ishimaia Mgibeoni, mwanajeshi kati ya wale thelathini ( na kiongozi wa wale thelathini); Yeremia, Yahazieli, Yohana, Yozabadi Wagederathi,
5 エルザイ、エリモテ、ベアリヤ、シマリヤ、ハリフびとシパテヤ、
Eluzai, Yerimothi, Bealia, Shemaria, Shefatia Waharufi,
6 エルカナ、イシア、アザリエル、ヨエゼル、ヤショベアムで、これらはコラびとである。
Wakorahi ni Elkana, Ishia, Azareli, Yoeza, Yashobeamu, na
7 またゲドルのエロハムの子たちであるヨエラおよびゼバデヤである。
Yoela na Zebadia, wana wa Yeroham wa Gedori.
8 ガドびとのうちから荒野の要害に来て、ダビデについた者は皆勇士で、よく戦う軍人、よく盾とやりをつかう者、その顔はししの顔のようで、その速いことは山にいるしかのようであった。
Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa wanaume wapiganaji, waliofundishwa kwa mapambano, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesi kwenye milima kama swala.
9 彼らのかしらはエゼル、次はオバデヤ、第三はエリアブ、
Kulikuwa na Eza kiongozi, Obadia wapili, Eliabu watatu,
10 第四はミシマンナ、第五はエレミヤ、
Mishimana wanne, Yeremia watano,
11 第六はアッタイ、第七はエリエル、
Atai wasita, Elieli wasaba,
12 第八はヨナハン、第九はエルザバデ、
Yohana wanane, Elizabadi watisa,
13 第十はエレミヤ、第十一はマクバナイである。
Yeremia wakumi, Makibanai wakumi na moja.
14 これらはガドの子孫で軍勢の長たる者、その最も小さい者でも百人に当り、その最も大いなる者は千人に当った。
Wana wa Gadi walikuwa viongozi wa jeshi. Wamwisho aliongoza mia moja, na mkubwa aliongoza elfu moja.
15 正月、ヨルダンがその全岸にあふれたとき、彼らはこれを渡って、谷々にいる者をことごとく東に西に逃げ走らせた。
Walikatisha Yordani kwa mwezi wa kwanza, wakati vijito vyake vilipofurika, na kuwafukuza wote wanaoishi katika mabonde, pande zote za mashariki na magharibi.
16 ベニヤミンとユダの子孫のうちの人々が要害に来て、ダビデについた。
Baadhi ya wanaume wa Benjamini na Yuda walikuja kwenye ngome kwa Daudi.
17 ダビデは出て彼らを迎えて言った、「あなたがたが好意をもって、わたしを助けるために来たのならば、わたしの心もあなたがたと、ひとつになりましょう。しかし、わたしの手になんの悪事もないのに、もしあなたがたが、わたしを欺いて、敵に渡すためであるならば、われわれの先祖の神がどうぞみそなわして、あなたがたを責められますように」。
Daudi alienda nje kuwasalimu na kuwahutubia: “kama mmekuja kwa amani kunisaidia, mnaweza kujiunga nami. Lakini kama mmekuja kunisaliti kwa maadui zangu, Ee Mungu wa mababu zetu awaone na kuwakemea, tangu sijafanya kosa.”
18 時に霊が三十人の長アマサイに臨み、アマサイは言った、「ダビデよ、われわれはあなたのもの。エッサイの子よ、われわれはあなたと共にある。平安あれ、あなたに平安あれ。あなたを助ける者に平安あれ。あなたの神があなたを助けられる」。そこでダビデは彼らを受けいれて部隊の長とした。
Kisha roho ikaja juu ya Amasai, ambaye alikuwa kiongozi wa wale thelathini. Amasai alisema, “Sisi ni wako, Daudi. Sisi tupo upande wako, mwana wa Yesse. na amani iwe juu ya yeyote atakaye kusaidia. Kuwa Mungu wako anakusaidia.” Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakuu wa watu wake.
19 さきにダビデがペリシテびとと共にサウルと戦おうと攻めて来たとき、マナセびと数人がダビデについた。(ただしダビデはついにペリシテびとを助けなかった。それはペリシテびとの君たちが相はかって、「彼はわれわれの首をとって、その主君サウルのもとに帰るであろう」と言って、彼を去らせたからである。)
Baadhi kutoka kwa Manase pia wakamwendea Daudi alipokuja na Wafilisti dhidi ya Sauli katika pambano. Lakini hawakuwasaidia Wafilisti kwasababu mabwana wa Wafilisti walishauriana na wakamfukuza Daudi. Walisema, “Atamwendea Bwana wake Sauli na kuhatarisha maisha yetu.”
20 ダビデがチクラグへ行ったとき、マナセびとアデナ、ヨザバデ、エデアエル、ミカエル、ヨザバデ、エリウ、ヂルタイが彼についた。皆マナセびとの千人の長であった。
Alipokwenda kwa Zikilagi, wanaume wa Manase walioungana nae walikuwa Adina, Yozabadi, Yediaeli, Yozabadi, Elihu, na Zilethai, viongozi wa maelfu wa Manase.
21 彼らはダビデを助けて敵軍に当った。彼らは皆大勇士で軍勢の長であった。
Walimsaidia Daudi kupigana na kikundi cha wezi, maana walikuwa wanaume wa mapambano. Baadae walikuwa wakuu katika jeshi.
22 ダビデを助ける者が日に日に加わって、ついに大軍となり、神の軍勢のようになった。
Siku hadi siku, wanaume walikuja kwa Daudi kumsaidia, mpaka wakawa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
23 主の言葉に従い、サウルの国をダビデに与えようとして、ヘブロンにいるダビデのもとに来た武装した軍隊の数は、次のとおりである。
Hii ni kumbukumbu ya wanajeshi wa vita, walio kuja kwa Daudi Hebroni, kuupindua ufalme wa Sauli kwake, ilikutimiza neno la Yahweh.
24 ユダの子孫で盾とやりをとり、武装した者六千八百人、
Kutoka Yuda walio beba ngao na mkuki ni 6, 800, tayari kwa vita.
25 シメオンの子孫で、よく戦う勇士七千百人、
Kutoka kwa Wasimeoni walikuwa 7, 100 wanaume wa mapambano.
26 レビの子孫からは四千六百人。
Kutoka kwa Walawi kulikuwa na wanaume wa mapambano 4, 600.
27 エホヤダはアロンの家のつかさで、彼に属する者は三千七百人。
Yehoiada alikuwa kiongozi wa uzao wa Aruni, na kwa yeye walikuwa 3, 700.
28 ザドクは年若い勇士で、彼の氏族から出た将軍は二十二人。
Kwa Zadoki, kijana, mwenye nguvu, na mjasiri, walikuwa viongozi ishirini na mbili kwa familia ya baba yake.
29 サウルの同族、ベニヤミンの子孫からは三千人、ベニヤミンびとの多くはなおサウルの家に忠義をつくしていた。
Kutoka kwa Benjamini, kabila la Sauli, walikuwa elfu tatu. Wengi wao walibaki waaminifu kwa Sauli mpaka muda huu.
30 エフライムの子孫からは二万八百人、皆勇士で、その氏族の名ある人々であった。
Kutoka kwa Waefraimu palikuwa na wanume wa mapambano 20, 800, wanaume maharufu kwenye familia za baba zao.
31 マナセの半部族からは一万八千人、皆ダビデを王に立てようとして上って来て、名をつらねた者である。
Kutoka kabila nusu la Manase palikuwa na wanaume elfu kumi na nane maharufu walio kuja kufanya Daudi mfalme.
32 イッサカルの子孫からはよく時勢に通じ、イスラエルのなすべきことをわきまえた人々が来た。その長たる者が二百人あって、その兄弟たちは皆その指揮に従った。
Kutoka kwa Isakari, palikuwa na viongozi mia mbili walio kuwa na ufahamu wa nyakati na walijua nini Israeli ya paswa kufanya. Ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
33 ゼブルンからは五万人、皆訓練を経た軍隊で、もろもろの武具で身をよろい、一心にダビデを助けた者である。
Kutoka Zebuloni palikuwa na wanaume elfu hamsini wa mapambano, tayari kwa vita, na silaha zote za vita, na tayari kutoa uwaminifu usio pungua.
34 ナフタリからは将たる者一千人および盾とやりをとってこれに従う者三万七千人。
Kutoka kwa Naftali palikuwa na askari elfu moja, na pamoja nao wanaume elfu thelathini na saba wenye ngao na mikuki.
35 ダンびとからは武装した者二万八千六百人。
Kutoka kwa Wadani palikuwa na wanaume 28, 600 wameandaliwa kwa ajili ya pambano.
36 アセルからは戦いの備えをした熟練の者四万人。
Kutoka kwa Asheri palikuwa na wanaume elfu arobaini wameandaliwa kwa pambano.
37 またヨルダンのかなたルベンびと、ガドびと、マナセの半部族からはもろもろの武具で身をよろった者十二万人であった。
Kutoka upande wa pili wa Yordani, kutoka kwa Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase, palikuwa na wanaume 120, 000 wameandaliwa na silaha za kila namna kwa ajili ya pambano.
38 すべてこれらの戦いの備えをしたいくさびとらは真心をもってヘブロンに来て、ダビデを全イスラエルの王にしようとした。このほかのイスラエルびともまた、心をひとつにしてダビデを王にしようとした。
Wanajeshi hawa wote, waliandaliwa kwa pambano, kuja Hebroni kwa dhumuni maalumu la kumfanya Daudi mfalme wa Israeli yote. Israeli yote ilikubaliana na kumfanya Daudi mfalme.
39 彼らはヘブロンにダビデとともに三日いて、食い飲みした。その兄弟たちは彼らのために備えをしたからである。
Walikuwa na Daudi siku tatu, kula na kunywa, kwa kuwa ndugu zao waliwapa mahitaji ya kwenda nayo.
40 また彼らに近い人々はイッサカル、ゼブルン、ナフタリなどの遠い所の者まで、ろば、らくだ、騾馬、牛などに食物を負わせて来た。すなわち麦粉の食物、干いちじく、干ぶどう、ぶどう酒、油、牛、羊などを多く携えて来た。これはイスラエルに喜びがあったからである。
Kwa kuongezea, wao walio kuwa karibu nao, kwa umbali wa Isakari na Zebuloni na Naftali, walileta mkate kwa punda, ngamia, ng'ombe, na keki, mvinyo, mafuta, ng'ombe, na kondoo, kwa kuwa Israeli walikuwa wana sherehekea

< 歴代誌Ⅰ 12 >