< תהילים 69 >

למנצח על-שושנים לדוד ב הושיעני אלהים-- כי באו מים עד-נפש 1
Uniokoe, Mungu; maana maji yameweka uhai wangu hatarini.
טבעתי ביון מצולה-- ואין מעמד באתי במעמקי-מים ושבלת שטפתני 2
Ninazama kwenye kina cha matope, pasipo na hahari pa kusimama; nimekuja kwenye kina kirefu cha maji, ambako mafuriko yananifunika.
יגעתי בקראי נחר גרוני כלו עיני--מיחל לאלהי 3
Nimechoka sana kwa kulia kwangu; koo langu ni kavu; macho yangu yanafifia wakati namngoja Mungu wangu.
רבו משערות ראשי-- שנאי חנם עצמו מצמיתי איבי שקר-- אשר לא-גזלתי אז אשיב 4
Wale wanichukiao bila sababu wako zaidi ya nywele za kichwa changu; wale ambao wangeweza kuniua, wakiwa adui zangu kwa sababu zisizo sahihi, ni wengi mno; wanalazimisha nirudishe kile ambacho sijaiba.
אלהים--אתה ידעת לאולתי ואשמותי ממך לא-נכחדו 5
Mungu, wewe unaujua ujinga wangu, na dhambi zangu hazifichiki kwako.
אל-יבשו בי קויך-- אדני יהוה צבאות אל-יכלמו בי מבקשיך-- אלהי ישראל 6
Usiwaache wale wanao kungoja wewe waaibishwe kwa sababu yangu, Bwana Yahwe wa majeshi; usiwaache wale wanaokutafuta wewe wadharauliwe kwa sababu yangu, Mungu wa Israeli.
כי-עליך נשאתי חרפה כסתה כלמה פני 7
Kwa ajili yako nimestahimili lawama; aibu imeufunika uso wangu.
מוזר הייתי לאחי ונכרי לבני אמי 8
Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, nisiye fahamika wala kuaminika kwa watoto wa mama yangu.
כי-קנאת ביתך אכלתני וחרפות חורפיך נפלו עלי 9
Kwa maana bidii ya nyumba yako imenila, na laumu zao wanao kulaumu wewe zimeniangukia mimi.
ואבכה בצום נפשי ותהי לחרפות לי 10
Wakati nilipolia na kutokula chakula, walinitukana.
ואתנה לבושי שק ואהי להם למשל 11
Nilipoteneneza mavazi ya gunia, nikawa kituko kwao.
ישיחו בי ישבי שער ונגינות שותי שכר 12
Wale wakaao katika lango la mji huniseng'enya; mimi ni wimbo wa walevi.
ואני תפלתי-לך יהוה עת רצון-- אלהים ברב-חסדך ענני באמת ישעך 13
Lakini kwangu mimi, maombi yangu ni kwako, Yahwe, wakati ambao wewe utayapokea; unijibu katika uaminifu wa wokovu wako.
הצילני מטיט ואל-אטבעה אנצלה משנאי וממעמקי מים 14
Unitoe matopeni, na usiniache nizame; uniondoe mbali na wale wanaonichukia na uniokoe katika kina cha maji.
אל-תשטפני שבלת מים-- ואל-תבלעני מצולה ואל-תאטר-עלי באר פיה 15
Usiache mafuliko ya maji yanielemee, wala kina kisinimeze. Usiache mdomo wa shimo unimeze.
ענני יהוה כי-טוב חסדך כרב רחמיך פנה אלי 16
Unijibu, Yahwe, maana uaminifu wa agano lako ni mwema; kwa maana rehema zako kwangu ni nyingi, unigeukie.
ואל-תסתר פניך מעבדך כי-צר-לי מהר ענני 17
Usiufiche uso wako mbali na mtumishi wako, maana niko katika dhiki; unijibu haraka.
קרבה אל-נפשי גאלה למען איבי פדני 18
Uje kwangu na unikomboe. Kwa sababu ya adui zangu, uwe fidia yangu.
אתה ידעת--חרפתי ובשתי וכלמתי נגדך כל-צוררי 19
Wewe wajua kulaumiwa kwangu, kuaibishwa kwangu, na kudharauliwa kwangu; wapinzani wangu wote wako mbele yako.
חרפה שברה לבי-- ואנושה ואקוה לנוד ואין ולמנחמים ולא מצאתי 20
Lawama imevunja moyo wangu; nimejawa na huzuni kubwa; nilitafuta mtu wa kunihurumia, lakini hakuwepo; nilitafuta wafariji, lakini sikupata.
ויתנו בברותי ראש ולצמאי ישקוני חמץ 21
Walinipa sumu kwa ajili ya chakula changu; katika kiu yangu walinipa siki ninywe.
יהי-שלחנם לפניהם לפח ולשלומים למוקש 22
Meza yao mbele yao na iwe mtego; wafikiripo wako kwenye usalama, iwe kitanzi.
תחשכנה עיניהם מראות ומתניהם תמיד המעד 23
Macho yao na yatiwe giza ili kwamba wasiweze kuona; uvifanye viuno vyao kutetemeka daima.
שפך-עליהם זעמך וחרון אפך ישיגם 24
Wamwagie gadhabu yako, ukali wa hasira yako uwafikie wao.
תהי-טירתם נשמה באהליהם אל-יהי ישב 25
Sehemu yao na iwe ukiwa; mtu yeyote asiishi katika hema yao.
כי-אתה אשר-הכית רדפו ואל-מכאוב חלליך יספרו 26
Kwa kuwa walimtesa yule uliyempa adhabu. Mara kwa mara walihesabu maumivu ya wale walioumizwa.
תנה-עון על-עונם ואל-יבאו בצדקתך 27
Wakiwashtaki kuwa wamefanya uovu juu ya uovu; usiwaache waje kwenye ushindi wa haki yako.
ימחו מספר חיים ועם צדיקים אל-יכתבו 28
Uwafute kwenye Kitabu cha Uzima na wasiandikwe pamoja na wenyehaki.
ואני עני וכואב ישועתך אלהים תשגבני 29
Lakini mimi ni maskini na mwenye huzuni; uruhusu wokovu wako, Mungu, uniweke juu sana.
אהללה שם-אלהים בשיר ואגדלנו בתודה 30
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo na nitamtukuza yeye kwa shukrani.
ותיטב ליהוה משור פר מקרן מפריס 31
Nitamsifu Yahwe zaidi kuliko ng'ombe au ndama aliye na mapembe na kwato.
ראו ענוים ישמחו דרשי אלהים ויחי לבבכם 32
Wanyenyekevu wameona na kufurahi; ninyi mnao matafuta Mungu, mioyo yenu itiwe nguvu.
כי-שמע אל-אביונים יהוה ואת-אסיריו לא בזה 33
Maana Yahwe husikia wenye uhitaji naye hawadharau wafungwa wake.
יהללוהו שמים וארץ ימים וכל-רמש בם 34
Mbingu na nchi zimsifu yeye, bahari na vyote vitembeavyo majini.
כי אלהים יושיע ציון ויבנה ערי יהודה וישבו שם וירשוה 35
Kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na ataujenga tena mji wa Yuda; watu wataishi huko na kupata umiliki wao.
וזרע עבדיו ינחלוה ואהבי שמו ישכנו-בה 36
Ukoo wa watumishi wake watairithi; nao walipendao jina lake wataishi humo.

< תהילים 69 >