< תהילים 45 >

למנצח על-ששנים לבני-קרח משכיל שיר ידידת ב רחש לבי דבר טוב-- אמר אני מעשי למלך לשוני עט סופר מהיר 1
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi.” Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi. Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.
יפיפית מבני אדם-- הוצק חן בשפתותיך על-כן ברכך אלהים לעולם 2
Wewe ni bora kuliko watu wengine wote na midomo yako imepakwa neema, kwa kuwa Mungu amekubariki milele.
חגור-חרבך על-ירך גבור-- הודך והדרך 3
Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, jivike fahari na utukufu.
והדרך צלח רכב-- על-דבר-אמת וענוה-צדק ותורך נוראות ימינך 4
Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi, kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki, mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha.
חציך שנונים עמים תחתיך יפלו בלב אויבי המלך 5
Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme, mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako.
כסאך אלהים עולם ועד שבט מישר שבט מלכותך 6
Ee Mungu, kiti chako cha enzi kitadumu milele na milele, fimbo ya utawala wa haki itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.
אהבת צדק ותשנא-רשע על-כן משחך אלהים אלהיך שמן ששון-- מחברך 7
Unaipenda haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako, kwa kukupaka mafuta ya furaha.
מר-ואהלות קציעות כל-בגדתיך מן-היכלי שן מני שמחוך 8
Mavazi yako yote yana harufu nzuri ya manemane, udi na mdalasini; kutoka kwenye majumba ya kifalme yaliyopambwa kwa pembe za ndovu, sauti za vinanda vya nyuzi zinakufanya ufurahi.
בנות מלכים ביקרותיך נצבה שגל לימינך בכתם אופיר 9
Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa; kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri.
שמעי-בת וראי והטי אזנך ושכחי עמך ובית אביך 10
Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio: Sahau watu wako na nyumba ya baba yako.
ויתאו המלך יפיך כי-הוא אדניך והשתחוי-לו 11
Mfalme ameshangazwa na uzuri wako; mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako.
ובת-צר במנחה פניך יחלו--עשירי עם 12
Binti wa Tiro atakuletea zawadi, watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako.
כל-כבודה בת-מלך פנימה ממשבצות זהב לבושה 13
Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake; vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.
לרקמות תובל למלך בתולות אחריה רעותיה--מובאות לך 14
Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, mabikira wenzake wanamfuata na wanaletwa kwako.
תובלנה בשמחת וגיל תבאינה בהיכל מלך 15
Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, na kuingia katika jumba la mfalme.
תחת אבתיך יהיו בניך תשיתמו לשרים בכל-הארץ 16
Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, mtawafanya wakuu katika nchi yote.
אזכירה שמך בכל-דר ודר על-כן עמים יהודוך לעלם ועד 17
Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote, kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele.

< תהילים 45 >