< איוב 7 >

הלא-צבא לאנוש על- (עלי-) ארץ וכימי שכיר ימיו 1
Je mtu hana kazi ngumu juu ya nchi? Je siku zake si kama siku za mwajiriwa?
כעבד ישאף-צל וכשכיר יקוה פעלו 2
Kama mtumwa atamaniye sana kivuli cha jioni, kama mwajiriwa atafutaye ujira wake -
כן הנחלתי לי ירחי-שוא ולילות עמל מנו-לי 3
hivyo nami nimeumbwa kuvumilia miezi ya taabu; Nami nimepewa taabu - zimeujaza usiku.
אם-שכבתי-- ואמרתי מתי אקום ומדד-ערב ושבעתי נדדים עדי-נשף 4
Hapo nilalapo chini, najiuliza mwenyewe, 'Lini nitatoka kitandani na lini usiku utatoweka?' Nimejawa na kujitupa huku na huko hadi mwanzo wa siku.
לבש בשרי רמה וגיש (וגוש) עפר עורי רגע וימאס 5
Mwili wangu umevikwa minyoo na madonda yenye vumbi; maumivu katika ngozi yangu yamekuwa magumu na kisha hutoweka na huendelea tena.
ימי קלו מני-ארג ויכלו באפס תקוה 6
Siku zangu zinakimbia kuliko chombo cha kufumia; zinapita bila tumaini.
זכר כי-רוח חיי לא-תשוב עיני לראות טוב 7
Mungu, anakumbuka kwamba maisha yangu ni pumzi tu; jicho langu halitaona mema tena.
לא-תשורני עין ראי עיניך בי ואינני 8
Jicho lake Mungu, huyo anionaye mimi, halitaniangalia tena; Macho ya Mungu yatanitazama, lakini sitakuwako.
כלה ענן וילך כן יורד שאול לא יעלה (Sheol h7585) 9
kama vile wingu liishavyo na kutoweka, hivyo wale waendao sheoli hawatarudi tena kabisa. (Sheol h7585)
לא-ישוב עוד לביתו ולא-יכירנו עוד מקמו 10
Yeye hatarudi tena nyumbani kwake, wala mahali pake hapatamtambua tena.
גם-אני לא אחשך-פי אדברה בצר רוחי אשיחה במר נפשי 11
Kwa sababu hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitasema juu ya maumivu makubwa ya roho yangu; Nitanung'unika juu ya uchungu wa nafsi yangu.
הים-אני אם-תנין כי-תשים עלי משמר 12
Je mimi ni bahari au kiumbe cha kutisha baharini hata ukaweka mlinzi juu yangu?
כי-אמרתי תנחמני ערשי ישא בשיחי משכבי 13
Hapo nisemapo, 'kitanda changu kitanifariji, na malazi yangu yatatuliza manung'uniko yangu,'
וחתתני בחלמות ומחזינות תבעתני 14
halafu unitishapo kwa ndoto na kunitisha kwa maono,
ותבחר מחנק נפשי מות מעצמותי 15
ili nichague kunyongwa na kufa kuliko kulinda mifupa yangu hii.
מאסתי לא-לעלם אחיה חדל ממני כי-הבל ימי 16
Ninayachukia kabisa maisha yangu; sitamani siku zote kuwa hai; usinisumbue maana siku zangu hazifai.
מה-אנוש כי תגדלנו וכי-תשית אליו לבך 17
Je mtu ni nini hata ukatia bidii kwake, na ukaweka akili yako kwake,
ותפקדנו לבקרים לרגעים תבחננו 18
na kumwangalia kila asubuhi, na kumjaribu kila mara?
כמה לא-תשעה ממני לא-תרפני עד-בלעי רקי 19
Je itachukuwa muda gani kabla hujaacha kuniangalia, wala kunisumbua muda wa kutosha kwaajili ya kumeza mate yangu?
חטאתי מה אפעל לך-- נצר האדם למה שמתני למפגע לך ואהיה עלי למשא 20
Hata kama nimefanya dhambi, itakusaidia nini, wewe ulindaye wanadamu? Kwa nini umenifanya shabaha yako, kiasi kwamba nimekuwa mzigo kwako?
ומה לא-תשא פשעי-- ותעביר את-עוני כי-עתה לעפר אשכב ושחרתני ואינני 21
Kwa nini hunisamehi makosa yangu na kuniondolea uovu wangu? kwa kuwa sasa nitalala mavumbini; na wewe utanitafuta kwa bidii, lakini sitakuwako.”

< איוב 7 >