< בראשית 49 >

ויקרא יעקב אל בניו ויאמר האספו ואגידה לכם את אשר יקרא אתכם באחרית הימים 1
Kisha Yakobo akawaita wana wake, na kusema: “Jikusanyeni pamoja, ili niwaambie yatakayowapata nyakati zijazo.
הקבצו ושמעו בני יעקב ושמעו אל ישראל אביכם 2
Kusanyikeni ninyi wenyewe na msikilize, enyi wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu.
ראובן בכרי אתה כחי וראשית אוני--יתר שאת ויתר עז 3
Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa uwezo wangu, aliyesalia katika heshima na nguvu.
פחז כמים אל תותר כי עלית משכבי אביך אז חללת יצועי עלה 4
Asiyezuilika kama maji yarukayo, hautakuwa na umaharufu, kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulikipanda kwa kuvizia.
שמעון ולוי אחים--כלי חמס מכרתיהם 5
Simoni na Lawi ni ndugu. Panga zao ni silaha za vurugu.
בסדם אל תבא נפשי בקהלם אל תחד כבדי כי באפם הרגו איש וברצנם עקרו שור 6
Ee nafsi yangu, usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao, kwani moyo wangu unaheshima kubwa kwa ajili yao. Kwani katika hasira yao waliua watu. Iliwapendeza kuwakata visigino ng'ombe.
ארור אפם כי עז ועברתם כי קשתה אחלקם ביעקב ואפיצם בישראל 7
Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili. Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli.
יהודה אתה יודוך אחיך--ידך בערף איביך ישתחוו לך בני אביך 8
Yuda, ndugu zako watakusifu. Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watainama mbele zako
גור אריה יהודה מטרף בני עלית כרע רבץ כאריה וכלביא מי יקימנו 9
Yuda ni mwana simba. Mwanangu, umetoka katika mawindo yako. Alisimama chini, alijikunyata kama simba, kama simba jike. Je nana atakayejaribu kumwamsha?
לא יסור שבט מיהודה ומחקק מבין רגליו עד כי יבא שילה ולו יקהת עמים 10
Fimbo haitaondoka katika Yuda, wala fimbo ya utawala kutoka katika miguu yake, hata atakapo kuja Shilo. Mataifa yatamtii.
אסרי לגפן עירה ולשרקה בני אתנו כבס ביין לבשו ובדם ענבים סותה 11
Kumfunga punda wake kwenye mzabibu, na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri, amefua mavazi yake katika divai, na kanzu yake katika damu ya vichala vya mzabibu.
חכלילי עינים מיין ולבן שנים מחלב 12
Macho yake yatakuwa mausi kama mvinyo, na meno yake meupe kama maziwa.
זבולן לחוף ימים ישכן והוא לחוף אנית וירכתו על צידן 13
Zabuloni atakaa katika fukwe ya bahari. Atakuwa bandari kwa ajili ya meli, na mpaka wake utakuwa hata Sidoni.
יששכר חמר גרם--רבץ בין המשפתים 14
Isakari ni punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya kondoo.
וירא מנחה כי טוב ואת הארץ כי נעמה ויט שכמו לסבל ויהי למס עבד 15
Anaona mahali pazuri pa kupumzikia na nchi ya kupendeza. Atainamisha bega lake kwa mzigo na kuwa mtumishi wake.
דן ידין עמו--כאחד שבטי ישראל 16
Dani atawaamua watu wake kama mojawapo ya makabila ya Israeli.
יהי דן נחש עלי דרך שפיפן עלי ארח--הנשך עקבי סוס ויפל רכבו אחור 17
Dani atakuwa nyoka kando ya njia, nyoka mwenye sumu aumaye visigino vya farasi katika njia, hivyo aongozaye farasi huanguka nyuma.
לישועתך קויתי יהוה 18
Ninaungoja wokovu wako, Yahwe.
גד גדוד יגודנו והוא יגד עקב 19
Gadi - wapanda farasi watamshambulia, lakini yeye atawapiga katika visigino vyao.
מאשר שמנה לחמו והוא יתן מעדני מלך 20
Vyakula vya Asheri vitakuwa vingi, naye ataandaa vyakula vya kifalme.
נפתלי אילה שלחה--הנתן אמרי שפר 21
Naftali ni dubu jike asiyefungwa; atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri.
בן פרת יוסף בן פרת עלי עין בנות צעדה עלי שור 22
Yusufu ni tawi lizaalo, tawi lizaalo karibu na kijito, ambaye matawi yake yako juu wa ukuta.
וימררהו ורבו וישטמהו בעלי חצים 23
Mpiga mishale atamshambulia na kumrushia na kumsumbua.
ותשב באיתן קשתו ויפזו זרעי ידיו מידי אביר יעקב משם רעה אבן ישראל 24
Lakini upinde wake utakuwa imara, na mikono yake itakuwa hodari kwa sababu ya mikono ya Mwenyenguvu wa Yakobo, kwa ajili ya jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli.
מאל אביך ויעזרך ואת שדי ויברכך ברכת שמים מעל ברכת תהום רבצת תחת ברכת שדים ורחם 25
Mungu wa baba yako atakusaidia na Mungu Mwenye enzi atakubariki kwa baraka mbinguni juu, baraka za vilindi vilivyo chini, na baraka za maziwa na tumbo.
ברכת אביך גברו על ברכת הורי עד תאות גבעת עולם תהיין לראש יוסף ולקדקד נזיר אחיו 26
Baraka za baba yako ni kuu kuliko baraka za milima ya zamani au vitu vilivyotamaniwa vya milima ya kale. Na viwe katika kichwa cha Yusufu, hata juu ya taji ya kifalme kichwani pa ndugu zake.
בנימין זאב יטרף בבקר יאכל עד ולערב יחלק שלל 27
Benjamini ni mbwamwitu mwenye njaa. Wakati wa asubuhi atalarua mawindo, na jioni atagawa mateka.”
כל אלה שבטי ישראל שנים עשר וזאת אשר דבר להם אביהם ויברך אותם--איש אשר כברכתו ברך אתם 28
Haya ni makabila kumi na mbili ya Israeli. Hiki ndicho baba yao alichowambia alipowabariki. Aliwabariki kila mmoja kwa baraka iliyomstahili.
ויצו אותם ויאמר אלהם אני נאסף אל עמי--קברו אתי אל אבתי אל המערה--אשר בשדה עפרון החתי 29
Kisha akawaelekeza na kuwaambia, “Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti,
במערה אשר בשדה המכפלה אשר על פני ממרא--בארץ כנען אשר קנה אברהם את השדה מאת עפרן החתי--לאחזת קבר 30
katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia.
שמה קברו את אברהם ואת שרה אשתו שמה קברו את יצחק ואת רבקה אשתו ושמה קברתי את לאה 31
Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea.
מקנה השדה והמערה אשר בו מאת בני חת 32
Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi.”
ויכל יעקב לצות את בניו ויאסף רגליו אל המטה ויגוע ויאסף אל עמיו 33
Yakobo alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe, akaiweka miguu yake kitandani, akakata roho, akawaendea watu wake

< בראשית 49 >