< עמוס 9 >

ראיתי את אדני נצב על המזבח ויאמר הך הכפתור וירעשו הספים ובצעם בראש כלם ואחריתם בחרב אהרג לא ינוס להם נס ולא ימלט להם פליט 1
Nilimwona Bwana amesimama karibu na madhabahu, na akasema, “Vipige vichwa vya nguzo ili kwamba misingi itikisike. Vivunje vipande vipande juu ya vichwa vyao vyote, nami nitamwua kwa upanga wa mwisho wao. Hakuna hata mmoja wao atakaye kimbia, hakuna hata mmoja wao atakayekimbia.
אם יחתרו בשאול משם ידי תקחם ואם יעלו השמים--משם אורידם (Sheol h7585) 2
Hata kama watachimba kwenye Sheoli, kuna mkono wangu utawachukua. Hata kama watapanda juu kwenda mbingunu, huko nitawaleta chini. (Sheol h7585)
ואם יחבאו בראש הכרמל משם אחפש ולקחתים ואם יסתרו מנגד עיני בקרקע הים--משם אצוה את הנחש ונשכם 3
Hata kama watajificha juu ya Karmeli, nitawatafuta huko na kuwachukua. Hata kama watajificha kwenye vilindi vya bahari nisiwaone, nimwagiza joka, na atawang'ata.
ואם ילכו בשבי לפני איביהם משם אצוה את החרב והרגתם ושמתי עיני עליהם לרעה ולא לטובה 4
Hata kama wataenda kwenye utumwa, watabanwa na maadui zao mbele yao, nitauagiza upanga huko, na utawau. Nitaelekeza macho yangu juu yao kwa ubaya sio kwa uzuri.”
ואדני יהוה הצבאות הנוגע בארץ ותמוג ואבלו כל יושבי בה ועלתה כיאר כלה ושקעה כיאר מצרים 5
Bwana Mungu wa majeshi ndiye agusaye nchi na ikayeyuka; wote waishio humo wataomboleza; yote yatainuka kama Mto, na itadidimia tena kama mto wa Misri.
הבונה בשמים מעלותו ואגדתו על ארץ יסדה הקרא למי הים וישפכם על פני הארץ--יהוה שמו 6
Ni yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuanzisha kuba yake juu ya dunia. Yeye huita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa dunia, Yahwe ndiye jina lake.
הלוא כבני כשיים אתם לי בני ישראל נאם יהוה הלוא את ישראל העליתי מארץ מצרים ופלשתיים מכפתור וארם מקיר 7
“Je ninyi sio kama watu wa Kushi kwangu, wana wa Israeli? -hivi ndivyo Yahwe asemavyo. Je sikuwapandisha Israeli kutoka nchi ya misri, Wafilisti kutoka Krete, na Washami kutoka Kiri?
הנה עיני אדני יהוה בממלכה החטאה והשמדתי אתה מעל פני האדמה אפס כי לא השמיד אשמיד את בית יעקב--נאם יהוה 8
Tazama, macho ya Bwana Yahwe yako juu ya ufalme wenye dhambi, na nitauharibu kutoka kwenye uso wa dunia, isipokuwa kwamba sintoiharibu kabisa nyumba ya Yakobo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
כי הנה אנכי מצוה והנעותי בכל הגוים את בית ישראל כאשר ינוע בכברה ולא יפול צרור ארץ 9
Tazama, nitaamuru, na nitaipepeta nyumba ya Israeli miongoni mwa mataifa yote, kama mtu apepetaye ngano kwenye ungo, hivyo basi hakuna hata chembe ya jiwe itakayoanguka kwenye aridhi.
בחרב ימותו כל חטאי עמי האמרים לא תגיש ותקדים בעדינו--הרעה 10
Watenda dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, wale wasemao, 'Majanga hayatatupita au kukutana nasi.'
ביום ההוא אקים את סכת דויד הנפלת וגדרתי את פרציהן והרסתיו אקים ובניתיה כימי עולם 11
Katika siku hiyo nitainua hema ya Daudi iliyokuwa imeanguka, na kuyafunga matawi yake. Nitayainua magofu yake, na kuijenga tena kama katika siku za zamani,
למען יירשו את שארית אדום וכל הגוים אשר נקרא שמי עליהם נאם יהוה עשה זאת 12
Kwamba wamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote ambayo yameitwa kwa jina langu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo-afanyayo haya.
הנה ימים באים נאם יהוה ונגש חורש בקצר ודרך ענבים במשך הזרע והטיפו ההרים עסיס וכל הגבעות תתמוגגנה 13
Tazama, siku zitakuja-hivi ndivyo Yahwe asemavyo-wakati mlimaji atampita mvunaji, na akanyagaye zabibu atampita yeye apandaye mbegu. Milima itadondosha divai tamu, na milima yote itabubujika kwa nayo.
ושבתי את שבות עמי ישראל ובנו ערים נשמות וישבו ונטעו כרמים ושתו את יינם ועשו גנות ואכלו את פריהם 14
Nitawarudisha kutoka utumwani watu wangu Israeli. Watajenga magofu ya miji na kuishi humo, watapanda bustani za mizabibu na kunywa divai, na watafanya bustani na kula matunda yao.
ונטעתים על אדמתם ולא ינתשו עוד מעל אדמתם אשר נתתי להם--אמר יהוה אלהיך 15
Nitaipanda hadi kwenye nchi yao, na hawataing'oa tena kutoka kwenye nchi ambayo niliyowapatia,” asema Yahwe Mungu wako.

< עמוס 9 >