< Exodus 38 >

1 He made the altar of burnt offering of acacia wood. It was square. Its length was five cubits, its width was five cubits, and its height was three cubits.
Naye akafanya madhabahu ya toleo la kuteketezwa kwa mbao za mshita. Mikono mitano urefu wake, na mikono mitano upana wake, ilikuwa mraba, na mikono mitatu kimo chake.
2 He made its horns on its four corners. Its horns were of one piece with it, and he overlaid it with bronze.
Halafu akafanya pembe zake kwenye zile ncha zake nne. Pembe zake zilitoka kwake. Kisha akaifunika kwa shaba.
3 He made all the vessels of the altar: the pots, the shovels, the basins, the forks, and the fire pans. He made all its vessels of bronze.
Baada ya hilo akavifanya vyombo vyote vya madhabahu, yale makopo na zile sepetu na yale mabakuli, zile nyuma na vile vyetezo. Vyombo vyake vyote alivifanya kwa shaba.
4 He made for the altar a grating of a network of bronze, under the ledge around it beneath, reaching halfway up.
Tena akaifanyia madhabahu kiunzi cha fito, mtandao wa shaba, chini ya ukingo wake, chini kuelekea katikati yake.
5 He cast four rings for the four corners of bronze grating, to be places for the poles.
Halafu akatengeneza pete nne kwenye ile miisho minne karibu na kile kiunzi cha shaba, ili kuitegemeza ile miti.
6 He made the poles of acacia wood, and overlaid them with bronze.
Bezaleli akafanya miti ya mshita na kuifunika kwa shaba.
7 He put the poles into the rings on the sides of the altar, with which to carry it. He made it hollow with planks.
Kisha akaitia ile miti kwenye zile pete zilizo pande za madhabahu ili kuibeba. Akaifanya kuwa sanduku la mbao lenye uwazi.
8 He made the basin of bronze, and its base of bronze, out of the mirrors of the ministering women who ministered at the door of the Tent of Meeting.
Kisha akafanya beseni ya shaba na kinara chake cha shaba. Kwa kutumia vioo vya watumishi wanawake ambao walifanya utumishi uliopangwa kwenye mwingilio wa hema la mkutano.
9 He made the court: for the south side southward the hangings of the court were of fine twined linen, one hundred cubits;
Naye akafanya ule ua. Upande unaokabili Negebu, kuelekea kusini, mapazia ya ua yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa, kwa mikono mia moja.
10 their pillars were twenty, and their sockets twenty, of bronze; the hooks of the pillars and their fillets were of silver.
Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha
11 For the north side one hundred cubits, their pillars twenty, and their sockets twenty, of bronze; the hooks of the pillars, and their fillets, of silver.
Pia, kwa ajili ya upande wa kaskazini kulikuwa na mikono mia. Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha.
12 For the west side were hangings of fifty cubits, their pillars ten, and their sockets ten; the hooks of the pillars, and their fillets, of silver.
Lakini kwa ajili ya upande wa magharibi mapazia yalikuwa mikono hamsini. Nguzo zake zilikuwa kumi na vikalio vyake kumi. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha.
13 For the east side eastward fifty cubits,
Na kwa ajili ya upande wa mashariki kulikuwa na mikono hamsini.
14 the hangings for the one side were fifteen cubits; their pillars three, and their sockets three;
Mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano kwa upande mmoja. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu.
15 and so for the other side: on this hand and that hand by the gate of the court were hangings of fifteen cubits; their pillars three, and their sockets three.
Na kwa ajili ya upande ule mwingine, huu na ule, wa lango la ua, mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu.
16 All the hangings around the court were of fine twined linen.
Mapazia yote ya ua kuzunguka pande zote yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa.
17 The sockets for the pillars were of bronze. The hooks of the pillars and their fillets were of silver. Their capitals were overlaid with silver. All the pillars of the court had silver bands.
Navyo vikalio vya nguzo vilikuwa vya shaba. Vibanio vya vikalio na viungo vyake vilikuwa vya fedha navyo vilifunikwa kwa shaba sehemu ya juu, na kulikuwa na viungo vya shaba kwa ajili ya nguzo zote za ua.
18 The screen for the gate of the court was the work of the embroiderer, of blue, purple, scarlet, and fine twined linen. Twenty cubits was the length, and the height along the width was five cubits, like the hangings of the court.
Nacho kisitiri cha lango la ua kilikuwa na mikono ishirini urefu. Cha uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, na urefu wake ulikuwa mikono ishirini, nacho kimo kotekote kilikuwa mikono mitano sawasawa na mapazia ya ua.
19 Their pillars were four, and their sockets four, of bronze; their hooks of silver, and the overlaying of their capitals, and their fillets, of silver.
Na nguzo zake nne na vikalio vyake vinne vilikuwa vya shaba. Misumari yake ilikuwa ya fedha na utando wa vichwa vyake na viungo vyake ulikuwa wa fedha.
20 All the pins of the tabernacle, and around the court, were of bronze.
Na misumari yote ya hema kwa ajili ya maskani na kwa ajili ya ua kuzunguka pande zote ilikuwa ya shaba
21 These are the amounts of materials used for the tabernacle, even the Tabernacle of the Testimony, as they were counted, according to the commandment of Moses, for the service of the Levites, by the hand of Ithamar, the son of Aaron the priest.
Hivi ndivyo vitu vilivyohesabiwa vya maskani, maskani ya Ushuhuda, vilivyohesabiwa kwa amri ya Musa, kuwa utumishi wa Walawi chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa Aruni kuhani.
22 Bezalel the son of Uri, the son of Hur, of the tribe of Judah, made all that the LORD commanded Moses.
Naye Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huru wa kabila la Yuda alifanya yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa.
23 With him was Oholiab, the son of Ahisamach, of the tribe of Dan, an engraver, and a skillful workman, and an embroiderer in blue, in purple, in scarlet, and in fine linen.
Na pamoja naye alikuwa Oholiabu mwana wa Ahisamaki wa kabila la Dani, fundi na mtarizi na mfumaji wa uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora.
24 All the gold that was used for the work in all the work of the sanctuary, even the gold of the offering, was twenty-nine talents and seven hundred thirty shekels, according to the shekel of the sanctuary.
Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya kazi katika kazi yote ya mahali patakatifu ikawa jumla ya dhahabu ya toleo la kutikisa, talanta ishirini na tisa na shekeli 730 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.
25 The silver of those who were counted of the congregation was one hundred talents and one thousand seven hundred seventy-five shekels, according to the shekel of the sanctuary:
Nayo fedha ya wale walioandikishwa kati ya kusanyiko ilikuwa talanta mia moja na shekeli 1, 775 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,
26 a beka a head, that is, half a shekel, according to the shekel of the sanctuary, for everyone who passed over to those who were counted, from twenty years old and upward, for six hundred three thousand five hundred fifty men.
ile nusu shekeli kwa ajili ya mtu mmoja ilikuwa nusu shekeli kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, Kwa kila mtu aliyekuwa akipita kuingia upande wa wale waliokuwa wameandikishwa kuanzia miaka ishirini na zaidi, jumla ya watu 603, 550.
27 The one hundred talents of silver were for casting the sockets of the sanctuary and the sockets of the veil: one hundred sockets for the one hundred talents, one talent per socket.
Na talanta mia moja za fedha zilitumiwa kutengeneza vikalio vya mahali patakatifu na vikalio vya lile pazia. Vikalio mia moja vilitoshana na talanta mia moja, talanta moja kwa kikalio kimoja.
28 From the one thousand seven hundred seventy-five shekels he made hooks for the pillars, overlaid their capitals, and made fillets for them.
Na kutokana na zile shekeli 1, 775 alifanyiza vibanio vya nguzo na kuvifunika sehemu yake ya juu na kuviunganisha pamoja.
29 The bronze of the offering was seventy talents and two thousand four hundred shekels.
Nayo shaba ya toleo la kutikisa ilikuwa talanta sabini na shekeli 2, 400.
30 With this he made the sockets to the door of the Tent of Meeting, the bronze altar, the bronze grating for it, all the vessels of the altar,
Naye akaitumia kufanya vile vikalio vya mwingilio wa hema la mkutano na ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, na vyombo vyote vya madhabahu,
31 the sockets around the court, the sockets of the gate of the court, all the pins of the tabernacle, and all the pins around the court.
na vile vikalio vya ua kuzunguka pande zote, na vile vikalio vya lango la ua, na misumari yote ya maskani na misumari yote ya ua kuzunguka pande zote.

< Exodus 38 >