< Job 42 >

1 Then Job answered the LORD:
Ndipo Ayubu akamjibu Bwana:
2 “I know that you can do all things, and that no purpose of yours can be restrained.
“Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.
3 You asked, ‘Who is this who hides counsel without knowledge?’ therefore I have uttered that which I didn’t understand, things too wonderful for me, which I didn’t know.
Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.
4 You said, ‘Listen, now, and I will speak; I will question you, and you will answer me.’
“Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena; nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’
5 I had heard of you by the hearing of the ear, but now my eye sees you.
Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako, lakini sasa macho yangu yamekuona.
6 Therefore I abhor myself, and repent in dust and ashes.”
Kwa hiyo najidharau mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.”
7 It was so, that after the LORD had spoken these words to Job, the LORD said to Eliphaz the Temanite, “My wrath is kindled against you, and against your two friends; for you have not spoken of me the thing that is right, as my servant Job has.
Baada ya Bwana kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.
8 Now therefore, take to yourselves seven bulls and seven rams, and go to my servant Job, and offer up for yourselves a burnt offering; and my servant Job shall pray for you, for I will accept him, that I not deal with you according to your folly. For you have not spoken of me the thing that is right, as my servant Job has.”
Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.”
9 So Eliphaz the Temanite and Bildad the Shuhite and Zophar the Naamathite went and did what the LORD commanded them, and the LORD accepted Job.
Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kama Bwana alivyowaambia; naye Bwana akayakubali maombi ya Ayubu.
10 The LORD restored Job’s prosperity when he prayed for his friends. The LORD gave Job twice as much as he had before.
Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, Bwana akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni.
11 Then all his brothers, all his sisters, and all those who had been of his acquaintance before, came to him and ate bread with him in his house. They comforted him, and consoled him concerning all the evil that the LORD had brought on him. Everyone also gave him a piece of money, and everyone a ring of gold.
Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yote Bwana aliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.
12 So the LORD blessed the latter end of Job more than his beginning. He had fourteen thousand sheep, six thousand camels, one thousand yoke of oxen, and a thousand female donkeys.
Bwana akaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja.
13 He had also seven sons and three daughters.
Tena alikuwa na wana saba na binti watatu.
14 He called the name of the first, Jemimah; and the name of the second, Keziah; and the name of the third, Keren Happuch.
Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki.
15 In all the land were no women found so beautiful as the daughters of Job. Their father gave them an inheritance amongst their brothers.
Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao.
16 After this Job lived one hundred and forty years, and saw his sons, and his sons’ sons, to four generations.
Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne.
17 So Job died, being old and full of days.
Hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee aliyekuwa ameshiba siku.

< Job 42 >