< Acts 15 >

1 Some men came down from Judea and taught the brothers, “Unless you are circumcised after the custom of Moses, you can’t be saved.”
Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo ya Sheria ya Mose, hamtaweza kuokolewa.”
2 Therefore when Paul and Barnabas had no small discord and discussion with them, they appointed Paul, Barnabas, and some others of them to go up to Jerusalem to the emissaries and elders about this question.
Jambo hili lilisababisha ubishi mkubwa, na baada ya Paulo na Barnaba kujadiliana nao, ikaamuliwa Paulo na Barnaba pamoja na waumini kadhaa wa lile kanisa la Antiokia waende Yerusalemu kuwaona wale mitume na wazee kuhusu jambo hilo.
3 They, being sent on their way by the assembly, passed through both Phoenicia and Samaria, declaring the conversion of the Gentiles. They caused great joy to all the brothers.
Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.
4 When they had come to Jerusalem, they were received by the assembly and the emissaries and the elders, and they reported everything that God had done with them.
Walipofika Yerusalemu walikaribishwa na kanisa, mitume na wazee; nao wakawapa taarifa juu ya yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
5 But some of the sect of the Pharisees who believed rose up, saying, “It is necessary to circumcise them, and to command them to keep the Torah of Moses.”
Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata Sheria ya Mose.”
6 The emissaries and the elders were gathered together to see about this matter.
Basi, mitume na wazee walifanya mkutano maalum wa kuchunguza jambo hilo.
7 When there had been much discussion, Peter rose up and said to them, “Brothers, you know that a good while ago God made a choice amongst you that by my mouth the nations should hear the word of the Good News and believe.
Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama, akasema, “Ndugu zangu, ninyi mnafahamu kwamba hapo awali Mungu alipenda kunichagua mimi miongoni mwenu niihubiri Habari Njema, ili watu wa mataifa wapate kusikia na kuamini.
8 God, who knows the heart, testified about them, giving them the Holy Spirit, just like he did to us.
Naye Mungu anayejua mioyo ya watu, alithibitisha kwamba amewakubali kwa kuwapa nao Roho Mtakatifu kama alivyotupa sisi.
9 He made no distinction between us and them, cleansing their hearts by faith.
Hakufanya ubaguzi wowote kati yetu na wao; aliitakasa mioyo yao kwa imani.
10 Now therefore why do you tempt God, that you should put a yoke on the neck of the disciples which neither our fathers nor we were able to bear?
Sasa basi, kwa nini kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hao waumini mzigo ambao wala babu zetu, wala sisi hatukuweza kuubeba?
11 But we believe that we are saved through the grace of the Lord Yeshua, just as they are.”
Isiwe hivyo, ila tunaamini kwamba, sisi kama vile wao, tunaokolewa kwa njia ya neema ya Bwana Yesu.”
12 All the multitude kept silence, and they listened to Barnabas and Paul reporting what signs and wonders God had done amongst the nations through them.
Kikundi chote kilikaa kimya, kikawasikiliza Barnaba na Paulo wakieleza miujiza na maajabu ambayo Mungu alitenda kwa mikono yao kati ya watu wa mataifa mengine.
13 After they were silent, Jacob answered, “Brothers, listen to me.
Walipomaliza kuongea, Yakobo alianza kusema: “Ndugu zangu, nisikilizeni!
14 Simeon has reported how God first visited the nations to take out of them a people for his name.
Simoni ameeleza jinsi Mungu hapo awali alivyojishughulisha na watu wa mataifa mengine, akachagua baadhi yao wawe watu wake.
15 This agrees with the words of the prophets. As it is written,
Jambo hili ni sawa kabisa na maneno ya manabii, kama Maandiko Matakatifu yasemavyo:
16 ‘After these things I will return. I will again build the tabernacle of David, which has fallen. I will again build its ruins. I will set it up
Baada ya mambo haya nitarudi. Nitaijenga tena ile nyumba ya Daudi iliyoanguka; nitayatengeneza magofu yake na kuijenga tena.
17 that the rest of men may seek after the Lord: all the Gentiles who are called by my name, says the Lord, who does all these things.’
Hapo watu wengine wote, watu wa mataifa yote niliowaita wawe wangu, watamtafuta Bwana.
18 “All of God’s works are known to him from eternity. (aiōn g165)
Ndivyo asemavyo Bwana, aliyefanya jambo hili lijulikane tangu kale. (aiōn g165)
19 Therefore my judgement is that we don’t trouble those from amongst the Gentiles who turn to God,
“Kwa hiyo, uamuzi wangu ni huu: tusiwataabishe watu wa mataifa wanomgeukia Mungu.
20 but that we write to them that they abstain from the pollution of idols, from sexual immorality, from what is strangled, and from blood.
Bali tuwapelekee barua kuwaambia wasile vyakula vilivyotiwa najisi kwa kutambikiwa sanamu za miungu; wajiepushe na uasherati; wasile mnyama yeyote aliyenyongwa, na wasinywe damu.
21 For Moses from generations of old has in every city those who proclaim him, being read in the synagogues every Sabbath.”
Kwa maana kwa muda mrefu maneno ya Mose yamekuwa yakihubiriwa katika kila mji na kusomwa katika masunagogi yote kila siku ya Sabato.”
22 Then it seemed good to the emissaries and the elders, with the whole assembly, to choose men out of their company, and send them to Antioch with Paul and Barnabas: Judah called Barsabbas, and Silas, chief men amongst the brothers.
Mitume, wazee na kanisa lote waliamua kuwachagua watu fulani miongoni mwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Basi, wakamchagua Yuda aitwaye pia Barsaba, na Sila ambao wote walikuwa wanajulikana zaidi kati ya ndugu.
23 They wrote these things by their hand: “The emissaries, the elders, and the brothers, to the brothers who are of the Gentiles in Antioch, Syria, and Cilicia: greetings.
Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni ninyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.
24 Because we have heard that some who went out from us have troubled you with words, unsettling your souls, saying, ‘You must be circumcised and keep the Torah,’ to whom we gave no commandment;
Tumesikia kwamba watu wengine kutoka huku kwetu waliwavurugeni kwa maneno yao, wakaitia mioyo yenu katika wasiwasi. Lakini wamefanya hivyo bila ya idhini yoyote kutoka kwetu.
25 it seemed good to us, having come to one accord, to choose out men and send them to you with our beloved Barnabas and Paul,
Hivyo, tumeamua kwa pamoja kuwachagua watu kadhaa na kuwatuma kwenu pamoja na wapenzi wetu Barnaba na Paulo,
26 men who have risked their lives for the name of our Lord Yeshua the Messiah.
ambao wamehatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
27 We have sent therefore Judah and Silas, who themselves will also tell you the same things by word of mouth.
Kwa hiyo, tunawatuma Yuda na Sila kwenu; hawa watawaambieni wao wenyewe haya tuliyoandika.
28 For it seemed good to the Holy Spirit, and to us, to lay no greater burden on you than these necessary things:
Basi, Roho Mtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwike mzigo zaidi ya mambo haya muhimu:
29 that you abstain from things sacrificed to idols, from blood, from things strangled, and from sexual immorality, from which if you keep yourselves, it will be well with you. Farewell.”
Msile vyakula vilivyotambikiwa sanamu; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”
30 So, when they were sent off, they came to Antioch. Having gathered the multitude together, they delivered the letter.
Baada ya kuwaaga, hao wajumbe walielekea Antiokia ambako waliita mkutano wa waumini, wakawapa hiyo barua.
31 When they had read it, they rejoiced over the encouragement.
Walipoisoma hiyo barua, maneno yake yaliwatia moyo, wakafurahi sana.
32 Judah and Silas, also being prophets themselves, encouraged the brothers with many words and strengthened them.
Yuda na Sila, ambao nao walikuwa manabii, walizungumza na hao ndugu kwa muda mrefu wakiwatia moyo na kuwaimarisha.
33 After they had spent some time there, they were dismissed in peace from the brothers to the emissaries.
Baada ya kukaa huko kwa muda fulani, ndugu wa Antiokia waliwaaga wakiwatakia amani, kisha wakarudi kwa wale waliokuwa wamewatuma.
Lakini Sila aliamua kubaki.
35 But Paul and Barnabas stayed in Antioch, teaching and proclaiming the word of the Lord, with many others also.
Paulo na Barnaba walibaki huko Antiokia kwa muda; wakafundisha na kuhubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
36 After some days Paul said to Barnabas, “Let’s return now and visit our brothers in every city in which we proclaimed the word of the Lord, to see how they are doing.”
Baada ya siku kadhaa, Paulo alimwambia Barnaba, “Turudi tukawatembelee wale ndugu katika kila mji tulikolihubiri neno la Bwana tukajionee jinsi wanavyoendelea.”
37 Barnabas planned to take Yochanan, who was called Mark, with them also.
Barnaba alitaka wamchukue pia Yohane aitwaye Marko.
38 But Paul didn’t think that it was a good idea to take with them someone who had withdrawn from them in Pamphylia, and didn’t go with them to do the work.
Lakini Paulo hakupendelea kumchukua Marko, ambaye awali aliwaacha kule Pamfulia na kukataa kushiriki katika kazi yao.
39 Then the contention grew so sharp that they separated from each other. Barnabas took Mark with him and sailed away to Cyprus,
Basi kukatokea ubishi mkali kati yao, na wakaachana. Barnaba akamchukua Marko, wakapanda meli kwenda Kupro.
40 but Paul chose Silas and went out, being commended by the brothers to the grace of God.
Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.
41 He went through Syria and Cilicia, strengthening the assemblies.
Katika safari hiyo alipitia Siria na Kilikia akiyaimarisha makanisa.

< Acts 15 >