< 2 Corinthians 7 >

1 Having therefore these promises, beloved, let’s cleanse ourselves from all defilement of flesh and spirit, perfecting holiness in the fear of God.
Wapendwa wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizi, na tujitakase wenyewe kwa kila jambo ambalo linatufanya kuwa wachafu katika miili yetu na katika roho. Na tuutafute utakatifu katika hofu ya Mungu.
2 Open your hearts to us. We wronged no one. We corrupted no one. We took advantage of no one.
Fanyeni nafasi kwa ajili yetu! Hatujamkosea mtu yeyote. Hatukumdhuru mtu yeyote. Hatujajinufaisha kwa faida ya mtu yeyote.
3 I say this not to condemn you, for I have said before that you are in our hearts to die together and live together.
Nasema hili siyo kwa kuwalaumu. Kwa kuwa nimeshasema kwamba mmo mioyoni mwetu, kwetu sisi kufa pamoja na kuishi pamoja.
4 Great is my boldness of speech towards you. Great is my boasting on your behalf. I am filled with comfort. I overflow with joy in all our affliction.
Nina ujasiri mwingi ndani yenu, na ninajivuna kwa ajili yenu. Nimejawa na faraja. Ninajawa na furaha hata katikati ya mateso yetu yote.
5 For even when we had come into Macedonia, our flesh had no relief, but we were afflicted on every side. Fightings were outside. Fear was inside.
Tulikuja Makedonia, miili yetu haikuwa na pumziko. Badala yake, tulipata taabu kwa namna zote kwa kupigwa vita upande wa nje na hofu upande wa ndani.
6 Nevertheless, he who comforts the lowly, God, comforted us by the coming of Titus,
Lakini Mungu, anayefariji waliokata tamaa, alitufariji kwa ujio wa Tito.
7 and not by his coming only, but also by the comfort with which he was comforted in you while he told us of your longing, your mourning, and your zeal for me, so that I rejoiced still more.
Haikuwa kwa ujio wake tu kwamba Mungu alitufariji. ilikuwa pia faraja zile Tito alizopokea kutoka kwenu. Yeye alituambia upendo mkuu mlionao, huzuni yenu, na mlivyokuwa na wasiwasi kwa ajili yangu. Hivyo nimezidi kuwa na furaha zaidi.
8 For though I grieved you with my letter, I do not regret it, though I did regret it. For I see that my letter made you grieve, though just for a while.
Hata ingawa waraka wangu uliwafanya kusikitika, mimi siujutii. lakini ninaujutia wakati nilipoona waraka huo uliwafanya ninyi kuwa na huzuni. lakini mlikuwa na huzuni kwa muda mfupi.
9 I now rejoice, not that you were grieved, but that you were grieved to repentance. For you were grieved in a godly way, that you might suffer loss by us in nothing.
Sasa nina furaha, si kwa sababu mlikuwa na shida, lakini kwa sababu huzuni zenu iliwaleta kwenye toba. Mlipatwa na huzuni ya kiungu, hivyo mliteswa si kwa hasara kwa sababu yetu.
10 For godly sorrow produces repentance leading to salvation, which brings no regret. But the sorrow of the world produces death.
Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu bila ya kuwa na majuto. Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti.
11 For behold, this same thing, that you were grieved in a godly way, what earnest care it worked in you. Yes, what defence, indignation, fear, longing, zeal, and vindication! In everything you demonstrated yourselves to be pure in the matter.
Angalieni huzuni hii ya kiungu ilizalisha azma gani kubwa ndani yenu. Jinsi gani azma ilikuwa kubwa ndani yenu kuthibitisha kuwa hamkuwa na hatia. Kwa jinsi gani uchungu wenu ulivyokuwa mkubwa, hofu yenu, matamanio yenu, bidii yenu, na shauku yenu kuona kwamba haki inapaswa kutendeka! Katika kila jambo mmethibitisha wenyewe kutokuwa na hatia.
12 So although I wrote to you, I wrote not for his cause that did the wrong, nor for his cause that suffered the wrong, but that your earnest care for us might be revealed in you in the sight of God.
Ingawa niliwaandikia ninyi, sikuandika kwa ajili ya mkosaji, wala si kwa mtu aliyeteswa na maovu. Nimeandika ili kwamba udhati wa mioyo yenu kwa ajili yetu ifanywe kujulikana kwenu mbele ya macho ya Mungu.
13 Therefore we have been comforted. In our comfort we rejoiced the more exceedingly for the joy of Titus, because his spirit has been refreshed by you all.
Ni kwa ajili ya hii kwamba tunafarijika. Katika nyongeza ya faraja yetu wenyewe, tunafurahi pia, hata zaidi kwa sababu ya furaha ya Tito, kwa kuwa roho yake iliburudishwa na ninyi nyote.
14 For if in anything I have boasted to him on your behalf, I was not disappointed. But as we spoke all things to you in truth, so our glorying also which I made before Titus was found to be truth.
Kwa kuwa kama nilijivuna kwake kuhusiana na ninyi, sikuwa na aibu. Kinyume chake, kama tu kila neno tulilolisema kwenu lilikuwa kweli, Majivuno yetu kuhusu ninyi kwa Tito yalithibitisha kuwa kweli.
15 His affection is more abundantly towards you, while he remembers all of your obedience, how with fear and trembling you received him.
Upendo wake kwa ajili yenu hata ni mkubwa zaidi, kama akumbukapo utii wenu nyote, jinsi mlivyomkaribisha yeye kwa hofu na kutetemeka.
16 I rejoice that in everything I am confident concerning you.
Ninafurahi kwa sababu nina ujasiri kamili ndani yenu.

< 2 Corinthians 7 >