< Leviticus 7 >

1 And this is the law of the guilt offering: it is most holy.
“‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya hatia, ambayo ni takatifu sana:
2 In the place where they kill the burnt offering shall they kill the guilt offering: and the blood thereof shall he sprinkle upon the altar round about.
Sadaka ya hatia itachinjiwa mahali pale ambapo sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa, nayo damu yake itanyunyizwa pande zote za madhabahu.
3 And he shall offer of it all the fat thereof; the fat tail, and the fat that covereth the inwards,
Mafuta yake yote yatatolewa sadaka: mafuta ya mkia na mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani,
4 and the two kidneys, and the fat that is on them, which is by the loins, and the caul upon the liver, with the kidneys, shall he take away:
figo zote mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo yataondolewa pamoja na hizo figo.
5 and the priest shall burn them upon the altar for an offering made by fire unto the LORD: it is a guilt offering.
Kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia.
6 Every male among the priests shall eat thereof: it shall be eaten in a holy place: it is most holy.
Mwanaume yeyote katika jamaa ya kuhani aweza kuila, lakini lazima iliwe mahali patakatifu; ni takatifu sana.
7 As is the sin offering, so is the guilt offering: there is one law for them: the priest that maketh atonement therewith, he shall have it.
“‘Sheria hii ya sadaka ya hatia ni sawasawa na ile ya sadaka ya dhambi: Nyama ya yule mnyama aliyetolewa sadaka ni ya yule kuhani anayesimamia ibada ya upatanisho.
8 And the priest that offereth any man’s burnt offering, even the priest shall have to himself the skin of the burnt offering which he hath offered.
Kuhani anayetoa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuichukua ngozi ya mnyama yule aliyetolewa iwe yake.
9 And every meal offering that is baken in the oven, and all that is dressed in the frying pan, and on the baking pan, shall be the priest’s that offereth it.
Kila sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni au kupikwa katika sufuria au katika kikaangio itakuwa ya kuhani anayeitoa.
10 And every meal offering, mingled with oil, or dry, shall all the sons of Aaron have, one as well as another.
Nayo kila sadaka ya nafaka, iwe imechanganywa na mafuta au iko kavu, itakuwa ya wana wa Aroni, nayo itagawanywa sawa kati yao.
11 And this is the law of the sacrifice of peace offerings, which one shall offer unto the LORD.
“‘Haya ndiyo masharti kwa ajili ya sadaka ya amani ambayo mtu aweza kuileta kwa Bwana:
12 If he offer it for a thanksgiving, then he shall offer with the sacrifice of thanksgiving unleavened cakes mingled with oil, and unleavened wafers anointed with oil, and cakes mingled with oil, of fine flour soaked.
“‘Ikiwa mtu atatoa sadaka ya amani kwa ajili ya kuonyesha shukrani, pamoja na sadaka hii ya shukrani, atatoa maandazi yasiyotiwa chachu yaliyochanganywa na mafuta, mikate myembamba isiyotiwa chachu iliyopakwa mafuta, maandazi ya unga laini uliokandwa vizuri na kuchanganywa na mafuta.
13 With cakes of leavened bread he shall offer his oblation with the sacrifice of his peace offerings for thanksgiving.
Pamoja na sadaka hii ya amani ya shukrani ataleta sadaka ya maandazi yaliyotengenezwa kwa chachu.
14 And of it he shall offer one out of each oblation for an heave offering unto the LORD; it shall be the priest’s that sprinkleth the blood of the peace offerings.
Ataleta moja ya kila aina ya andazi kama sadaka, matoleo kwa Bwana; hii ni ya kuhani anayenyunyiza damu ya sadaka ya amani.
15 And the flesh of the sacrifice of his peace offerings for thanksgiving shall be eaten on the day of his oblation; he shall not leave any of it until the morning.
Nyama ya sadaka ya amani kwa ajili ya shukrani lazima iliwe siku iyo hiyo inapotolewa; hutabakiza kitu chochote mpaka asubuhi.
16 But if the sacrifice of his oblation be a vow, or a freewill offering, it shall be eaten on the day that he offereth his sacrifice: and on the morrow that which remaineth of it shall be eaten:
“‘Lakini kama sadaka yake ni kwa ajili ya nadhiri au ni sadaka ya hiari, sadaka hiyo italiwa siku hiyo inapotolewa, lakini chochote kinachobakia kinaweza kuliwa kesho yake.
17 but that which remaineth of the flesh of the sacrifice on the third day shall be burnt with fire.
Nyama yoyote ya sadaka inayobaki mpaka siku ya tatu lazima iteketezwe kwa moto.
18 And if any of the flesh of the sacrifice of his peace offerings be eaten on the third day, it shall not be accepted, neither shall it be imputed unto him that offereth it: it shall be an abomination, and the soul that eateth of it shall bear his iniquity.
Kama nyama yoyote ya sadaka ya amani italiwa siku ya tatu, Bwana hataikubali. Haitahesabiwa kwake huyo aliyeitoa, kwa kuwa ni najisi. Mtu atakayekula sehemu yake yoyote atahesabiwa hatia.
19 And the flesh that toucheth any unclean thing shall not be eaten; it shall be burnt with fire. And as for the flesh, every one that is clean shall eat thereof:
“‘Nyama ile inayogusa chochote ambacho ni najisi kwa kawaida ya ibada kamwe haitaliwa, ni lazima iteketezwe kwa moto. Kuhusu nyama nyingine, mtu yeyote aliye safi kwa kawaida ya ibada anaweza kuila.
20 but the soul that eateth of the flesh of the sacrifice of peace offerings, that pertain unto the LORD, having his uncleanness upon him, that soul shall be cut off from his people.
Lakini kama mtu yeyote najisi akila nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Bwana, huyo mtu lazima akatiliwe mbali na watu wake.
21 And when any one shall touch any unclean thing, the uncleanness of man, or an unclean beast, or any unclean abomination, and eat of the flesh of the sacrifice of peace offerings, which pertain unto the LORD, that soul shall be cut off from his people.
Kama mtu yeyote akigusa kitu kilicho najisi, iwe ni uchafu wa mwanadamu, au mnyama najisi, au kitu chochote kilicho najisi, kitu cha kuchukiza, kisha akala nyama yoyote ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Bwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.’”
22 And the LORD spake unto Moses, saying,
Bwana akamwambia Mose,
23 Speak unto the children of Israel, saying, Ye shall eat no fat, of ox, or sheep, or goat.
“Waambie Waisraeli: ‘Msile mafuta yoyote ya ngʼombe, kondoo wala mbuzi.
24 And the fat of that which dieth of itself, and the fat of that which is torn of beasts, may be used for any other service: but ye shall in no wise eat of it.
Mafuta ya mnyama aliyekutwa amekufa au ameraruliwa na mnyama pori yanaweza kutumika kwa kazi nyingine yoyote, lakini kamwe msiyale.
25 For whosoever eateth the fat of the beast, of which men offer an offering made by fire unto the LORD, even the soul that eateth it shall be cut off from his people.
Mtu yeyote alaye mafuta ya mnyama ambaye ametolewa sadaka kwa Bwana kwa moto ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
26 And ye shall eat no manner of blood, whether it be of fowl or of beast, in any of your dwellings.
Popote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege yeyote wala ya mnyama.
27 Whosoever it be that eateth any blood, that soul shall be cut off from his people.
Ikiwa mtu yeyote atakunywa damu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.’”
28 And the LORD spake unto Moses, saying,
Bwana akamwambia Mose,
29 Speak unto the children of Israel, saying, He that offereth the sacrifice of his peace offerings unto the LORD shall bring his oblation unto the LORD out of the sacrifice of his peace offerings:
“Waambie Waisraeli: ‘Mtu yeyote aletaye sadaka ya amani kwa Bwana ataleta sehemu ya sadaka hiyo kama dhabihu yake kwa Bwana.
30 his own hands shall bring the offerings of the LORD made by fire; the fat with the breast shall he bring, that the breast may be waved for a wave offering before the LORD.
Ataleta sadaka kwa mikono yake mwenyewe iliyotolewa kwa Bwana kwa moto; ataleta mafuta ya huyo mnyama pamoja na kidari, naye atainua hicho kidari mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa.
31 And the priest shall burn the fat upon the altar: but the breast shall be Aaron’s and his sons’.
Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu, lakini kidari kitakuwa cha Aroni na wanawe.
32 And the right thigh shall ye give unto the priest for an heave offering out of the sacrifices of your peace offerings.
Paja la kulia la sadaka zako za amani utampa kuhani kama matoleo.
33 He among the sons of Aaron, that offereth the blood of the peace offerings, and the fat, shall have the right thigh for a portion.
Mwana wa Aroni atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani ndiye atakayepewa paja hilo la kulia kuwa fungu lake.
34 For the wave breast and the heave thigh have I taken of the children of Israel out of the sacrifices of their peace offerings, and have given them unto Aaron the priest and unto his sons as a due for ever from the children of Israel.
Kutoka kwenye sadaka za amani za Waisraeli, mimi Mungu nimepokea kidari kile kilichoinuliwa pamoja na lile paja lililotolewa, nami nimevitoa kwa kuhani Aroni na wanawe kuwa fungu lao la kawaida kutoka kwa Waisraeli.’”
35 This is the anointing-portion of Aaron, and the anointing-portion of his sons, out of the offerings of the LORD made by fire, in the day when he presented them to minister unto the LORD in the priest’s office;
Hii ndiyo sehemu ya sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, ambazo zilitengwa kwa ajili ya Aroni na wanawe siku ile walipowekwa wakfu ili kumtumikia Bwana katika kazi ya ukuhani.
36 which the LORD commanded to be given them of the children of Israel, in the day that he anointed them. It is a due for ever throughout their generations.
Siku ile walipotiwa mafuta, Bwana aliagiza kwamba Waisraeli wawape hili kama fungu lao la kawaida kwa vizazi vijavyo.
37 This is the law of the burnt offering, of the meal offering, and of the sin offering, and of the guilt offering, and of the consecration, and of the sacrifice of peace offerings;
Basi haya ndiyo masharti kuhusu sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, sadaka ya dhambi, sadaka ya hatia, sadaka ya kuwekwa wakfu, na sadaka ya amani,
38 which the LORD commanded Moses in mount Sinai, in the day that he commanded the children of Israel to offer their oblations unto the LORD, in the wilderness of Sinai.
ambayo Bwana alimpa Mose juu ya Mlima Sinai siku ile alipowaagiza Waisraeli walete sadaka zao kwa Bwana, katika Jangwa la Sinai.

< Leviticus 7 >