< Isaiah 11 >

1 And there shall come forth a shoot out of the stock of Jesse, and a branch out of his roots shall bear fruit:
Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese, kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.
2 And the spirit of the LORD shall rest upon him, the spirit of wisdom and understanding, the spirit of counsel and might, the spirit of knowledge and of the fear of the LORD;
Roho wa Bwana atakaa juu yake, Roho wa hekima na wa ufahamu, Roho wa shauri na wa uweza, Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana
3 And his delight shall be in the fear of the LORD: and he shall not judge after the sight of his eyes, neither reprove after the hearing of his ears:
naye atafurahia kumcha Bwana. Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake, wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,
4 but with righteousness shall he judge the poor, and reprove with equity for the meek of the earth: and he shall smite the earth with the rod of his mouth, and with the breath of his lips shall he slay the wicked.
bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji, kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia. Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.
5 And righteousness shall be the girdle of his loins, and faithfulness the girdle of his reins.
Haki itakuwa mkanda wake na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.
6 And the wolf shall dwell with the lamb, and the leopard shall lie down with the kid; and the calf and the young lion and the fatling together; and a little child shall lead them.
Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, naye chui atalala pamoja na mbuzi, ndama, mwana simba na ngʼombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja, naye mtoto mdogo atawaongoza.
7 And the cow and the bear shall feed; their young ones shall lie down together: and the lion shall eat straw like the ox.
Ngʼombe na dubu watalisha pamoja, watoto wao watalala pamoja, na simba atakula majani makavu kama maksai.
8 And the sucking child shall play on the hole of the asp, and the weaned child shall put his hand on the basilisk’s den.
Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka, naye mtoto mdogo ataweka mkono wake kwenye kiota cha fira.
9 They shall not hurt nor destroy in all my holy mountain: for the earth shall be full of the knowledge of the LORD, as the waters cover the sea.
Hawatadhuru wala kuharibu juu ya mlima wangu mtakatifu wote, kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana kama maji yajazavyo bahari.
10 And it shall come to pass in that day, that the root of Jesse, which standeth for an ensign of the peoples, unto him shall the nations seek; and his resting place shall be glorious.
Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu.
11 And it shall come to pass in that day, that the Lord shall set his hand again the second time to recover the remnant of his people, which shall remain, from Assyria, and from Egypt, and from Pathros, and from Cush, and from Elam, and from Shinar, and from Hamath, and from the islands of the sea.
Katika siku hiyo Bwana atanyoosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi na kutoka visiwa vya baharini.
12 And he shall set up an ensign for the nations, and shall assemble the outcasts of Israel, and gather together the dispersed of Judah from the four corners of the earth.
Atainua bendera kwa mataifa na kuwakusanya Waisraeli walioko uhamishoni; atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika kutoka pembe nne za dunia.
13 The envy also of Ephraim shall depart, and they that vex Judah shall be cut off: Ephraim shall not envy Judah, and Judah shall not vex Ephraim.
Wivu wa Efraimu utatoweka, na adui wa Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamwonea Yuda wivu, wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu.
14 And they shall fly down upon the shoulder of the Philistines on the west; together shall they spoil the children of the east: they shall put forth their hand upon Edom and Moab; and the children of Ammon shall obey them.
Watawashukia katika miteremko ya Wafilisti hadi upande wa magharibi, kwa pamoja watawateka watu nyara hadi upande wa mashariki. Watawapiga Edomu na Moabu, na Waamoni watatawaliwa nao.
15 And the LORD shall utterly destroy the tongue of the Egyptian sea; and with his scorching wind shall he shake his hand over the River, and shall smite it into seven streams, and cause men to march over dryshod.
Bwana atakausha ghuba ya bahari ya Misri; kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake juu ya Mto Frati. Ataugawanya katika vijito saba ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.
16 And there shall be an highway for the remnant of his people, which shall remain, from Assyria; like as there was for Israel in the day that he came up out of the land of Egypt.
Itakuwepo njia kuu kwa mabaki ya watu wake wale waliosalia kutoka Ashuru, kama ilivyokuwa kwa Israeli walipopanda kutoka Misri.

< Isaiah 11 >